Mwana wa Nuru
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 589
- 412
Tatizo naona mtoa mada ni Almaamuma! hawezi kutofautisha kiarabu na uislamu.Hajui kuwa kiarabu ni lugha na kilikuwapo hata kabla ya uislamu kufikiriwa kuwepo.Hajui kuwa hata hicho kitabu anachokisemea kiliandikwa lini na kwa jinsi gani.Yamkini hajui hata kilichizisibu nakala zake halisi za kale zimefikwa na madhira gani. Sijui kama anajua hata ile hadithi inayoonesha uchina kuwa ni kitovu cha elimu wakati wa mtume na si arabuni au ulaya. Labda pia ana usubi hata kwa mambo ya kisiasa na kijamii ya Tanzania kwani utofautishaji wake wa awamu za uongozi wa nchiunatia shaka. Nyerere na Kikwete kamwe hawatalingana hata kwa namna ya kuwaza kwao tu. Namshauri mtoa mada asisumbuke na suala la udini kwani si issue kwa sasa,burning issue ni uchumi wetu unavyokua kwa wageni(wawekezaji) na kushuka kwetu kila mara chini ya uongozi thabiti wa chama cha mapinduzi. Mgeni wetu anaitwa Barack Hussein Obama hivyo labda ni mwislamu au wazazi wake, lakini haituhusu.