Dar-Es-Salaam: Obama Umedanganywa!

Dar-Es-Salaam: Obama Umedanganywa!

Mkuu nakushangaa sana, em kapitie dictionary yako vizuri au hujui neno "harbour" unaweza ukatumia kama "haven" vile vile?? Harbour of Peace na Haven of Peace na Nyumba ya amani ni kitu kile kile.. au we hapo ulielewa vipi??
Em kapitie dictionary vizuri basi alafu utarudi tena, na note kua inaandikwa "harbour" ama "harbor" British n American respectively, hiyo "Habour" yako ni Programming language sio neno la kiingereza. Kwa hiyo jamaa alikua sana kabisa

Bandari. Ukiikubali maana hiyo ina maana unakataa kuwa Dar Es Salaam si Kiarabu. Wakati aliyetoa jina hilo ni Mwaarabu. Na nnakuhakikishia Mwaarabu hatoi jina hilo ila anai"quote" Qur'an na Qur'an haikumaanisha "bandari...".
 
Mji wetu ni Mzizima, vingine ni mbwembwe tu na ukoloni mambo leo
 
Kuhusu dini.ni vizuri kujadili kuhusu dini, To this day,the great majority of the human race accept this pagan doctirne of an already fallen race[Babylonian,Hebrew]in preference to the Solar God concept of a Creator of Good which sheds His light and heat upon the world to create all that is good for the needs of all Creation.
 
Sitaki kuwa mdini...ukweli katika upekuzi wangu Dar Es Salaam its an arabic word same as Darussalam....guys wikipedia is created for you.
 
Uislaam ni "global", Qur'an imeandikwa kiarabu, lugha kubwa kuliko zote uzijuazo.

Jee, unajuwa kuwa hata Kiswahili unachotumia asilimia kubwa ya maneno yake yametokana na Kiarabu? jiulize kwa nini?

Kiarabu na Kiingereza (uislam na ukristo) ni ukoloni tu (kujifunza na kuvijua sio kosa),kwa Mtanzania wala sio vitu vya kujivunia..Tujivunie kiswahili ambacho kina chembe chembe za damu kutokana na ukoloni ambazo siku moja mungu bariki zitafutika kutokana na maendeleo ya lugha..Bongo watu wakitaja hizo Dini utadhani kama kitu muhimu sana kwetu,Tuimarishe mambo ya maendeleo ya Elimu,Afya,Uchumi na mshikamano wetu ili tusonge mbele..

Ukweli ni kwamba kila nchi inataka lugha yake iwe global na Waarabu walidhani lugha ya kiarabu itaimarika kwa kutokuitafsiri Qur'an,lakini kumbe dini sio njia imara ya kuendeleza kugha,.Uchumi na factor nyingine kama elimu zaweza kuendeleza lugha na sio dini peke yake.Niliwahi kusikia kua watu wa TZ kanda fulani walipendekeza lugha yao iwe lugha ya Taifa TZ kwa vile wao wako wengi na lugha yao inatumika eneo kubwa la TZ:ila ili FAIL kama kilivyo FAIL kiarabu hapa TZ na kwingineko.
 
Wakti namsikiliza Mheshimiwa mgeni wetu adhyim, Rais wa Muungano wa Mataifa ya Kimerekani (USA), Barack Hussein Obama, nilimsikia alipoitaja Dar Es Salaam, aliitafsiri kuwa ni "Habour of Peace" (labda iwe ung'eng'e ulinipiga chenga). Mheshimiwa kama ulitafsiriwa hivyo, wamekosea watafsiri wako, kama ni wewe mwenyewe, kwani naelewa kuwa unakijuwa Kiswahili kwa kiasi fulani, basi umekosea.

Maana halisi ya Dar Es Salaam, ni ngumu sana kuitafsiri ikiwa huupendi Uislaam na umeaminishwa na wabaguzi wa ujinga, kwani Dar Es Salaam inapatikana ndani ya Qur'an ikimaanisha ni moja kati ya pepo au kwa maulamaa wengine, moja kati ya milango ya kuingilia peponi "Baab Dar as Salaam", kwa maana moja au nyingine inamaanisha "haven of Peace" au "Nyumba" ya amani au kwa maana halisi "Pepo" ya amani.

Aliyekufunda kuwa Dar Es Salaam ni "Habour of Peace" hakukutendea haki wewe wala hakututendea haki sisi wa Dar Es Salaam.

Kwa kusherehesha; Dar Es Salaam si jina geni kwa miji ya duniani na haikuanzia hapa kwetu, kuna nchi nyingi ambazo zina majina ya majiji au miji iitwayo hivyo kwa lafdhi tofauti, maarufu ni Jerusalem, ina maanisha hivyo-hivyo. Nyingine ni Darussalaam, iliyopo Brunei, Ni hiyo hiyo, kama yetu tu.

Mnhhh mnhhh!

Karibu mgeni wetu.

Zomba,Unapotaka kuzungumzia kitu au neno la lugha fulani ni vizuri ukatumia KAMUSI ya lugha husika,Maana neno likiwa kwenye kitabu kitakatifu chochote,mfano Qur'an au Biblia; huwezi kupata maana kusudiwa ya kukubalika na jamii zote,Kamusi ndio 'reference' ya mambo ya academic,Usilazimishe watu wakafanye reference kwenye Qur'an au Biblia.Maandiko yaliyoko huko kwenye vitabu tunavyoviita Vitabu vitakatifu ni DOCTRINE tu,sio lazima ukubali na uamini mambo ya Qur'an au Biblia,Mimi nakuomba uwe unatumia General accepted tool ya kuelimisha jamii yoyote kama KAMUSI ya lugha husika ili hoja zako zipate mshiko.Maana umetoa hoja nzuri ila umeichafua kidogo,Nadhani umenipata hapo..
 
Bandari. Ukiikubali maana hiyo ina maana unakataa kuwa Dar Es Salaam si Kiarabu. Wakati aliyetoa jina hilo ni Mwaarabu. Na nnakuhakikishia Mwaarabu hatoi jina hilo ila anai"quote" Qur'an na Qur'an haikumaanisha "bandari...".
Sasa unalazimisha tufuate maana ya Qur'an kwenye jina la mji? kwani lazima?
 
Wakti namsikiliza Mheshimiwa mgeni wetu adhyim, Rais wa Muungano wa Mataifa ya Kimerekani (USA), Barack Hussein Obama, nilimsikia alipoitaja Dar Es Salaam, aliitafsiri kuwa ni "Habour of Peace" (labda iwe ung'eng'e ulinipiga chenga). Mheshimiwa kama ulitafsiriwa hivyo, wamekosea watafsiri wako, kama ni wewe mwenyewe, kwani naelewa kuwa unakijuwa Kiswahili kwa kiasi fulani, basi umekosea.

Maana halisi ya Dar Es Salaam, ni ngumu sana kuitafsiri ikiwa huupendi Uislaam na umeaminishwa na wabaguzi wa ujinga, kwani Dar Es Salaam inapatikana ndani ya Qur'an ikimaanisha ni moja kati ya pepo au kwa maulamaa wengine, moja kati ya milango ya kuingilia peponi "Baab Dar as Salaam", kwa maana moja au nyingine inamaanisha "haven of Peace" au "Nyumba" ya amani au kwa maana halisi "Pepo" ya amani.

Aliyekufunda kuwa Dar Es Salaam ni "Habour of Peace" hakukutendea haki wewe wala hakututendea haki sisi wa Dar Es Salaam.

Kwa kusherehesha; Dar Es Salaam si jina geni kwa miji ya duniani na haikuanzia hapa kwetu, kuna nchi nyingi ambazo zina majina ya majiji au miji iitwayo hivyo kwa lafdhi tofauti, maarufu ni Jerusalem, ina maanisha hivyo-hivyo. Nyingine ni Darussalaam, iliyopo Brunei, Ni hiyo hiyo, kama yetu tu.

Mnhhh mnhhh!

Karibu mgeni wetu.

mkuu zomba, ni busara zaidi kufanya research kwanza kabla ya ku-post habari yoyote hapa jukwaani. Acha kupotosha ummah.
 
mkuu zomba, ni busara zaidi kufanya research kwanza kabla ya ku-post habari yoyote hapa jukwaani. Acha kupotosha ummah.

Naam, nimefanya research na ndio maana nikaandika, jee, wewe umeshaanza kufanya research yako uje kutuwekea hapa kama unapinga?
 
Huyu jamaa bwana! Kwa hiyo unataka kusema wadaidizi wa Obama ni mbumbumbu,wewe ndo mwerevu.toa ujinga wako hapa
 
Back
Top Bottom