Mimi naona majibu rahisi ya 'aghali sana' bila kufafanua ughali sana wake ni upi, ni majibu ya 'wabunge vihiyo' wanaojibu bila utafiti ama kwa ghilba za ubinafsi.
Maana kuna nchi, hii teknolojia wanayo kitambo sana.
Wao wameweza wana nini na sisi tumeshindwa tunanini?
Maana ingelikuwa ni ghali kama tunavyopotoshwa, waIsraeli wasingelikuwa na ubavu wa kuyachuja kutosheleza hadi ziada ya kumwagilia mashamba.
WaTz ama waAfrika sijui huwa kwanini tunapenda kubweteka hadi akili, maana zamani ilikuwa kuongelea kwa mfano treni za umeme kwenye nchi kama ya kwetu hii, unaonekana mtu kama unaota, lakini kumbe dhamira chanya ikiwepo hakuna linaloshindikana!