Uchaguzi 2020 Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano

Uchaguzi 2020 Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wamewashika watu watatu zaidi kwa tuhuma za kuwashawishi watu kuandamana.

Walikamatwa ni pamoja na Baunsa wa aliyekuwa Mbunge Kawe, Halima Mdee na wengine wawili ambao wamekamatwa kuzuia vurugu zinazopanga kufanyika.

Kamanda Mambosasa amesema watu hao walikamatwa wakiwa katika vikao vya kupanga vurugu hizo ambazo zimepangwa kufanyika leo.

Waliokuwa wanatakiwa kuandamana wametakiwa kuchoma matairi barabarani, kuchoma magari, vituo vya mafuta na masoko wameahidiwa pesa.

Pia watu wanaotumika kushawishi wanaambiwa wawatafute vijana wasio waoga, wanaotumia dawa za kulevya.

PIA SOMA:
= > Uchaguzi 2020 - ACP Mambosasa: Tunawashikilia Mbowe, Lema na Boniface Jacob kwa kuhatarisha maisha ya Raia na mali zao
 
Halafu wanakosea wanaposema kwamba ni vurugu wakati ni maandamano ya amani kudai Uchaguzi huru na wa haki, Kudai Tume huru ya Uchaguzi, Uchaguzi uandaliwe sababu kilichofanyika Tanzania tarehe 28 hakikuw na sifa za kuitwa uchaguzi
 
Kwamba........
Waliokuwa wanatakiwa kuandamana wametakiwa kuchoma matairi barabarani, kuchoma magari, vituo vya mafuta na masoko wameahidiwa pesa.

Pia watu wanaotumika kushawishi wanaambiwa wawatafute vijana wasio waoga, wanaotumia dawa za kulevya..🤨😲😲
Duhhhhhhh....
Nimejikuta nasikitika sana
 
Halafu wanakosea wanaposema kwamba ni furugu wakati ni maandamano ya amani kudai uchaguzi huru na wa haki, Kudai tume huru ya uchaguzi, Uchaguzi uandaliwe sababu kilichofanyika tanzania tarehe 28 hakikuw na sifa za kuitwa uchaguzi
Nenda kwenye maandamano sasa Kama wewe upo online unachat muda huu nani ataandamana sasa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa imekuwa kusema uwongo ndio utamaduni mpya wa Kitanzania, watu wanashindwa kujiamini, sasa hawa wamepewa vyeo vya fadhila au ujamaa au kujuana bila ya kutathmini elimu yao au utendaji wao.

Sasa hii inakuwa ni aibu hata waliokuwa si Watanzania wanaona wazi kuwa Watanzania walishwa uongo japo hakuna anaeuamini isipokuwa wanaousema.

Hivi tumekuwa Taifa linaloongozwa na waongo ??? Maana maajabu yote yapo Tanzania.
 
Kwamba........
Waliokuwa wanatakiwa kuandamana wametakiwa kuchoma matairi barabarani, kuchoma magari, vituo vya mafuta na masoko wameahidiwa pesa.
Pia watu wanaotumika kushawishi wanaambiwa wawatafute vijana wasio waoga, wanaotumia dawa za kulevya..[emoji2955][emoji44][emoji44]
Duhhhhhhh....
Nimejikuta nasikitika sana
Na hivi vyote vimegundulika haraka sana kabla muda wa maandamano[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

"Ira kuhusu Mtwara bado jeshi retu rinafuatiria kujua kama kweri watu wariuawa au si kweri ni uchochezi tu wa kuwatia hofu Watanzania"
 
Back
Top Bottom