Dar es salaam yashika nafasi ya tano duniani

Dar es salaam yashika nafasi ya tano duniani

Baraka255

Member
Joined
Jun 25, 2014
Posts
73
Reaction score
14
Sijajua serikali imejipangaje katika mpango huu. KITABU cha Takwimu za Dunia kinachotolewa kila mwaka na Jarida la The Economist kimetoka mwaka huu na kuna baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kutufikirisha kama Taifa.

Kwa mfano, The Economist wametaja jiji la Dar es Salaam kama la tano duniani miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi duniani. Katika eneo lote la Afrika Mashariki, Dar es Salaam inazidiwa na Kampala, Uganda pekee ambayo imeshika nafasi ya tatu.

Takwimu hizo, pamoja na mambo mengine, zinaonyesha pia ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha kupata watoto –ambapo mwanamke mmoja anaweza kupata hadi watoto wanne. Imeshika nafasi ya 11.

Mwaka 2050, linasema jarida hilo, Tanzania itakuwa mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu duniani. Barani Afrika, Tanzania itakuwa ya tatu kwa idadi kubwa ya watu huku ikiwa ya 13 duniani.

Kwa sasa, jarida hilo linasema, Tanzania imeizidi Kenya kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika makazi duni (slums); ikichagizwa na ongezeko la idadi kubwa ya watu wanaohama kutoka vijijini na kuja mijini.

Swali langu ni je Serikali ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania wamejipangaje na mabadiliko haya hasa katika swala zima la miundombinu?
 
Ndio maana tunasema madaraka yagatuliwe kwa tawala za mikoa ili kusawazisha maendeleo ya kiuchumi nchi nzima, watu wanaokuja Dar watapungua kwa vile kila mkoa utakua na fursa ya kujiendeleza kiuchumi. CDM hoyeee!
 
Kati ya mambo nisiyoyapenda ni hiyo sera ya majimbo haijawahi kufanyakazi Afrika inaweza kutuletea matatizo makubwa sana kuliko faida tunazotarajia.

Kenya, South Africa, Nigeria na nchi zote za G8 zinatumia mfumo wa ugatuzi kwa namna moja au nyingine (either through devolution au federalism). Huu mfumo umechangia vikubwa kwenye maendeleo ya nchi nyingi sana. Sioni wasiwasi wako uko wapi???!
 
Mawazo. mazuri lazima yatoke kwao.Kama mikoa kikanda ingepewa madaraka ya kujiendesha bila kuingiliwa na serkl kuu;na kwa kutumia sehemu kubwa Ya raslimali zzipatikazo huko;vijana wasingelikimbilia DSM kufanya mini?
 
Utawala wa kikanda au majimbo ni mzuri sana. Huwa unaharakisha maendeleo. Tumeona sehemu nyingi.Tanzania ni kama tunachelewa kuamua hili!
 
Kati ya mambo nisiyoyapenda ni hiyo sera ya majimbo haijawahi kufanyakazi Afrika inaweza kutuletea matatizo makubwa sana kuliko faida tunazotarajia.

ila ndugu siyo kwasababu flani kashindwa na wewe ushindwe. hivi si ni Tanzania inajisifu kuwa na aina pekee ya Muungano ulimwenguni?
 
Boko haram huku Nigeria imeletwa na sera ya majimbo au hata hili limekushinda.Kenya unaonaje ukabila.Nakwambia siku CDM ikikamata dola na kulazimisha sera ya majimbo utasikia Mtwara inataka kujitenga kwasababu ina gesi,kabla haujakaa vizuri kanda ya ziwa watasema wanataka usemi zaidi kwakuwa wanachangia zaidi na kadhalika na kadhalika.......

Kenya, South Africa, Nigeria na nchi zote za G8 zinatumia mfumo wa ugatuzi kwa namna moja au nyingine (either through devolution au federalism). Huu mfumo umechangia vikubwa kwenye maendeleo ya nchi nyingi sana. Sioni wasiwasi wako uko wapi???!
 
Ndugu yangu Mapi wanasiasa ni watu wa ajabu sana usipokuwa makini unaweza kujikuta unashabikia jambo bovu bila kujijua.

ila ndugu siyo kwasababu flani kashindwa na wewe ushindwe. hivi si ni Tanzania inajisifu kuwa na aina pekee ya Muungano ulimwenguni?
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu uchafu tunashika namba ngapi?
 
Ndugu yangu Mapi wanasiasa ni watu wa ajabu sana usipokuwa makini unaweza kujikuta unashabikia jambo bovu bila kujijua.

sijaisoma hiyo sera ya majimbo, ila unaweza nisaidia faida, hasara zake na uwezekano wake wa kufeli hapa kwetu?

ili tujaribu kupima kama wadau wa nchi kujua tutakapoelekea?
 
Kiongozi, ugatuzi ni nini kwanza?

Kenya, South Africa, Nigeria na nchi zote za G8 zinatumia mfumo wa ugatuzi kwa namna moja au nyingine (either through devolution au federalism). Huu mfumo umechangia vikubwa kwenye maendeleo ya nchi nyingi sana. Sioni wasiwasi wako uko wapi???!
 
Naona Ngogo ana hoja inayohitaji umakini sana. Sijafahamu sera ya majimbo ya CDM itafanya kazi kwa utaratibu upi. Lakini katika mfumo wowote utakaoundwa wa majimbo, hoja ya Ngogo si ya kuidharau. Tunajenga Tanzania yetu. Hatuhitaji kunakili mfumo wa majimbo kwa mfano kama wa kenya. Badala yake, CDM wachukue somo kwa failures za kenya na nigeria kwa mfano, halafu, mfumo wa majimbo yetu uwe wa aina fulani isiyotoa mwanya wa makundi ya kikabila, kidini ama ki raslimali. Nina imani na vichwa vya CDM, kwamba kwa kuzingatia hoja ya Ngogo, wahakikishe kwamba mapema wanarekebisha muundo wa majimbo yao ili badala ya kutugawa, ilete tia katika uwajibikaji, mipango, matumizi ya raslimali na mgawanyo katika nchi.

Jioni njema

sijaisoma hiyo sera ya majimbo, ila unaweza nisaidia faida, hasara zake na uwezekano wake wa kufeli hapa kwetu?

ili tujaribu kupima kama wadau wa nchi kujua tutakapoelekea?
 
Kiongozi, ugatuzi ni nini kwanza?
Kwa kiingereza inaitwa decentralization. Ni kugawa madaraka kwa serikali za ngazi ya chini kama vile za mikoa au majimbo. Ni mfumo mzuri sana wenye faida nyingi kama ukitekelezeka vizuri!
 
Tatizo hapa sioni nia ya kweli ya kugawa madaraka. Kinachofanyika ni maneno tu. Utasikia eti ccm wanasema wapinzania wana uroho wa madaraka, wakati wao ndio wanathibitisha uroho huo kwa kuhujumu upinzani makusudi ili waendelee kutawala hata kama hawatakiwi, na pia kwa kuzidi kucentralize maamuzi bila kujali ongezeko la population na idadi kuwa ya wataalamu nchini.

Decentralization kwa Tanzania itakuwa nguvu kwa sababu si agenda wala nia ya ccm na ndiyo sababu bado wanapma raisi madaraka ya teuzi zote na kuweka walilnzi wa matakwa yake kila mkoa na wilaya (RCs and DCs). Sana sana wakiona pressure watadandia hoja na kuifanya ovyoovyo na hata kuleta shida kubwa kwa nchi kama katiba waliyoghushi.

Lakini kwa sasa wanaikataa kwa ajili lya uroho wa madaraka, udictator na uchakachuaji wa maamuzi, na usalama wa itikadi fisadi.

Kikubwa, decentralization inatakiwa iwe planned vizuri ili kuepuka mgawanyiko na upotevu wa dhana ya utaifa.

Kwa kiingereza inaitwa decentralization. Ni kugawa madaraka kwa serikali za ngazi ya chini kama vile za mikoa au majimbo. Ni mfumo mzuri sana wenye faida nyingi kama ukitekelezeka vizuri!
 
Back
Top Bottom