Baraka255
Member
- Jun 25, 2014
- 73
- 14
Sijajua serikali imejipangaje katika mpango huu. KITABU cha Takwimu za Dunia kinachotolewa kila mwaka na Jarida la The Economist kimetoka mwaka huu na kuna baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kutufikirisha kama Taifa.
Kwa mfano, The Economist wametaja jiji la Dar es Salaam kama la tano duniani miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi duniani. Katika eneo lote la Afrika Mashariki, Dar es Salaam inazidiwa na Kampala, Uganda pekee ambayo imeshika nafasi ya tatu.
Takwimu hizo, pamoja na mambo mengine, zinaonyesha pia ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha kupata watoto –ambapo mwanamke mmoja anaweza kupata hadi watoto wanne. Imeshika nafasi ya 11.
Mwaka 2050, linasema jarida hilo, Tanzania itakuwa mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu duniani. Barani Afrika, Tanzania itakuwa ya tatu kwa idadi kubwa ya watu huku ikiwa ya 13 duniani.
Kwa sasa, jarida hilo linasema, Tanzania imeizidi Kenya kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika makazi duni (slums); ikichagizwa na ongezeko la idadi kubwa ya watu wanaohama kutoka vijijini na kuja mijini.
Swali langu ni je Serikali ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania wamejipangaje na mabadiliko haya hasa katika swala zima la miundombinu?