Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,033
Reaction score
723



Tulikotoka

Ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina la Mfugale ulioanza miaka miwili iliyopita umegharimu Sh bilioni 92 hadi kukamilika kwake, huku Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) likichangia Sh bilioni 26. Jina la Mfugale limetokana na jina la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale, ambaye Rais Magufuli alisema amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini na kumpa heshima ya kulitunuku daraja hilo jina lake.

Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 20 1 5 kati ya Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd. Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi huku akiwataka wananchi, viongozi wa siasa kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi huo wenye historia ya kipekee nchini.


d11dd1c9e4022b37aae7a799d987f466.JPG


Rais Magufuli amewasili katika eneo hilo zinapokutana barabara za Mandela na Nyerere na amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

RC Makonda

Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport

"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!

Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu

Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"

Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi

Mkurugenzi Mtendaji TANROADs

Mwaka 2008, Tanzania iliandaa ‘Master Plan’ ya kupunguza msongamano jijini Dar. 2013 Japan wakajitokeza kuwa watatusaidia kujenga daraja hili; 2014 ilitangazwa tenda! Wazabuni walikuja na gharama kubwa

Japan iliongeza ufadhili hadi Bilioni 103 mwaka 2015 Machi, Mkandarasi mmoja alikuja lakini gharama zake zilikuwa mara mbili zaidi. Tulifanya ‘Selective Tendering’ ambapo mkandarasi aliyejenga daraja hili alipatikana

Daraja hili limejengwa kwa nguzo kubwa 26; zimekaa juu ya Piles 133. Daraja lina urefu wa zaidi ya km 1. Linaweza kubeba tani 180 kwa wakati mmoja. Daraja hili linaweza kutumika kwa zaidi ya miaka 100. Limejengwa kwa jumla ya Sh. Bilioni 92

Tunao mkakati wa kujenga BRT ya kutoka mjini(CBD) hadi Gongo la Mboto katika awamu ya 3

Balozi wa Japan

Naamini watanzania wote wamefurahi kuona Flyover ya kwanza nchini Tanzania. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Nafarijika kuwa nikiwa narudi Japan nitatumia ‘Mfugale Flyover’

Eng. Ninatubu Lema(ERB)

Mhandisi Patrick Aaron Lipilima Mfugale ametumikia taaluma ya Uhandisi kwa miaka 41
- Alizaliwa Ifunda, Iringa na alikamaliza Sekondari mwaka 1975. Alipata 1st Degree nchini India, Masters nchini Uingereza
- Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi 1977

Mfugale ametumia muda wake mwingi wa kazi kama Mtaalamu wa Madaraja. Alibuni daraja la Malagarasi; ameshiriki ktk ujenzi wa madaraja ya Mkapa, Umoja, Rusumo, Kikwete, Nyerere, Mto Sibiti, Kilombero na mengine mengi (zaidi ya 1,400 nchini)

Mhandisi Patrick Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS; leo atapata heshima kubwa sana kwa Flyover ya kwanza Tanzania kupewa jina lake!

Elias J. Kwandikwa

Mradi huu jumla umegharimu Bilioni 106. Serikali ya Tanzania imegharimia kodi zote. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Toka Flyover imeanza kutumika, msongamano eneo la TAZARA umepungua kwa kiwango kikubwa

Miradi inayotarajiwa jijini Dar kwa kushirikiana na JICA:
> Upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge
> Ujenzi wa Daraja la Gerezani (Kariakoo)

Rais Magufuli

Natoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao kufuatia ajali ya #MVNyerere na kuwaombea majeruhi uponyaji wa haraka. Nawashukuru watanzania kwa mshikamano walioonyesha

Ajali hii ya #MVNyerere iwe funzo kwetu. Ajali kama hizi zinaepukika, na zikitokea basi madhara yake yanaweza kuwa madogo kama tukipata funzo kwa kilichotokea

Nawapongeza Wizara ya Ujenzi, TANROADS na Wahandisi washauri kwa kusimamia ujenzi wa #MfugaleFlyover. Daraja limegharimu Bilioni 106.65; Japan wamechangia kiwango kikubwa cha pesa hii, ni marafiki wa kweli kwenye masuala ya maendeleo

Nampongeza Mbarawa ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi wakati ujenzi wa #MfugaleFlyover unaanza

Nakumbuka wakati Daraja la Umoja linaandaliwa kujengwa, nilimwita Mfugale anisaidie design ya Daraja hilo; nilipoipeleka kwa marais wa Tanzania na Msumbiji, ikapitishwa. Wakati wa uzinduzi wala hakutambulishwa

Mwaka 2008 Mfugale na mwenzake walipewa maagizo wakayakataa, Katibu Mkuu wa wakati huo aliwaokoa; mwenzake (marehemu Mjungi) alijiua kwa kujipiga risasi lakini Mfugale alivumilia. Ndo gharama ya kusimamia maadili

Ujenzi wa Flyover ya Ubungo itagharimu Bilioni 247. Itakuwa flyover ya aina yake kwa hapa Dar es Salaam! Wazaramo watasema ‘Ina ghorofa 3’

Tunajenga barabara ya njia 6 kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa Sh. Bilioni 140 na fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania. Kutakuwa pia na njia ndogo 2 (service road). Bomoabomoa ya Kimara ilizingatia sheria!

Katika #MfugaleFlyover, nataka zifungwe kamera kote! Kazi hii ianze mara moja. Hatutaki watu wajiue hapa. Na madaraja mengine yote yatakayojengwa yawekewe kamera

Kwa kazi alizozifanya Eng. Mfugale, Flyover hii ilistahili kuitwa jina lake. Hakupendelewa, ni haki yake. Wataalamu wengine wamuige!

Gharama za umeme hapa nchini ni kubwa mno. Ni kikwazo katika ushindani wa viwanda. Bila umeme wa uhakika, viwanda ni ndoto!

Naomba flyover ya Gerezani ifanyiwe kazi ambayo tayari hadi tenda yake imeshatangazwa

Nawaomba Japan pia waikumbuke barabara ya Morocco-Mwenge waliyoahidi, imechukua muda mrefu!

Baadhi ya mikwamo hapa nchini imeletwa na wataalam ambao ni watanzania wenzetu! Wataalam wetu walipendekeza vyoo vya mradi wa Stiegler's Gorge vijengwe kilomita 10 toka eneo la mradi...

Miradi hii inaumiza baadhi ya watu. Tusitumike kukwamisha maendeleo ya watanzania. Yapo mengi tunayaweza kwa fedha zetu. Fedha za kujenga Stiegler's Gorge zipo!

Hatuwezi kuingia Uchumi wa Kati wakati tuna umeme unaokatikakatika. Hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Flyovers, miundombinu ya Reli n.k. Maendeleo hayana chama!

Sijasema wapinzani wote waje, ila wale wanaoelemewa na mizigo. Wakija tutawapokea kwa mikono miwili (akimtolea mfano Waitara)

Nawapongeza sana wana Dar es Salaam kwa mshikamano wenu. RC Makonda ameomba nifanye ziara. Nitafanya hivyo, msiwe na wasiwasi nitawatembelea

Rais Magufuli kuzindua Flyover ya TAZARA. Yamaliza Foleni iliyokuwa ikisababisha hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa Mwezi - JamiiForums

Barabara ya Njia sita yaiva: Baada ya bomoabomoa, ujenzi waanza kwa kasi Kimara - JamiiForums
 
yaan nimekereka eti wamefunga barabara ya kutoka ubungo kwenda mbagala kisa uzinduzi Wa daraja
 
Una uhakika kama mimi napata tabu,pumbavu kabisa wewe.
Hujui wanachofanyiwa watumishi wa umma.
Eti mnalazwa njaa, pambaneni na hali zenu bot. Mnataka mtafuniwe na mmezewe.
Kwa iyo mwenyewe umeitenga siku ya leo kucriticize tu huu uzinduzi, walahi kuna watu mtapata tabu sana chini ya kichaa bulldozer.
 
Nipo eneo la tukio na nitawaletea yanayojiri Mungu akijalia. TBC na Clouds TV nawaona hapa hao watarusha tukio zima mubashara. Stay tuned!
 
Leo atarudia ile kauli yake kwamba ana kichaa stage Z. Naomba kwenye hotuba yake aliongelee hilo vizuri kama aliweza kuliongelea la uzazi wa mpango sasa hashindwi kulitolea maelezo ya kutosha
 
Huu mradi ulikuwa wa Jk sijui anazindua nini hajui hata pesa za huu mradi zimetoka wapi . mwambieni huyo kichaa leo hatutaki mipasho
taratibu rafiki yangu si unajua tena nchi hii si salama! Naona sheikh wa Dar yupo, eti naye anasali, huyo Mungu simtaki, nitatafuta wa kwangu asiyehusiana na huyo Sheikh!
 
Back
Top Bottom