Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kabisa kitu kizuri hakidumu ndio maana sometimes tunaamua kuwa wabaya tuMkuu story ile inatia simanzi sana,siku zote dunia hii ukiwa muadilifu kuna hatari ya kuishia kupotezwa na manya'ng'au
It is exhilarating to be recognized for an astounding performance. Civil servants should emulate this patriotic Tanzanian.Wengi tulikuwepo pale TAZARA leo katika ufunguzi wa Flyover, daraja lilopewa jina la Eng Patrick Kipilimba Mfugale.
Pamoja na utani mwingi wa Rais, lakini ametuonyesha upande wa shilingi ambao watendaji wengi wa serikali wanapitia lakini umma hauuoni.
Kati ya sifa alizo mwagiwa Eng Mfugale:
1. Amebuni na kusimamia madaraja mengi nchini
2.Ni mwadilifu na amewahi kusimamishwa kazi kwa kutetea ukweli na akavumilia manyanyaso ya bosi wake. Mwenzake ambaye hakuweza kuvumilia alijipiga risasi.
3. Ni mchapa kazi, alisanifu (draft) daraja la Umoja linalounganisha Tz na Msumbiji ndani ya siku tatu.
(Na bado siku ya ufunguzi daraja hilo wala hakutajwa hadi Waziri wakati huo J Magufuli alipomtaja hadharani kwa marabya kwanza)
4. Akiwa Mkuu wa TANROADS kasimamia ujenzi wa maelfunya kilometa zikiwemo 9,000 kiwango cha lami.
Hapo nilipokuwa nimekaa, wananchi walianza kutikisa vichwa na wengine kujisemea, kuwa kweli Tanzania tuna watu wanafanya kazi kwa moyo.
Kwa upande wa wahandisi namshukuru mh. Magufuli kwa kumuinua Eng Patrick Mfugale na kuitambua fani ya Uhandisi.
Fani ya Uhandisi ikitumika vyema na kwa uadilifu kama alivyo fanya Eng Patrick Mfugale, basi nchi itapata maendeleo chanya.
Na 2015 Mungu alituepusha na yale manyang'au, tungejuta.Mkuu story ile inatia simanzi sana,siku zote dunia hii ukiwa muadilifu kuna hatari ya kuishia kupotezwa na manya'ng'au
Kwani umeambiwa tokea 1977 alikua mkurugenzi TANROAD?How old is this guy! Nafasi ya mtendaji mkuu TANROADS haina umri wa kustaafu?!
Mimi labda sina uelewa hiyo fly over au daraja?
Fly over gani imeshindwa kutengeneza njia ya kuingia buburuni juu na kutoka buburuni kwenda njia ya kurasini kupitia juu pia yaani magari mepesi madogo yawe yanarotate juu na marori makubwa yapite chini.?
Hapana, nilikuwa najaribu kufikiria mtu aliyekuwa mhandisi 1977 after 18 years of schooling and JKT, anaweza akawa na umri gani leo!Kwani umeambiwa tokea 1977 alikua mkurugenzi TANROAD?
Nadhani mambo yote yanakuaga kwe ilani ya chama tawala then aliyechaguliwa anakuwa huru kuchagua kipi kiendelee, kipi kianze kipi cha kuachana nacho. Nafikiri pia ni vyema sana tukiwa na Ilani ya Taifa isiyofungamana na chama chochote cha siasa ili tumchague chama/mtu atakayekuwa na namna nzuri ya kuitekeleza.Nimefuatilia nchi kama Malawi haiendelei coz kila kiongoz anayekuja anakuja na mambo yake kuonekana kaanzisha yeye. Huyu akianza mradi kabla haujaisha na mda wake ukapita anapiga anayeingia ananza mradi wake. So unakuta nchi ipo ipo tu haina mipango ya mda mrefu. Tanzania unakuta kuna mipango ya mda mrefu na kila kiongoz akiingia anaangalia kipi akitekeleze na sio kwa kutaka sifa za nani kafanya. Kuna mradi wa Airport kauacha jk lkn jpm anauendeleza, mloganzila, kinyerezi yote ni miradi imeachwa nusunusu na kwa akili za ufipa ilitakiwa jpm apige chini aanze na ya kwake na kwa akili hizi cjui ka nchi ingeenda. Mradi kafungua jpm na kazindua jpm lkn mtu anakuambia jpm hajajenga yy kajenga jk.
Italipwa hadi na vizazi kumi vijavyo. Masikini Tz, akili zimeenda martenity leave.Tuwekewe sawa jamani hiyo figure ya 400 Billion inafikiwaje?
Tulikotoka
Ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina la Mfugale ulioanza miaka miwili iliyopita umegharimu Sh bilioni 92 hadi kukamilika kwake, huku Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) likichangia Sh bilioni 26. Jina la Mfugale limetokana na jina la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale, ambaye Rais Magufuli alisema amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini na kumpa heshima ya kulitunuku daraja hilo jina lake.
Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 20 1 5 kati ya Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd. Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi huku akiwataka wananchi, viongozi wa siasa kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi huo wenye historia ya kipekee nchini.
View attachment 879144
Rais Magufuli amewasili katika eneo hilo zinapokutana barabara za Mandela na Nyerere na amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
RC Makonda
Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport
"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!
Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu
Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"
Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi
Mkurugenzi Mtendaji TANROADs
Mwaka 2008, Tanzania iliandaa ‘Master Plan’ ya kupunguza msongamano jijini Dar. 2013 Japan wakajitokeza kuwa watatusaidia kujenga daraja hili; 2014 ilitangazwa tenda! Wazabuni walikuja na gharama kubwa
Japan iliongeza ufadhili hadi Bilioni 103 mwaka 2015 Machi, Mkandarasi mmoja alikuja lakini gharama zake zilikuwa mara mbili zaidi. Tulifanya ‘Selective Tendering’ ambapo mkandarasi aliyejenga daraja hili alipatikana
Daraja hili limejengwa kwa nguzo kubwa 26; zimekaa juu ya Piles 133. Daraja lina urefu wa zaidi ya km 1. Linaweza kubeba tani 180 kwa wakati mmoja. Daraja hili linaweza kutumika kwa zaidi ya miaka 100. Limejengwa kwa jumla ya Sh. Bilioni 92
Tunao mkakati wa kujenga BRT ya kutoka mjini(CBD) hadi Gongo la Mboto katika awamu ya 3
Balozi wa Japan
Naamini watanzania wote wamefurahi kuona Flyover ya kwanza nchini Tanzania. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Nafarijika kuwa nikiwa narudi Japan nitatumia ‘Mfugale Flyover’
Eng. Ninatubu Lema(ERB)
Mhandisi Patrick Aaron Lipilima Mfugale ametumikia taaluma ya Uhandisi kwa miaka 41
- Alizaliwa Ifunda, Iringa na alikamaliza Sekondari mwaka 1975. Alipata 1st Degree nchini India, Masters nchini Uingereza
- Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi 1977
Mfugale ametumia muda wake mwingi wa kazi kama Mtaalamu wa Madaraja. Alibuni daraja la Malagarasi; ameshiriki ktk ujenzi wa madaraja ya Mkapa, Umoja, Rusumo, Kikwete, Nyerere, Mto Sibiti, Kilombero na mengine mengi (zaidi ya 1,400 nchini)
Mhandisi Patrick Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS; leo atapata heshima kubwa sana kwa Flyover ya kwanza Tanzania kupewa jina lake!
Elias J. Kwandikwa
Mradi huu jumla umegharimu Bilioni 106. Serikali ya Tanzania imegharimia kodi zote. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Toka Flyover imeanza kutumika, msongamano eneo la TAZARA umepungua kwa kiwango kikubwa
Miradi inayotarajiwa jijini Dar kwa kushirikiana na JICA:
> Upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge
> Ujenzi wa Daraja la Gerezani (Kariakoo)
Rais Magufuli
Natoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao kufuatia ajali ya #MVNyerere na kuwaombea majeruhi uponyaji wa haraka. Nawashukuru watanzania kwa mshikamano walioonyesha
Ajali hii ya #MVNyerere iwe funzo kwetu. Ajali kama hizi zinaepukika, na zikitokea basi madhara yake yanaweza kuwa madogo kama tukipata funzo kwa kilichotokea
Nawapongeza Wizara ya Ujenzi, TANROADS na Wahandisi washauri kwa kusimamia ujenzi wa #MfugaleFlyover. Daraja limegharimu Bilioni 106.65; Japan wamechangia kiwango kikubwa cha pesa hii, ni marafiki wa kweli kwenye masuala ya maendeleo
Nampongeza Mbarawa ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi wakati ujenzi wa #MfugaleFlyover unaanza
Nakumbuka wakati Daraja la Umoja linaandaliwa kujengwa, nilimwita Mfugale anisaidie design ya Daraja hilo; nilipoipeleka kwa marais wa Tanzania na Msumbiji, ikapitishwa. Wakati wa uzinduzi wala hakutambulishwa
Mwaka 2008 Mfugale na mwenzake walipewa maagizo wakayakataa, Katibu Mkuu wa wakati huo aliwaokoa; mwenzake (marehemu Mjungi) alijiua kwa kujipiga risasi lakini Mfugale alivumilia. Ndo gharama ya kusimamia maadili
Ujenzi wa Flyover ya Ubungo itagharimu Bilioni 247. Itakuwa flyover ya aina yake kwa hapa Dar es Salaam! Wazaramo watasema ‘Ina ghorofa 3’
Tunajenga barabara ya njia 6 kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa Sh. Bilioni 140 na fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania. Kutakuwa pia na njia ndogo 2 (service road). Bomoabomoa ya Kimara ilizingatia sheria!
Katika #MfugaleFlyover, nataka zifungwe kamera kote! Kazi hii ianze mara moja. Hatutaki watu wajiue hapa. Na madaraja mengine yote yatakayojengwa yawekewe kamera
Kwa kazi alizozifanya Eng. Mfugale, Flyover hii ilistahili kuitwa jina lake. Hakupendelewa, ni haki yake. Wataalamu wengine wamuige!
Gharama za umeme hapa nchini ni kubwa mno. Ni kikwazo katika ushindani wa viwanda. Bila umeme wa uhakika, viwanda ni ndoto!
Naomba flyover ya Gerezani ifanyiwe kazi ambayo tayari hadi tenda yake imeshatangazwa
Nawaomba Japan pia waikumbuke barabara ya Morocco-Mwenge waliyoahidi, imechukua muda mrefu!
Baadhi ya mikwamo hapa nchini imeletwa na wataalam ambao ni watanzania wenzetu! Wataalam wetu walipendekeza vyoo vya mradi wa Stiegler's Gorge vijengwe kilomita 10 toka eneo la mradi...
Miradi hii inaumiza baadhi ya watu. Tusitumike kukwamisha maendeleo ya watanzania. Yapo mengi tunayaweza kwa fedha zetu. Fedha za kujenga Stiegler's Gorge zipo!
Hatuwezi kuingia Uchumi wa Kati wakati tuna umeme unaokatikakatika. Hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Flyovers, miundombinu ya Reli n.k. Maendeleo hayana chama!
Sijasema wapinzani wote waje, ila wale wanaoelemewa na mizigo. Wakija tutawapokea kwa mikono miwili (akimtolea mfano Waitara)
Nawapongeza sana wana Dar es Salaam kwa mshikamano wenu. RC Makonda ameomba nifanye ziara. Nitafanya hivyo, msiwe na wasiwasi nitawatembelea
Rais Magufuli kuzindua Flyover ya TAZARA. Yamaliza Foleni iliyokuwa ikisababisha hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa Mwezi - JamiiForums
Barabara ya Njia sita yaiva: Baada ya bomoabomoa, ujenzi waanza kwa kasi Kimara - JamiiForums
😀😀😀Nyerere alimwambia kwenye kikao cha Nec nitapendekeza jina lako ili uwe Rais wa Tanzania lakini wewe utasimama na uikatae nafasi hiyo, basi ndani ya kikao Nyerere alipompendekeza Mwinyi kuwa mgombea Urais Mwinyi alisimama na kuanza kuwashukuru wajumbe kwa imani yao kubwa kwake na yuko tayari kwa nafasi hiyo.
Unaweza ambulia chochote hapa 👉Mkurugenzi wa Barabara Ajiua - JamiiForumsMwenye taarifa ya kina ya jambo hili hebu atupie humu, tuwajue waliosababisha kujiua kwa Leopord Mjungi, pia tumjue na katibu mkuu aliyewaokoa, ili historia iweze kukaa sawa sawa.