Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

Uchaguzi 2020 Dar: Helkopta ya Kampeni ya Tundu Lissu, yanyimwa kibali cha kutumia anga, ni baada ya kuomba kibali hapo jana

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Ratiba ya mikutano 5 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo mkoani Pwani, imevurugika baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kunyimwa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kuruka.

Taarifa za kukataliwa kwa helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara wa Mhe. Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa Mhe. Lissu umeshatoka nje ya jengo la abiria, ametoa sababu zisizoeleweka kuzuia helkopta hiyo kuruka kutoka Uwanja wa JNIA kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema imelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Mhe. Lissu na msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana. Mbali ya Mhe. Lissu, abiria wengine waliokuwa watumie usafiri huo ni watu 3, akiwemo Ofisa Mnadhimu wa Msafara Amani Golugwa, Katibu wa Mgombea, David Jumbe, msaidizi wa masuala ya ulinzi pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Mbona huelezi kikamilifu kwa nini mmenyimwa kibali ili sisi 'third party' tuweze kupima na kuona uhalali au uonevu uliotendeka? Hivi sasa tunasikia upande mmoja tu wako jinsi Chadema 'ilivyoonewa'. Barua ya kukatazwa kutumia anga lazima ilisema ni kwa sababu hii na ile. Tujuze au vizuri zaidi ibandike hapa JF barua hiyo ili na sisi tuweze kupima uhalali au la wa sababu hizo.
 
Kila siku unaanzisha mada za Cdm . Kumbe kichwani ni mtupu hivi ?!. Hellcopter zinapakiwa majumbani ?
We boya kweli, kwa hiyo lowassa na mbowe hapo wapo airport?
IMG_20200910_171053.jpg
 
Kuna wakati unashindwa kuelewa hawa watu wana roho mbaya ama Wana wivu.

Inakuwaje Lissu aogopwe namna hii ilhali walio madarakani wana kila kitu kinachowahakikishia ushindi?

Tume, mahakama, polisi na jeshi vyote vipo upande wao.

Kuwaachia wananchi wapate furaha ya moyo mara moja katika miaka mitano iliyopita napo imekuwa nongwa.

Watawala nia yao ni kuishi peke yao bila shaka.

Inachosha!
Wangemwacha aruke bila kibali, wajeda wa ngerengere wamshushe, na asidhani yeye ni mtu special Sana anaweza shushwa na Mambo yakawa poa tu
 
Huyo afisa alitumwa kutoa taarifa,Kuna kambale wako ofisini ambao ni Johari na Filikunjombe,tangia Johari asifiwe na Magufuri kuwahujumu fastjet Basi no mwendelezo uleule wa hujuma.
Tunakushukuru kwa kuwafichua , kama unazo picha zao zimwage hadharani dunia iwajue
 
Sijaelewa, ina maana;.

1. Ndege (Helicopter) ilishakaguliwa, ikapata cheti cha usalama (Safety certificate), right?

2. Mgombea Tundu Lissu na msafara wake wakawa tayari wako hapo Airport na ghafla tu wakaambiwa hakuna kibali cha kuruka?

3. Sababu za kutopata Kibali ni nini sasa iwapo walishapata Safety Certification?

4. Ndiyo kwa heri moja kwa moja hawatapata au wamecheleweshwa tu kupata kibali hicho kwa leo?

Hebu tupeni taarifa kamilifu pls...
 
Wakataze helicopter wakubali

Tarehe 28 kura yangu na familia yangu ni kwa Lissu
NCHI YA MAAJABU SANA HII , HIVI WANAO YAFANYA HAYA WAMETAFAKALI KESHO YAO , AU NI ILE BENDELA FUATA UPEPO, TUNADHALILISHA TAIFA HILI SANA , KWA MABO YA MAAJABU SANA , HAYA NGOJA TUONE MWISHO WAO , MPAKA HAPO WANAZIDI KUWAPIGIA KAMPENI CHADEMA BILA KUTOJUA ,
 
Mkuu maana ya kuleta habari kwa fumo hii ni kwamba ili sisi hapa jukwaani tujadili tukiegemea upande mmoja tu kuwapa haki chadema huku tukiwa hatujui ya upande wapili ambapo inawezekana hawakufuata taratibu husika.

Fikiria kibali kimeombwa jana kwa mujibu wa hiyo taarifa hapo na huwezi jua hiyo jana ni saa ngapi ( kwa siku moja wanataka mamlaka ya anga itoe kibali Cha kurusha ndege)

Wakati huo kumbuka kesho toa tamko kuwa Kuna njama ovu dhidi yake kwenye hiyo ndege ili apate ajali ,hapo unadhani mamlaka itaruhusu kirahisi? ( Mdomo wake ndio unamponza)

Alafu mtu hujapewa kibali bado lakini tayari usha andaa safari unataka kurusha ndege.
Aende kwenye kampeni asitafute sababu zisizokuepo
 
CDM wasiwafanye wananchi wapuuzi. Uungwana watuambie hizo sbb walizoambiwa na TCAA nasie tupime. Lkn si kutupa kauli za jumla jumla za kitoto. Kama issue ni kuwazuia mbona juzi wameenda na kurudi Unguja kwa chata? Kwa nn hawakuzuiwa pia?. Sbb zisizoeleweka maana yake ni nn kiasi ikawa rahisi kwao kuchukua aina ingine ya usafiri?

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;
chadema msiwafanye watu wajinga
jukumu la kuomba kibali cha kuruka ni la mwenye helicopter sio chadema
Mamlaka inafanya kazi na mwenye chopper ambaye ndie anapewa vibali na usajli,kwa mantiki hiyo,mamlaka ilipaswa kuizuia kampuni ya ndege tena kwa maandishi
Tuonesheni hiyo barua ya mamlaka kuzuia msiruke.
Chadema hamna pesa ya kampeni,msilete visingizio
 
Aende kwenye kampeni asitafute sababu zisizokuepo
Makene tangu mkewe anyanyaswe kijinsia huko hayuko vyema kichwani. Ukichanganya na hawa kina Munisi wanaomhujumu afukuzwe kazi ndio kabisa anachanganyikiwa.
 
Nadhani mngeweka wazi hizo sababu mlizopewa ili na sie tuone kama kweli hazieleweki
 
Lissu angepanda British Airways Business Class hadi huko Kibaha na Bagamoyo kuwakomesha maccm
 
Waliomba kwa barua , wanazuiwa kwa barua
Au waliomba kwa mdomo na kuzuiwa kwa mdomo. Ki ofisi haipo
Ni swali zuri, hata baada ya kuzuiliwa hamkuna sababu zisizo na msingi ziwekwe hapa sababu walizo pewa. Japo najua moja lazima hawaja identify mahali pa kutua. Maana nakumbuka kuna wakati zilitolewa regulations za helkopta kutua Tanzania. Kwa ajili ya usalama.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Ratiba ya mikutano 5 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Lissu, iliyopangwa kufanyika leo mkoani Pwani, imevurugika baada ya helkopta aliyokuwa aitumie kufika katika maeneo hayo, kuzuiliwa kwa kunyimwa kibali na Mamlaka ya Anga nchini, muda mfupi kabla ya kuruka.

Taarifa za kukataliwa kwa helkopta hiyo kuruka zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa, wakati msafara wa Mhe. Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) terminal I.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga aliyewasilisha taarifa hiyo wakati msafara wa Mhe. Lissu umeshatoka nje ya jengo la abiria, ametoa sababu zisizoeleweka kuzuia helkopta hiyo kuruka kutoka Uwanja wa JNIA kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, wakati kibali chake kiliombwa tangu jana.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema imelazimika kutafuta njia mbadala ili Mgombea Urais Mhe. Lissu na msafara wake, aweze kuendelea na ratiba ya mikutano kwa kadri inavyowezekana. Mbali ya Mhe. Lissu, abiria wengine waliokuwa watumie usafiri huo ni watu 3, akiwemo Ofisa Mnadhimu wa Msafara Amani Golugwa, Katibu wa Mgombea, David Jumbe, msaidizi wa masuala ya ulinzi pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Imetolewa leo, Alhamis, Septemba 10, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Very pathetic. This is possible only in Tanzania!!!!
 
Back
Top Bottom