Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Kwa kweli inatisha sana
 
Aiseeee!

Nchi hii mbona inaelekea pabaya hivi!
 
Watekaji wote wamefahamika majina yao yote na hata wanakoishi, tusubiri porojo za Muliro
 
Nimpe pole jamaa kunasuka hapo, maana wange mu RIP, pili inasikitisha sana wabongo hawasaidii wanamuangalia mtu akiwa matatizoni, baadae watume RIP

Aisee jamii inahitaji revolution , hii ni zaidi ya ukondoo
Kama swala wa mwituni mwenzao anaponyakuliwa na simba hana msaada.
 
Ila pamoja na yote watu wa Dar mmezidi uoga aise mnazidiwa na hata watoto wadogo wa shule ya msingi angalau wanejipitisha hapo.

Nchi yetu bado tuna bonge la safari ambalo halijajulikana litaisha lini. Hao wapumbavu walikuwa wa kugongeshwa mawe mpaka wapoteane.
 
Watu wanaoshindia mihogo na miguu ya kuku unategemea nini?
 
Nimeona wengi sana wakilaumu kuhusu watu kutojitokeza kutoa msaada, Kwa upande flani ni sahihi lakini je nani anaweza kuhatarisha MAISHA yake Kwa kupambana na watu ambao ameshafahamishwa kuwa wanatembea na siraha za moto (bunduki), wote tuna kumbuaka kuhusu lile tukio lililotokea kule club ya masaki watu walitamani kuzuia ila walishindwa sababu ya hivyo (bunduki) na hata miaka kadhaa iliyopita katika tukio na nape nauye (kama sikosei) ni maulidi kitenge pekee ndo alijitoa muhanga na ikawa ajabu kiasi watu walianza kushuku pengine ni agent wa TISS, ipo mifano mingi tu, sio kwamba watu wanashindwa ama hawataki kutoa msaada ila ni kwamba Kuna wakati watu wanabaki wanaumia tu na kukosa Cha kufanya na wengine kuthubutu hata kurecord na kuacha JAMII ishuhudie huu uovu
NB. HATA SIJUI NI LINI NA NI NINI HATIMA YA HAYA YANAYOTOKEA DAH!.
 
Mshana Jr JANA KASEMA KUNA MATUKIO YANATENGENEZWA ILI KUZUBAISHA WATU KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI NAANZA KUMUAMINI KATIKA HILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…