Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Mungu Kampa Mwili Wake Mkubwa Kama Kinga Ya Kuuliwa Na Wapumbavu kama hawa na Bado Watanzania Tunawacheki tu.

Nchi gani hii

Na Ajabu Utasikia Kimya

Hawajulikani

Na Kunakauli ya mwisho hapo Tutakupata/ Tutakufuata hawa Tunaomba Majina yao Yasambae tujue hawa ndio Wauwaji
Kwa kweli inatisha sana
 
Wakuu,​

Nimekutana na video hii duniani huko, pamoja na kujaribu kupiga kelele watu waliuchuna. Angalu video hii imepatikana, kama ni tukio la kweli wasiyojulikana wataanza kujulikana.

=====

Kumbusho Dawson kaandika haya kupitia ukurasa wake akisindikiza video hiyo;

"Tukio hili la utekaji limetokea jana Rovvenpec Resort, Kiluvya madukani, kutokana na nguvu za mwamba aliwashinda watekaji.
"Inasikitisha Sana kwamba hakuna pamoja Na kwamba kulikuwa na watu wanashuhudia hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada inasikitisha.

Pia soma: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

"Mstari unaotofautisha akili za nyumbu na Watanzania ni ndogo kama punje ya haradali. Mtu anakamatwa watu wanashangàa kama kundi la nyumbu porini. Shame be upon you."

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Aiseeee!

Nchi hii mbona inaelekea pabaya hivi!
 
"Nisaidieni naenda kuuawa, naenda kuuawa, siwajui hawa, naenda kuuawa" jamaa anapambania uhai wake nje ya Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya madukani, jijini Dar. Lakini wananchi wanashuhudia tu, na hawatoi msaada wowote. Yani ilitakiwa hicho kigari kigeuke "majivu" dakika sifuri lakini watu wanashangaa tu kama vile wanaangalia sinema.

Angalau huyu aliyechukua video amesaidia kuhabarisha umma, lakini wengine wamesimama tu wakiangalia mwenzao akilalamika kwenda kuuawa. Halafu kesho maiti yake ikiokotwa huko Ununio watu haohao wangejifanya kusikitika. Watanzania wengi ni wanafiki sana aisee. Ptuu mbaka.!

Ukifuatwa na hawa wahuni jitetee kwa nguvu zako zote, its a margin between death and life. Usitegemee watanzania maana wengi ni makondoo tu. Pigania uhai wako mwenyewe. Kama una silaha yoyote itumie kujihami. Usitembee kiboya.

Huyu jamaa ubonge umemsaidia. Mungu kamjalia mwili na nguvu za kujitetea. Lakini angekua "kimbaumbau" kama mimi, saivi tungeshaandika BringBack za kutosha, au mwili wake ungeokotwa huko Ununio.

Nimejisikia vibaya sana kuona vitendo vya utekaji vinafanyika katika nchi huru na viongozi wala hawajali. Fikiria "watekaji" wanaongea kwa kujiamini kwamba "ukigoma kuingia hapo tutakuua" na bado wananchi wanashangaa tu. Pamoja na jamaa kujitetea na kufanikiwa kuokoa roho yake, bado watekaji wamejibu kwa dharau kwamba "Tutakurudia" maana yake hajakwepa kifo. Amekiahirisha tu 😭. Halafu wale tuliowapa dhamana za uongozi wanatuambia kifo ni kifo tu. Mene mene tekeli na peresi. Mungu yupo.!

Chanzo Melissa Gj .
View attachment 3150726
Facebook
Watekaji wote wamefahamika majina yao yote na hata wanakoishi, tusubiri porojo za Muliro
 
Ila pamoja na yote watu wa Dar mmezidi uoga aise mnazidiwa na hata watoto wadogo wa shule ya msingi angalau wanejipitisha hapo.

Nchi yetu bado tuna bonge la safari ambalo halijajulikana litaisha lini. Hao wapumbavu walikuwa wa kugongeshwa mawe mpaka wapoteane.
 
Watu wanaoshindia mihogo na miguu ya kuku unategemea nini?
 
Nimeona wengi sana wakilaumu kuhusu watu kutojitokeza kutoa msaada, Kwa upande flani ni sahihi lakini je nani anaweza kuhatarisha MAISHA yake Kwa kupambana na watu ambao ameshafahamishwa kuwa wanatembea na siraha za moto (bunduki), wote tuna kumbuaka kuhusu lile tukio lililotokea kule club ya masaki watu walitamani kuzuia ila walishindwa sababu ya hivyo (bunduki) na hata miaka kadhaa iliyopita katika tukio na nape nauye (kama sikosei) ni maulidi kitenge pekee ndo alijitoa muhanga na ikawa ajabu kiasi watu walianza kushuku pengine ni agent wa TISS, ipo mifano mingi tu, sio kwamba watu wanashindwa ama hawataki kutoa msaada ila ni kwamba Kuna wakati watu wanabaki wanaumia tu na kukosa Cha kufanya na wengine kuthubutu hata kurecord na kuacha JAMII ishuhudie huu uovu
NB. HATA SIJUI NI LINI NA NI NINI HATIMA YA HAYA YANAYOTOKEA DAH!.
 
Wakuu,​

Nimekutana na video hii duniani huko, pamoja na kujaribu kupiga kelele watu waliuchuna. Angalu video hii imepatikana, kama ni tukio la kweli wasiyojulikana wataanza kujulikana.

=====

Kumbusho Dawson kaandika haya kupitia ukurasa wake akisindikiza video hiyo;

"Tukio hili la utekaji limetokea jana Rovvenpec Resort, Kiluvya madukani, kutokana na nguvu za mwamba aliwashinda watekaji.
"Inasikitisha Sana kwamba hakuna pamoja Na kwamba kulikuwa na watu wanashuhudia hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada inasikitisha.

Pia soma: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

"Mstari unaotofautisha akili za nyumbu na Watanzania ni ndogo kama punje ya haradali. Mtu anakamatwa watu wanashangàa kama kundi la nyumbu porini. Shame be upon you."

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Mshana Jr JANA KASEMA KUNA MATUKIO YANATENGENEZWA ILI KUZUBAISHA WATU KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI NAANZA KUMUAMINI KATIKA HILI
 
Back
Top Bottom