Dar kama hujaja siku nyingi siku ya kuja lazima udakwe na kichefuchefu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Dar kama hujaja siku nyingi, siku ya kuja lazima udakwe na kichefuchefu. Kichefuchefu ni kitendo cha mwili kujilinda dhidi ya sumu.

Mtu akila sumu au kitu cha kudhuru mwili una sense na kuleta kichefuchefu ili ukitapike. Sasa hata hewa nzito na mbaya inaenda kushtua eneo lile lile linaloshtuliwaga na sumu. Na mwili unajua njia nzuri ni kuleta kichefuchefu na kuitapika hiyo sumu.

Lakini ukiwa mwenyeji mwili unazoea na kujua kuwa kitu kile siyo sumu. Ndiyo maana wenyeji wanadunda tu. Mji wa Dar ni mchafu sana, si kwa mazingira na si kwa moshi wa kutoka kwenye magari kuukuu. Ile habari ya Michael Jackson kuziba pua alipofika Dar es Salaam inawezekana ni kweli kabisa.
 
Naunga mkono hoja!
 
Upo sawa mkuu. Yani kama unaenda Dar kupitia Chalinze ukianza kufika Mlandizi unahisi kabisa hali ya hewa inabadilika, mapigo ya moyo yanaenda mbio, pumzi inakata, unatokwa jasho.

Mpaka uje ufike Mbezi, Kimara, Ubungo unakuwa ushajuta.

Hilo jiji lilinishinda. Nikifika huko ni kuzunguka siku kadhaa tu na kuondoka japo nilisoma na kuishi huko
 
Hamuishi Kuja Dar mamia Kwa makumi wanatoka mikoani na kuingia Dar Kila siku huku wakijiapiza kutorudi Tena huko kwenye hewa safi.Siku mkiacha unafiki hii nchi itapona.
 
Ndugu zangu kila wakiniuliza unakuja lini dar? Nawajibu nakuja kufanyeje kwenye jiji chafu kama hilo? Lenye joto kali na harufu mbaya na nzito? Kati ya bolt 11 nilizopanda kwenye mizunguko yangu 7 hawawashi AC sijui kwann. Anyways kila nikipata safari ya dar inakuja sonona ila kwa mbali nacheka sababu tinder ipo vere ektive jijini 😁
 
Tokea nihamie dar sijawahi kufikiri kuondoka sasa niende wapi kwa hapa Tanzania??

Ukiachana na kwenda nyumbani Arusha kusalimia dar ndio my second home.
 
Dar es Salaam is among of the most dirtiest and unplanned towns in the world.

'Dsm ni Jiji au Zizi ??????'
 
Hamuishi Kuja Dar mamia Kwa makumi wanatoka mikoani na kuingia Dar Kila siku huku wakijiapiza kutorudi Tena huko kwenye hewa safi.Siku mkiacha unafiki hii nchi itapona.
Tunakuja kwa shida tu sio kwa kutaka. Dar sio sehemu ya kuishi mtu ambae anapenda kufurahia maisha
 
Hahahah
 
Mm Hilo jiji nalielewa sna umenipa ujanja mwingi sna natumiaa akili za dar kuishi dodoma pakame

Kila mwezi al
lzm nilazimiashe safri za kwenda dar mobibo Kisha keko machungwa Kisha kigamboni gezaulele. Alfu anarudi vikindu namkamua mzaramo wangu vzr
 
Hamuishi Kuja Dar mamia Kwa makumi wanatoka mikoani na kuingia Dar Kila siku huku wakijiapiza kutorudi Tena huko kwenye hewa safi.Siku mkiacha unafiki hii nchi itapona.
Ndiyo jiji lenye hela, vyuo vikuu, biashara na serikali. Halikwepeki.
 
mji mchafu sana wenyeji wanakula chakula na nzi. Kuna harufu fulani kama ya nya inatembea na upepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…