Dar: Kiwanda cha Magodoro GSM, Chawaka Moto

Dar: Kiwanda cha Magodoro GSM, Chawaka Moto

picha haina uhusino na kilichotokea ...

C3F291E1-5A8D-4496-8594-EB61FC51846B.jpeg
 
Waache uhuni wanavichoma viwanda wavute pesa bima, huwezi jenga kiwanda ukashindwa kujenga mfumo wa udhibiti moto auzidi hata milioni 20.
 
Kuna moshi mzito anga la Mwenge, Mawasiliano na Ubungo. Inasemekana Kiwanda cha Magodoro GSM kinateketea.

---
Kiwanda cha kutengeneza magodoro kinachomilikiwa na Kampuni ya GSM kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kimeungua moto

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kwa sasa.

View attachment 2148653

Soma > Baada ya kiwanda kuwaka moto GSM wasema “Tumepata hasara kubwa sana, hakuna kilichosalia"
Katika hili naamini.kbsa makonda hahusiki ila hao gsm kumbe ndio wale homeshoping center ni watu wabaya sana hao na wamerudi kwa kasi si ajabu utasikia kiwanda kilokuwa na mkopo.wanataka sababu ya kulipwa tena kutokana na janga hilo naamni hii issue imetengenezwa na hawa jamaa na wale vigogo wa bwagamoyo ni marafiki wakubwa kbsa...
 
Unachoma moto mwenyewe alafu unatengeneza mazingira fulani aonekane ndiyo kafanya hayo...

Au...

Fulani kweli katuma wasiojulikana kufanya hayo, kuoneshana misuli...
Hii dhana ya pili sio rahisi, hana mbavu hizo sasa hivi
 
Wadau, kwa vile moyo umeumbwa na vijiswali ambavyo wakati mwingine havina majibu, lakini najiuliza tu,kiwanda cha GSM kuungua kunani?
 
Hivi mnapozungumzia Mtu kuchoma kiwanda ili alipwe na bima huwa mmefanya analysis ya mnachokituhumu?
Kuchoma mali kama kiwanda ili upate faida ya ziada katika bima si jambo rahisirahisi kama ambayo Watu huwa wanasema mara kwa mara.

Msingi wa bima ni kukurudisha ulipokuwa kabla ya mali yako kuungua. Na inapobidi, kama kampuni ya bima itahisi kuna 'mchezo' itafanya investigation hata kwa kuwatumia investigator kutoka Nje wenye ujuzi.

Unapokata bima unalipia asilimia flani kutokana na thamani halisi ya mali uliyonayo. Mathalani kama unataka bima ya nyumba yako, valuation itafanyika na kusema kwa mfano nyumba yako ina thamani ya milioni mia moja, halafu utalipia asilimia mbili ya thamani kama ada ya mwaka ya bima. Nyumba ikiungua utalipwa kwa kuzingatia thamani ya ujenzi wakati tathmini ya uharibifu inafanyika.

Kwa hiyo ama utapata milioni mia moja au zaidi au chini ya hapo kutegemea na gharama za ujenzi wakati husika. Kwa hiyo huwezi ku-risk kuchoma nyumba kwa sababu ya nyongeza au pungufu ya milioni mia moja. Zingatia pia, inawezekana ikagundulika umochoma, hapo sasa utajua haujui.

Kwa habari ya kiwanda ni almost risk yake ni kama nilivyoeleza hapo juu lakini nyongeza ya hilo, kuna risk ya kupoteza imani kwa Mfanyabiashara mkubwa kama yule itakapogundulika amechoma kiwanda kwa makusudi. Hili Wafanyabiashara wengi wakubwa huwa wanaliogopa sana.

Nasema hivi si kuwa hakuna foul zinazochezwa na Wafanyabiashara wakubwa lakini pia si rahisi kufanya jambo kama lile kwa kuzingatia risk zinazoambatana nazo.

Nimeona mara nyingi hata gari ya Mtu ikiungua mtu anasema kirahisi amechoma ili alipwe, bandugu, kama gari yako ina thamani ya milioni ishirini bima haitakulipa zaidi ya hiyo thamani tena zaidi lazima utakatwa kitu kinaitwa 'excess'. Kuna Mtu alichoma Range rover used akifikiri atalipwa mpya, akaambiwa kwenye preliminary assessment kuwa atalipwa thamani halisi ya gari yake kabla ya kuungua, na mbaya zaidi ikaja gundulika aliichoma. Si tu hakulipwa, hata Benki alikokuwa anakopa mara kwa mara kwa kutumia dhamana ya magari wakawa kwenye high alert wakiamini si Mtu sahihi kufanya naye biashara (benki na bima zinaitwa financial institution, kwa hiyo kwa kiasi flani zinashirikiana kupeana taarifa).
 
Back
Top Bottom