Hivi mnapozungumzia Mtu kuchoma kiwanda ili alipwe na bima huwa mmefanya analysis ya mnachokituhumu?
Kuchoma mali kama kiwanda ili upate faida ya ziada katika bima si jambo rahisirahisi kama ambayo Watu huwa wanasema mara kwa mara.
Msingi wa bima ni kukurudisha ulipokuwa kabla ya mali yako kuungua. Na inapobidi, kama kampuni ya bima itahisi kuna 'mchezo' itafanya investigation hata kwa kuwatumia investigator kutoka Nje wenye ujuzi.
Unapokata bima unalipia asilimia flani kutokana na thamani halisi ya mali uliyonayo. Mathalani kama unataka bima ya nyumba yako, valuation itafanyika na kusema kwa mfano nyumba yako ina thamani ya milioni mia moja, halafu utalipia asilimia mbili ya thamani kama ada ya mwaka ya bima. Nyumba ikiungua utalipwa kwa kuzingatia thamani ya ujenzi wakati tathmini ya uharibifu inafanyika.
Kwa hiyo ama utapata milioni mia moja au zaidi au chini ya hapo kutegemea na gharama za ujenzi wakati husika. Kwa hiyo huwezi ku-risk kuchoma nyumba kwa sababu ya nyongeza au pungufu ya milioni mia moja. Zingatia pia, inawezekana ikagundulika umochoma, hapo sasa utajua haujui.
Kwa habari ya kiwanda ni almost risk yake ni kama nilivyoeleza hapo juu lakini nyongeza ya hilo, kuna risk ya kupoteza imani kwa Mfanyabiashara mkubwa kama yule itakapogundulika amechoma kiwanda kwa makusudi. Hili Wafanyabiashara wengi wakubwa huwa wanaliogopa sana.
Nasema hivi si kuwa hakuna foul zinazochezwa na Wafanyabiashara wakubwa lakini pia si rahisi kufanya jambo kama lile kwa kuzingatia risk zinazoambatana nazo.
Nimeona mara nyingi hata gari ya Mtu ikiungua mtu anasema kirahisi amechoma ili alipwe, bandugu, kama gari yako ina thamani ya milioni ishirini bima haitakulipa zaidi ya hiyo thamani tena zaidi lazima utakatwa kitu kinaitwa 'excess'. Kuna Mtu alichoma Range rover used akifikiri atalipwa mpya, akaambiwa kwenye preliminary assessment kuwa atalipwa thamani halisi ya gari yake kabla ya kuungua, na mbaya zaidi ikaja gundulika aliichoma. Si tu hakulipwa, hata Benki alikokuwa anakopa mara kwa mara kwa kutumia dhamana ya magari wakawa kwenye high alert wakiamini si Mtu sahihi kufanya naye biashara (benki na bima zinaitwa financial institution, kwa hiyo kwa kiasi flani zinashirikiana kupeana taarifa).