Dar Kuna fursa nyingi za biashara na kupiga pesa, ni kuamua na kutokuwa na aibu tu

Dar Kuna fursa nyingi za biashara na kupiga pesa, ni kuamua na kutokuwa na aibu tu

Mtoa mada Asante , ubarikiwe na Bwana.

Sasa nashangaa hao majamaa hapo juu wamekukalia kooni , wakati wewe umejaribu kuwaonyesha fursa , wako busy wanakosoa wakati hizo Biashara tajwa wapo watu wanazifanya hapa Dar na maisha yanakwenda vizuri , Sasa wao wanabisha nini ?

Mtu hana mbele hana nyuma na yeye eti anachagua cha kufanya 😄 Mara hiki vile mara hiki hivi ili mradi tu atoe kasoro , Sasa kwa mentality hiyo ngumu kutoboa

Kuna mishe tunaita Kama ni stepping stone , ufanye ulipe Kodi, ule , huku ukisave mtaji kidogokidogo kufanya mishe nyingine au kuiboresha hiyo uliyo nayo

Sasa wajuba wako so negative duh
 
Mkuu kuna vitu ni vigumu kuwaaminisha watu, ushaplay part yako....

Mi nlikuaga nawaangalia watu wanaofanya biashara ya sh 100 naona huyu hata afu kumi anafikisha kweli?? Mwaka huu nmeifanya mauzo ilikua afu 50 hadi laki kwa siku. Mauzo nkitoa hesabu zangu faida ya maana sana tu.

Nkuambie tu faida nliokua napata hata salary yangu haifiki 😀
Acha kazi ufanye biashara mkuu.😃
 
Me Huwa napenda kutafiti njia za utafutaji hata ziwe ndogo vipi, ili kujua watu wanapataje pesa na hizo biashara ambazo watu wanaziona ni duni
Nikasema haaa kumbe aisee watu wanapiga pesa ambazo hata watu wenye ajira za kuchomekea mashati na kuvaa viatu mchuchumio hawapati

Nitaorodhesha baadhi ya biashara hapa za kupiga pesa chap na bila kelele.

1. Biashara ya kununua chuma chakavu.
Kuna jamaa angu yupo hapo bunju anapiga pesa ndefu, alinielezea Kwa uwazi nikashangaa utajiri wa hii biashara ambao wengi hawajaistukia
Yeye ana kijiwe na mzani wake, vijana hasa wale mateja wanaokota vyuma ananunua sh 700 ana uweZo wa kukusanya kilo 200 Kwa siku,
Yeye anawauzia madalali wa wahindi sh 1000
Kwaiyo kila kilo anapata sh 300.
Hapo ni 300*200=60000
Ana uhakika wa kuingiza sh 60, 000 Kwa siku bila kelele

2. Biashara ya kifurushi.
Hivi ni viongeza nyege, yaani ni package ya karanga mbichi, mihogo mibichi, nazi, karoti n.k hufungwa kifurushi kidogo
Kuna mdada anauza pale Mbagala na Mimi bi mteja wake akinikuta Dar Niko bar Huwa nanunua alinisimulia anavopiga pesa nikashangaa

Yeye anafunga kuanzia vifurushi 100 hadi 200
Anatembeza mitaani hasa nyakati za jioni hadi usiku na mzigo wake anaukata
Huyu Binti amejenga mjengo wake maeneo ya Vikindu

3. Biashara ya supu ya pweza
Hii biashara ina pesa ndefu sana na mtaji wake ni Sh 70000 tu ila jamaa wanakunja pesa ndefu
Anzisha biashara hii ajiri vijana utapiga pesa nzuri

4. Kuku wa kienyeji
Hapa watu wa Dar hasa kutoka maeneo yenye pesa kama upanga, mikocheni,mbezi nk
Fuata kuku Morogoro njoo upige pesa Dar

5. Maji ya kandolo
Mjinwa Dar umejaa masikini wengi
Sio kila mtu kwenye mihangaiko ataweza kununua maji ya buku
Wengi hukimbilia maji ya 100
Hapa mtaji ni maji yasiokuwa na chumvi, deli na barafu nenda kariakoo, Makumbusho, Temeke, Mbagala piga pesa

6. Kuuza barafu shuleni au mihogo
Watoto wa mjini laZima kila siku wapewe pesa ya kula shule sio kama kwetu Ngara mtoto humpi hela ya shule
Kwa mihogo ya kuchemsha au barafu utapiga pesa hadi ukimbie

7. Umachinga
Umachinga inalipa
Usidharau machinga
Dar Kuna Chimbo vitu bei kubwa na watu wa Dar Kwa uvivu wao hayo machimbo hawajui
Mfano Kuna chupi nzuri za akina dada kariakoo hapo zinauzwa 700 pic 1 mtaani unaweza uza buku 5
Yaani hapa Kwa siku ukiza pisi 7 tu unafaida ya sh 30,000

8 Fanya delivery ya chakula.
Watu wengi wa Dar hawapendi kuhangaika
Wewe unaweza pika msosi ukawatafuta vijana mabachelor na watu wa madukani ukawa unawapelekea chakula na laZima uuze sio story utapiga pesa

9 kuuza screen protector na cover za simu
Huku ndo Kuna pesa
Aslimia 80ya wakazi wa Dar wana Smart phone
Na simu zinahitaji hivyo vitu
Hapa kariakoo hayo phone protector na covers ni Sh 600
Ukitembeza mtaani kumwekea mtu ni buku 5
Ukiwawekea watu 6 Kwa siku
Pesa yako Kwa mwezi hata mhasibu pale nmb hakufikii Kwa maokoto

10. udalali
Japo hapo unaweza kuliwa na njaa ni kazi ambayo wateja sio wa kila siku
Tafuta vyumba, nyumba, viwanja, frem nk
Wateja ni wengi utapiga pesa upo umetulia
😅😅😅😅hizi stori bwana kila mtu anataka pale alipo paheshimike.
 
Back
Top Bottom