Ni Jumatano tulivu.Kukiwa na maandalizi ya tukio kubwa la kisiasa kwa siasa za Tanzania.
Vijana wa CHADEMA katika majimbo yote 10 ya mkoa wa DSM watakwenda kumuomba rasmi Freeman Mbowe agombee kwa mara nyingine Uenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza na vyombo vya habari Mratibu wa kampeni ya #MwambaTuvushe Daniel Naftali Ngogo amesema vijana watakutana makao makuu ya chama Ufipa saa 4 asubuhi kisha itaanza safari ya kuelekea alipo Mbowe ili kumshawishi na kumkabidhi fomu.
Vijana wa Chadema wakiongozwa na Daniel Ngogo na Twaha Mwaipaya walianzisha kampeni ya kitaifa ya kuchanga fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu Mbowe na zikapatikana shilingi milioni 5 na laki 6.
Juzi Jumatatu maelfu ya vijana waliandamana kuelekea makao makuu CDM kumchukulia fomu Mbowe na kuvuta hisia za watu wengi.
Mbowe mwenye ushawishi na nguvu kubwa ndani ya CDM endapo kama atakubali wito wa vijana anatarajiwa kukumbana na wapinzani kadhaa wakiwemo Cecil Mwambe na Fredrick Sumaye wanaotarajiwa nao kupimana ubavu na mwamba huyo wa kisiasa nchini.