DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Nani kakudanganya ? Wewe subiri tu . Yani jiwe amtumbue makonda kisa huyu mtu wa kuja ?
Hii movie jiwe atajitokeza amtumbue mpango na awatumbue watu wa bandari then apate sifa yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
ile barua ya mpango aliyomjibu bashite kuhusu makontena kutokuwa na msamaha wa kodi nakala ilienda ikulu so ukiona ikulu imekaa kimya ujue mpango ameisha pewa go ahead mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpango alichofanya ni ku encourage watu waende kununua hivyo vifaa na hakumjibu Bashite

Sent using Jamii Forums mobile app
Akishaanza kuongelea habari za kwamba amesikitishwa na vitisho vya Mkuu wa Mkoa tayari kashajiingiza katika malumbano na Mkuu wa Mkoa na wananchi tunaoelewa "collective responsibility" katika serikali ni nini, tunaona wote wanakosea.

Bashite kakosea kwenye kosa la msingi la kujifanya yeye ni special case anatakiwa kuwa treated kwa sheria ya peke yake, Mpango kakoseakuendekeza malumbano ya kumtaja Mkuu wa Mkoa na positions zake through the media in public.

Ni vile tupo katika zamaambazo kazi za serikali hazina heshima tu, lakiniingekuwa zama za uongozi wa kujiheshimu, hapo Waziri hata kama anahimiza watu waje kununua, asingeongelea habari za Mkuu wa Mkoa, au angesema tu "ofisi yangu inawasiliana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuzungumza zaidi, lakini kwa sasa huu ni manada halali na wananchi msiwe na hofu"
 
Mm niko nchi gani?si ilisemekana haya makontena hayana mwenyewe,na yameingizwa kwa jina la Makonda,sasa inakuwaje yeye kuwajibishwa kuyalipia kodi?Mhh...nchi inatafunwa na wanaojitapa kumsaidia mwananchi mnyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa jambo la msingi ni kuwa tunajipanga kwenda kununua hayo makonteina tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitake kuwa neutral sema tu Bashite kakosea,Waziri hajarumbana na mtu bali katoa maagizo kwa watendaji wake.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono! Haiji akilini Mhe. Waziri unaenda hadharani kumpinga kiongozi mwenzako tena mbaya zaidi kwa kutumia mrejeo wa magazeti na vyombo vingine vya Habari. Kweli Tanzania tumelaaniwa!
 
Watanzania wote wanajua kwamba wale watu wasiojulikana walojaribu kumuua lussu ni vyombo vya ulinzi ambavyo makonda anavitumia, sasa Hao wateja hawaogopi Lana za makonda bali wanaogopa nao kujakupotea.
 
Ukiona Dk Mpango anaongea ujue kweli kaumia na maneno ya makonda, mpango hanaga muda mtu yeye ni kazi tu, na makonda anapoharibu asiwe anakimbilia kujificha kwa mungu au makanisani hii kitu ni mbaya sana,nani hamjui mungu? makonda ni mtumishi wa serikali anatakiwa afanye kazi sio biashara.
 
Usitake kuwa neutral sema tu Bashite kakosea,Waziri hajarumbana na mtu bali katoa maagizo kwa watendaji wake.!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungenisoma ungeshaona nilishasemahilounalosema niseme kitambo.

Inawezekana mimina wewe tuna viwango tofauti vya ustaarabu tunaoutegemea kutoka uongozi, na hilo si jambo la kustaajabisha kwa kuangalia nchi inavyokwenda.

Watu wana very low expectations, kiasi kwamba mtu akija na expectations za normal decorum na kutaka collective responsibility tu, anaonekana anaongea Kigiriki cha kale.
 
Hii mechi Kali tena ya fainali. Tuone kati ya bashite na waziri ,nani zaidi? Kwenye huu mpambano mtoto hatumwi dukani
Waziri ataondoshwa, bashite yuko Gambush anashikilia ndude za jiwe hafurukuti
 

Hii ni dalili Magufuli ameshindwa uongozi.

Haiwezekani nchi ikawa na kiongozi wa juu anayeheshimiwa na appointees wake, haalafu wakalumbana hivi hadharani.

Hatukuona haya enzi za Nyerere.

Bashite is a scumbag and all, but this makes the entire government look like a joke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…