Zemanga zoze
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,016
- 1,722
Kihele Helen cha madaraka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante,na nia yangu wanielewe wachache ikibidi Mello tu
Inawezekana alijisahau badala yakuandika Mkoa kaandika Makokonda akiamini yeye ndio mkoahivyo vifaa angevileta kwa jina la wizara ya elimu au kwa jina la ofisi ya mkuu wa mkoa na si jina lake shida ndo inaanzia hapo ,mwambie alipe ushuru tu !
Mwandishi yuko sawa Tanzania ni ngumu hata kuisaidia. Kwa wanaokaa TZ wengi hawawezi kuamini haya lakini sisi wa nje tunajua ndugu zetu. Tunaenda kwenye ma hospital na mashule kuombea vifaa mfano Ali ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Zanz ndiye aliyetuma hivyo vifaa cha ajabu akituma nchi nyingine hakuna hizi shida! Yuko seattle na watu wanajitolea kupakia kwenye makontena, watu wanachangia gharama za kutuma na storage halafu zikifika TZ eti tulipe kodi wakati vifaa ni vya watoto wanaokaa chini ndiyo wameomba. Sasa hiyo kodi ni ya nani kama haitasaidia watoto wanaokaa chini! Tulifikiri kodi ni kusaidia Watanzania.... Halafu watu hao hao wanasema sisi watu
Wa nje hatuna faida maana hatusaidii. Mna mkomoa nani Makonda yupo kwenye jumba la serikali, sisi tuko huku US anayepata shida ni yule mtoto. Sasa wazuri wakitucheka tutasema nini mlitaka watu wasaidiaje kutoa pesa tu ambazo zitaishia kwa wajanja..!
ahahahaha! !Inawezekana alijisahau badala yakuandika Mkoa kaandika Makokonda akiamini yeye ndio mkoa
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole. Inasikitisha sana na kukatisha tamaa. Na uuzwaji wa hivyo vitu utakuwa wa dili dili, yaani vitanunuliwa kwa bei ya ovyo then vitauzwa tena mitaani kwa bei kubwaWanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,
Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??
Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,
Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,
Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,
Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi
Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,
Britanica
Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.
View attachment 848681
Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.
"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.
Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.
"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango
Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.
Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.
"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango
View attachment 848680
Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.
Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.
Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
HakikaPole. Inasikitisha sana na kukatisha tamaa. Na uuzwaji wa hivyo vitu utakuwa wa dili dili, yaani vitanunuliwa kwa bei ya ovyo then vitauzwa tena mitaani kwa bei kubwa
kuna miradi kama wa reli ya SGR,waziri ameondoa kodi kwa samani za ofisi na majumbani wa wataalam wa mradi,unasemaje kwa hiloMkuu nina shaka na upenzi wako wa somo la sheria, kuna kifungu kipi kinampa waziri nguvu za kusamehe kodi kwenye samani? Nimesikia waziri akisema samani inabidi zilipiwe kodi kwa mujibu wa sheria.
walisema ngoma ikilia sanaaaaa. hii inapsuka! wajuzi wa mambo humu walimwambia bwana makonda/bashite juu ya tabia zake za kiburi na majivuno. aitishe tena mkutano wa ilani aeleze hili lipo ukurasa wa ngapi?Sheria si mnatunga wenyewe na kuzipitisha kwa kusema ndioooo!!Sasa hapo unashangaa nini?!
Alafu jiulize ni kwanini mwanzoni aliakana alafu baadae akayakubali?
We jua tu hilo ni dili limebumbuluka.
Kwaiyo umeona hiyo 1.2b ni ndogo kiasi cha waziri kuendelea kukaa Dodoma?Acha utoto wewe
Huyo mpango kaacha ofisi dodoma kaenda bandarini kushindilia container za Makonda tu?Basi hata kutumia ziara hiyo kuamuru na mizigo mingine yote inadiwe,lakini kwa kua anaongozwa kwa chuki mizigo mingine kwake si lolote hata ikikaa miaka 10
Ndiyo na nikaingia cha kike nikachanga kuputia CRDB 400 USDUkisikia utawala uliofitinika ndo huu, visasi na chuki nje nje. Yaani walimtumia mama wa watu kuuza sura kumbe wanaitafuta pesa waile, zile pesa kama kuna watu kulaanika lazima watalaanika tu
Uwezo mbona anao wa kununuaDk Mpango angeonesha njia kwa kununua angalau kontena moja kuthibitisha kwamba yeye haogopi vitisho vya kulaaniwa yeye na uzao wake.
Mwisho wa siku hizo fanicha zitaozea hapo bandarini wakose wote!
Nadhani shetani ni baba yako MalliaHii series hii inaonyesha magu kashamchoka Bashite na ndio maana wateuliwa wa magu hawatishiki kwa sasa, na napata uhakika sasa kuwa ni kweli Bashite akili zake hazipo sawasawa maana mara ya kwanza aliyakana hayo makontena kuwa sio yake akaja tena akisema kuwa ni yake na anaomba msamaha wa kodi na sasa anawalaani wanaoyapiga mnada wakati ni yeye mwenyewe mwazo aliyakana kuwa sio yake
Alafu ukimkuta kule insta anavyopost mambo ya kilokole huwezi mshtukia kuwa ni shetani mkubwa huyu
Sent using Jamii Forums mobile app