DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Mh! Masikini hana chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani hold on nani anaweza nunua container kwa value ya milion 60 kwa ajili ya viti na makabati? Na hivyo vitu ni kwa ajili ya shule au office! Time are hard, hayo ma containers hayatopata wateja! 20 containers mnataka mchukue kodi ya 1.2B! ( meaning kila kontena 60 million tsh), Never been fan of makonda I just hate the guy, but on this, its pure drama. No customers will come forth.
 
Makonda amepata wapi hela za kununua huo mzigo kutoka marekani jamani?
 
Ndivyo itakavyokuwa mkuu....

Na yakishataifishwa yatapelekwa kule alikotaka mwenye mkoa wake...hii ni sinema tu, script writer anajua mwisho wa muvi utakuwaje...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama alikuwa na nia njema. kwanini aandike majina yake? huyu mtu hajawahi kuaminika, kama mtu hata majina yake sio halisi unatarajia nini?
 
Hapa tusubiri yena kama baba atafumba macho. Maana mtoto habebeki tena kwa mbeleko. Ina kera sana huyu jamaa amejaa kashfa lakini baba hujifanya haoni. Ila kwa wengine hata kama ni tetesi mtu ana chinjiwa baharini... Tujiulize je na jili baba ata kaa kimya??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
makonda anajua vizuri njia na taratibu sahihi za kufuata ili hii kodi ipate kusamehewa ikiwa ni pamoja na kusalander documents zote zisomeke si kwa jina lake na ihakikishwe kuwa linafanywa hivyo.
kwenda kulalamika kwenye vyombo vya habari hili ni tatizo zaidi na sio njia ya kulitatua.
sidhani kama ni njia sahihi ya kupeleka miemko kwa jambo la msingi kama hili.
afuate taratibu kama viliagizwa kwa ajili ya shule za dar es salaam si wana accaunt yao walipe wakati wakifuatilia jinsi ya kuasamehewa kwa kukata rufaa?
 
Aliwahi kukana makontena sio yake, tukumbuke pia kuwa hata jina lake halisi alilikana! Sidhani kama anafaa kuaminika.
 
Kwamba husithubutu kuchangia inua familia yako tu
Kwanini vitu viwe addressed kwenda kwa Paul na sio ofisi ya mkuu wa mkoa?
Nia yenu ni njema sana lakini vipi kuhusu Paul,naamini jamaa hawajakurupuka bali kuna mchezo wameushtukia.
 
Inawezekana tukamshangilia Mpango kumbe kuna mpango wa ku-divert attention na kutusahaulisha machungu, ulemavu, vipigo tunavyopata kutoka kwa watawala ktk chaguzi za marudio hapa hapa nchini.....
 
Hao wenye elimu kubwa si ndio hao waliokuwa wanabuni miradi ya upigaji kama EPA,, ESCROW na uchafu mwingine wa aina hiyo!!?.

Hao wenye shule za maana si ndio hao ambao wanaendesha ma-vogue na magari ya milioni 400 wakati Mama zao vijijini wanajisaidia haja kubwa maporoni pembeni ya nyoka na chatu!!?.

Hao wenye shule nzuri si ndio hawa walioua mashirika makubwa mpaka yakawa yanashindwa kutoa gawio serikali kuu!!.

Hizi ndizo akili za mtanzania halisi, anajivunia elimu wakati hakuna cha maana ambacho elimu yake inaisaidia nchi hii.

Huyu dogo anaweza kuwa na matatizo yake binafsi lakini hizi juhudi za kuwatafutia waalimu furnitures, hizi juhudi za kusaidia kinamama wanaotelekezewa watoto, ni lazima Mungu atazilipa. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Serikali kupitia ofis ya magogoni naona inazidi kudhoofisha power ya makonda...

na huyu jamaa maadui aliowatengeneza ndio mtaji wake kwa sasa, asingekuwa na maadui wengi na hatar kwa afya yake, angishatumbuliwa kitambo..

ila mamlaka za uteuzi zinapata shida sana endapo zitamuondoa kwenye nafasi yake, ataishi vip huyu jamaa...

nadhan labda akafungue kikanisa aanze kujisafisha, maana anaonekana mahiri sana kwenye icho kieneo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…