DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Ujinga ni kushangilia magari ya kubebea wagonjwa yakizuiwa kutoka bandarini kisa kodi na kulalamika viti na meza za kukalia watu watu wenye afya zikizuiliwa bandarini kwa kutolipiwa kodi.
Kinachowasumbua nyinyi mnaojiita wazalendo ni unafiki uliopitiliza na adhabu mnayoipata ni kubwa kweli kwani hamjui msimamie sheria au matakwa yenu binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Go go go! Mpango....asikuyumbishe mtu......we huna hofu ya ajira kama hela unayo.
Simamia sheria....usiskilize maneno ya watu
Unless kwenye containers kuna other dubious business.
Ila kama ni sheria, kuna wakati Misri ilipitishwa sheria watoto wa kiume wasio Wa-misri wauwawe. Nayo ilikuwa sheria. Kama ni sheria, Mandela alifungwa gerezani kwa kama gaidi. Yet ilikuwa sheria.
Sote tunaheshimu sheria, ila kama zinatunjenga au kutubomoa hapo tuna jukumu kuulizana maswali
 
Taja misaada iliyotoka marekani ya mahindi, wakati kuna mahindi mengi Tanzania.
Usipende kuongea vitu visivyo na ukweli ili kuthibitisha vitu ambavyo havina ukweli.
Try another argument.
Mkuu, toka 2012 kuna mahindi yanaingia kwa mradi named food for education mkoani Mara. Beneficiaries ni Wilaya ya Bunda na Musoma vijijini. Fuatilia Wizara ya Kilimo au fika mkoani Mara.
 
This was my point! Ahsante kwa maelezo mazuri. Bashite aache kulialia afwate sheria kanuni na utaratibu tulio jiwekea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna taratibu zake,MTU binafsi akipewa msamaha akipeleka kwake huwezi mdai,mizigo imekuja Kwa jina lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kesi tofauti. Hii imetokea utawala mmoja. Hapa tunakoswa nguvu kuunga mkono bandiko lako .
 
NIA YAKE YA KUOMBA MSAADA WA SAMANI ZA SHULE NI NJEMA. TATIZO SHERIA ZETU ZA KODI HAZIJATOA MWANYA WA MSAMAHA WA KODI KWA BIDHA ZAA INA HIYO NA NIA YA SHERIA PIA NJEMA. NIA YASHERIA NI KUKUZA AJIRA ZA NDANI ILI VIJANA WETU WAPATE AJIRA ZA KUTENGENEZA SAMANI ZA OFISI HUMU HUMU NCHINI NA PIA WAKULIMA WA MBAO KULE NJEMBE, IRINGA, LUSHOTO NA KWINGINEKO WAPATE SOKO LA BIDHAA ZAO. UKITOA MWANYA WA MSAMAHA KATIKA ENEO HILO WATU WABAYA WANAWEZA KUTUMIA MWANYA HUO KUINGIZA BIDHA ZA MBAOTOKA NJE YA NCHI NA KUUA AJIRA ZETU HUKU NDANI. KATIKA HILI KWA KWELI AMA MHE. MAKONDA ATAFUTE WADAUWA KULIPA KODI YA SERIKALI AU AU TUPELEKE MSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA BUNGENI ILI KUMPA MAMLAKA YA KISHERIA WAZIRI WA FEDHA KUTOA MSAMAHA WA KODI KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA YA MAKONTENA YA MHE.MAKONDA.
 
Nchi za watu alitakiwa ajiuzulu sema bongo atapeta. Hawa si ndiyo huapa "nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko"!!?
 
Mkuu naona unaendeleza siasa nyepesi za mitandaoni. Una uhakika gani kama hana marafiki huko nje.

Kibaya zaidi kuna watu wa Diaspora wenye nia njema na nchi yao, lakini upuuzi unaokuwa unaendelea humu nchini unawakwamisha na kuwakwaza katika lile wazo la kuiendeleza Tanzania.

Kumbuka kuwa walimu ndio wametuwezesha hata kuweza kuandika chochote humu jukwaani. Labda ulikuwepo ukosefu wa mawasiliano kati ya RC na serikali kuu na labda ndio yaliyosababisha haya yanayoendelea kwa sasa.

Punguzeni kiburi cha kijinga, jifunzeni kutazama pande mbili za kila tukio.
 
serekali inahimiza tusomeshe watoto ili baadae watumie elimu yao kwa ajili yao wenyewe na taifa.

sasa kwa mfano....usiku wa manane nimekwenda pale NBC nikavunja safe ya benki na kupora pesa kwa ajili ya ada ya watoto.... je, sitashitakiwa jinai kwa kuwa tu nia ya uporaji huo ni njema?

nauliza tu.
 
Mtoto kanyea mkono, haukatwi utaoshwa tu na maisha yataendelea. Fanyeni kazi
 
Kwani si alipe tu hiyo kodi, maana ya kaisari ni ya kaisari tu siku zote,

Angefata taratibu za uingizaji mbona tusingekuwa na hizi mbwembwe, angewaachia mashirika yasiyo ya kiserikali ziingize hizo mambo km misaada mbona tungeshangilia, ila sasa kwa kuwa sheria ni msumeno ukiingiza makontena kwa jina lako umeshakuwa mteja wa nchi na unatakiwa kulipa kodi yake, so ailipe tu walimu wakapige kazi,

Huku kulalamika ni kufanya MAZOEA kuwa HAKI, nakubali wazo lake la kuleta fanicha ila sijakubali njia aliyotumia kuzileta hizo kontena, amejifunga kwa kutojua au kujua protokali za kuagiza vitu kutoka nje, na wanasheria wanasema kutojua sheria ni kosa pia na utahukumiwa kutokana na kosa,

Anachofanya Mh Mpango ni kufuata sheria, maana ukishaweka upenyo huu kuruhusu msamaha kwa kisingizio cha kunufaisha watanzania kuna watu wengi tu watafuata huu upenyo na watashinda kesi zao, wataagiza kila kitu kwa mgongo wa msaada na watadai msamaha na watashinda kesi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe acha uongo, misaada ikiingia kwa mgongo wa mashirika ya misaada inapewa msamaha wa kodi, ipo kwenye sheria. Ila sheria hiyo hiyo haimruhusu raia binafsi kuingiza mizigo kwa kisingizio cha msaada kwa jamii, lazima uilipe kodi yake, mbona ishu iko wazi sana,
Mh Makonda awaambie tu watanzania wachange tu hiyo kodi ipatikane, lasivyo awaambie diaspora tushirikiane na watanzania wamchangie ipatikane kodi, serikali kila mara inasema lipeni kodi, ndo tuilipe sasa, tusione mkuki mchungu sana ukitugonga sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaohitaji viti na meza ni wanafunzi, walimu wanahitaji mishahara iongezwe pamoja na madeni wanaoidai serikali yalipwe
 
Ndo hicho nilichokuwa nakiongelea [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…