Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mkuu tumekuwepo nchini muda mrefu sana na tunaweza kumtambua mwanasiasa mwizi kwa mbali sana.Mkuu naona unaendeleza siasa nyepesi za mitandaoni. Una uhakika gani kama hana marafiki huko nje.
Kibaya zaidi kuna watu wa Diaspora wenye nia njema na nchi yao, lakini upuuzi unaokuwa unaendelea humu nchini unawakwamisha na kuwakwaza katika lile wazo la kuiendeleza Tanzania.
Kumbuka kuwa walimu ndio wametuwezesha hata kuweza kuandika chochote humu jukwaani. Labda ulikuwepo ukosefu wa mawasiliano kati ya RC na serikali kuu na labda ndio yaliyosababisha haya yanayoendelea kwa sasa.
Punguzeni kiburi cha kijinga, jifunzeni kutazama pande mbili za kila tukio.
Njia ya kijinga na ya kwanza ni mwanasiasa kujidai ana uchungu sana na kada fulani ya watu masikini, wakati hasa ni kupiga cha juu.
Hiyo huruma ni changa la macho.
Makonda huyu huyu ambaye majuzi(less than 10 years) alikuwa hana kitu, leo ana ma VX, BMW na mali za kutisha, na baadaye anawaagizia wananchi wake makontena zaidi ya 20 ,samani za shule?
Mtu ukipumbazika na hilo, basi una matatizo ya kimsingi.
Hela isiyopatikana kihalali daima kama jipu, linajitokeza ili lipasuke.