DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wengi sasa tunajua kuwa kuna sakata la makontena 20 yanayoshikiliwa na TRA yakidaiwa kuingizwa nchini kwa jina binafsi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Mnada wa makontena hayo, kwa mujibu wa gazeti la leo la Mtanzania, umepangwa kufanyika tena mnamo Septemba 1 mwaka huu yaani Jumamosi ijayo.

Kwa mujibu wa maelezo ya upande wa Makonda yaliyoripotiwa, inadaiwa kuwa makontena hayo 20 yana samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam zilizochangwa na kuingizwa nchini na watanzania wema waishio nje ya nchi almaarufu kama Diaspora. taarifa zinadai kuwa wanaDiaspora hao walichanga na kuleta samani hizo ili kuunga mkono juhudi za Rais na Mkuu huyo wa mkoa wa Dar za kuboresha elimu.

Iko wazi kuwa JamiiForums ni mtandao wa kijamii wenye wanachama kila kona ya dunia hii. Kuanzia watanzania hadi wale wasio watanzania wamekuwa wanachama wa mtandao huu. Katika kusema hivyo, wapo wana-JF ambao ni wanaDiaspora mfano mtani wangu Nyani Ngabu anayesemekana kuwepo nchini Marekani. Ndiyo maana nimeona vyema kuwauliza wanaDiaspora kokote walipo, kama 'wachangiaji' wa makontena 20 yanayohusika maswali yafuatayo ya lazima.

Mosi, ni kweli kuwa wanaDiaspora ndio waliochanga na kufanikisha kuletwa kwa makontena yaliyo mikononi mwa TRA? Pili, makontena hayo yamebeba bidhaa gani hasa? Tatu, mlengwa wa makontena hayo na bidhaa zake ni nani? Nne, kwanini yaliingizwa nchini kwa jina binafsi la Paul Makonda na si Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Wizara au Taasisi yoyote ya kiserikali? Na tano, watumaji mliambiwaje kuhusu kodi ya bidhaa hizo ili ziweze kutoka mikononi mwa TRA?
NPO SITI YA MBELE HAPA.... naenda kutafuta POPCONE
 
Heading na kilichomo tofauti!!
Uache tabia yako ya kutuvutia kusoma thread yako na hali unajua umeandika MASHUDU😡😡😡😡
 
Mosi, ni kweli kuwa wanaDiaspora ndio waliochanga na kufanikisha kuletwa kwa makontena yaliyo mikononi mwa TRA? Pili, makontena hayo yamebeba bidhaa gani hasa? Tatu, mlengwa wa makontena hayo na bidhaa zake ni nani? Nne, kwanini yaliingizwa nchini kwa jina binafsi la Paul Makonda na si Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Wizara au Taasisi yoyote ya kiserikali? Na tano, watumaji mliambiwaje kuhusu kodi ya bidhaa hizo ili ziweze kutoka mikononi mwa TRA?

Mpaka sasa wanaoitwa WanaDiaspora kimya.Hili nalo linaacha maswali.
Pili Documents zakuingiza mzigo zinasemaje???
 
Mkuu ipo wazi kama sio kujitengenezea maadui wa madawa ya kulevya,makonda angekuwa ameisha tumbuliwa
.
Basi tuseme kila mtu aweke sababu ambazo zinapelekea mpaka sasa Makonda hutumbuliwi,asilimia 98 watasema madawa ya kulevya sio kitu kingine..akitumbuliwa sasa hivi maisha yake yatakuwa hatarini

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu kubwa ni kuwa anashirikiana na mukulu. Kwa makonda sikuona mapambano yoyote dhidi ya madawa ya kulevya zaidi ya kutaja taja mateja. Hana adui wa hivyo isipokuwa yeye ni partner wake.....
 
Mkuu umezisoma hoja za Dr. Mpango katika barua aliyomjijibu Mh. Paul Makonda juu ya ombi lake la kutaka kupewa msamaha wa kodi wa mzigo huo?

Je katika barua hiyo umeusoma vizuri ushauri alioutoa Dr. Mpango kwa Mh. Makonda ili Mzigo huo apate Tax execemption?

Je kwa nini Mh. Makonda hakufata ushauri huo aliopewa toka May mapaka leo.

Sheria ni sheria tu. Kama tunashindwa kusimamia sheria ndogo kama hizi tulizojiwekea, vipi sheria katika maswala makubwa?

Ndio hicho nilichokisema kwamba siamini serikali yetu sio waelewa au wakatili kiasi ambacho tunataka kuaminishwa.

Kuna mahali taratibu zimekiukwa.
 
Kwa hiyo Bashite hata akimchapa kofi Mteule wa rais hadharani hatamtumbua?

Kuna watu wanarisk maisha yao kupambana na ujambazi na magenge hatari au kuiweka nchi salama lakini wanakuwa na nidhamu. Kazi zao siyo kinga ya kufanya upuuzi kwa hoja kuwa mamlaka za juu yao zitawavumilia!

Bashite kama anapendwa sana basi apangiwe kazi nyingine, kama anampenda sana apewe jimbo akagombee, kisha atangazwe na Mkurugenzi, baada ya hapo amtoe Kasimu amuweke yeye!. Naamini kwa cheo kama cha Kasimu atakuwa na ulinzi mzuri zaidi au vipi?
Basi wakuu wa kitengo cha madawa ya kulevya wawekewe ulinzi na wasistaafu maana was wanapambana siyo kwa kibahatisha Bali pia kwa kutumia teknolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diaspora hawawezi kuchangia pesa ndefu kama hiyo ............ michango tu ya misiba ni issue!!

Kwanza kufanikisha kitu kama hiki tungesikia siku nyingi kabla hata ya macontainer kufika Bongo. Ingewezekana kabisa wangekabidhi rasmi kwa kiongozi wa serikali ............!!
 
Ni ufahamu mdogo wa taratibu za uagizajia
mizigo ya misamaha ya kodi
Pili ni kujiona kila ulifanyalo liko sawa hata kama si kwa mamlaka yako , hayo yote tunaita ukurupukaji wa kila jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wapo duniani kama bendera hawajahi tumia japo punje ya ubongo wao kwasababu ya mahaba.

1. Yale makontena yamebeba viti vya ofisini wala si madawati, Niambieni ni shule gani wanakalia viti vya kuzunguka?
2. Uagizwaji Wa makontena haukuzingatia taratibu, niambieni tangu lini msamaha umeanza kutolewa kwa huruma ya walengwa?
3. Kwanini mwenye Makontena aliyakana pale mwanzo?
4. Yakiachwa yapite Bure Tutakuwa tumewafundisha nini Wasimamizi Wa forodha na ushuru kwa vitu visivyo zingatia utaratibu?
5. Kwanini yaliandikwa jina la Makonda (Personal)?
===============
NOTE; Mtoto hata ukimkalisha kiti cha mwalimu Mkuu haina maana ndiyo atajua kusoma na kuandika
1535611629193.jpeg
 
Mkuu MAGACHA ,ndiyo hiyo sababu moja tu? Ulikuwa na haja gani kusema sababu ni hizi hapa kama ipo moja? Nadhani,kawaida wananchi kama wewe hupiga ramli chonganishi. Kimsingi,ni Rais tu ndiye anayejua kwanini amemteua au kwanini amtumbue/asimtumbue.

Umejiuliza lengo hasa ya kuweka hiyo sababu?
Defense mechanisms?. Kuonewa huruma?.
 
Back
Top Bottom