DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Ungesoma kichwa cha hii thread kwanza. Nakubaliana na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama mleta mada heading inakinzana na content inatakiwa afute uzi!
Makonda aipa sifa mbaya serikali ya jpm.

Hapa unataka usome content ili ugundue nini wakati upuuzi wa hawa wawili unajulikana, hawana hekima wala woga wamefanya nchi kama familia yao.
 
  • Wateule wako ambao ni Waziri wa Fedha (Phillip Mpango) na Mkuu wa Mkoa wa Dar (Paul Makonda alias DAB) wanaparurana hadharani
  • Mmoja anasimamia sharia za kodi; mwenzake analialia kusaka huruma yako na ya wananchi ya kujichora kama anayeonewa na kukwamishwa.
  • Wizara ya Fedha na TRA walitishwa na DAB kushtakiwa kwako lakini wameng'ang'ania upande wa kusimamia na kutekeleza sharia za kodi kuyahusu makontena.
  • Waziri wa Fedha ameponda waziwazi laana ya DAB kuhusu wanunuzi kwenye mnada wa makontena.
  • TRA wameshaelekezwa na Waziri wa Fedha kuendelea na mnada kama ulivyopangwa. Tarehe ya mnada uliotishiwa kuwa na laana ni 1/9/2018
  • Nyaraka za kiserikali kutoka Ofisi ya DAB kuyahusu makontena sasa zinaanikwa mitandaoni katika kumtetea DAB.
  • Wateule wako wanatunishiana misuli ya mwili na akili na wananchi wanamsubiri mshindi na mshindwa.
Pamoja na yote hayo, bado Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM umekuwa kimya. Hukusema wala hukufanya lolote hadi sasa. Tangu kuanza kwa sakata lenye utata la makontena. Ukimya wako unamaanisha nini? Sema au tenda jambo moja ili tuujue msimamo kuhusu jambo hili.

Uchaguzi unaotokana na ununuzi na wenye uchafuzi wala haunogi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Usiwe Na wasiwasi Chuma kimeanza Ziara Mikoa ya kanda ya Ziwa jibu utalipata
 
Hawezi toa neno lolote anaacha wajichanganye hapo yupo anaandaa waziri mwingine ukija kumsikia basi ujue anatangaza uteuzi mpya
 
Maisha yanaenda kwa kasi sana yani!...yani Mkuu wa Mkoa wazi wazi kabisa anabishana na Waziri anayehusika na jambo lililo chini yake!...na hata baadhi ya Mawaziri kufyata mkia kwa RC!

Tunazeeka kwa kasi sana aisee!

Zamani haya mambo usingeweza yadikia achilia mbali kuwaona kwenye Magazeti wakivuana nguo!
 
Tiyari akiwa chato amesema Makonda alipe Kodi.
 
  • Wateule wako ambao ni Waziri wa Fedha (Phillip Mpango) na Mkuu wa Mkoa wa Dar (Paul Makonda alias DAB) wanaparurana hadharani
  • Mmoja anasimamia sharia za kodi; mwenzake analialia kusaka huruma yako na ya wananchi ya kujichora kama anayeonewa na kukwamishwa.
  • Wizara ya Fedha na TRA walitishwa na DAB kushtakiwa kwako lakini wameng'ang'ania upande wa kusimamia na kutekeleza sharia za kodi kuyahusu makontena.
  • Waziri wa Fedha ameponda waziwazi laana ya DAB kuhusu wanunuzi kwenye mnada wa makontena.
  • TRA wameshaelekezwa na Waziri wa Fedha kuendelea na mnada kama ulivyopangwa. Tarehe ya mnada uliotishiwa kuwa na laana ni 1/9/2018
  • Nyaraka za kiserikali kutoka Ofisi ya DAB kuyahusu makontena sasa zinaanikwa mitandaoni katika kumtetea DAB.
  • Wateule wako wanatunishiana misuli ya mwili na akili na wananchi wanamsubiri mshindi na mshindwa.
Pamoja na yote hayo, bado Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM umekuwa kimya. Hukusema wala hukufanya lolote hadi sasa. Tangu kuanza kwa sakata lenye utata la makontena. Ukimya wako unamaanisha nini? Sema au tenda jambo moja ili tuujue msimamo kuhusu jambo hili.

Uchaguzi unaotokana na ununuzi na wenye uchafuzi wala haunogi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Huna lolote unataka upate chakuongea
Chochote kile asemacho lazima utapinga
 
Back
Top Bottom