DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Beloved son! otherwise dad is coming
 
Mpango lazima awang'oe dadeeek sijui utakula wapi maana akifukzwa Bashite nawe unakosa kibarua

Sent using Jamii Forums mobile app
Tehe tehe labda kama hatuhitaji elimu bure
Kila siku Rais anasema kuna viongozi hawamuelewi,wanabishana wao kwa wao kwa ajili ya kazi ya serikali.
Sheria imempa nguvu waziri wa fedha kusamehe kodi kwa kutoa Government notice na kuichapisha katika gazeti la serikali
Mpango anaudanganya moyo wake kwamba hizo container 20 ni za Makonda zikitoka zitaenda kuuzwa congo,huku akili yake inajua kabisa makonda aliomba msaada kwa niaba ya serikali
Watu warasimu kama akina Mpango hawatufai kwa sasa
 
Unaongea ugoro wewe yaani mpango na wewe nani anajua mipango ya serikali?njaa imekupanda kichwani sasa umebakia kuwayawaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo la aibu kabisa kwa watendaji wa serikali moja, chama kimoja, wameteuliwa na rais mmoja, wanalumbana wazi wazi kama watoto wasio na adabu.

Jambohili linaonesha udhaifu wa serikaliyetu,haifanyi maamuzikwa pamoja na kuzingatia "collective responsibility".

Kila mtu anafanya maamuzi kivyake.

Na panapotokeamgongano, viongozi hawana ukomavu wa kuongea na kumaliza tofauti zao kwenye vikao vya ndani.

Wanagombana kwenye vyombo vya habari kama wendawazimu.

Hapo, kitu cha kwanza kabisa, sijalinani yukosawana nani kakosea, kule kulumbana hivi tu, kunawafanya wote wawe wamekosea.

Kama viongozi wakubwa kabisa wa serikali wanatoa mfano huu, watoto wa shule ya msingi wanajifunza nini hapo?
Mkuu kwa jambo hili ipo wazi Makonda kakosea.
Anaweka vitisho kujaribu kuzuia kutekelezwa kwa sheria halali sio tamko binafsi la kiongozi flani.

Alichofanya Dk. Philip Mpango ni kwenda kuondoa wasiwasi kwa umma ili sheria ikitekelezwa basi mali ziuzike bila shida.

Hapo waziri kaenda kufanya kazi ya mawasiliano kwa umma. Angeweza kumuagiza afisa alie chini yake lakini huyo anaweza kuwa chini kiitifaki kumpinga mkubwa wake kiitifaki.
 
Wakitaka makontena yanunuliwe basi wamuhamishe wampeleke Songea, Rukwa au Mtwara.

Mark my words, the move is coming soon!
 
kwani kutokana na sheria za kodi raisi si anauwezo wa kutoa msamaha wa kodi kwenye bidhaa yoyote anayoona inafas kupewa kodi kwanini yuko kimya asimsaidie raisi wa dareesalaam akaamuru tax exemption kama kweli mzigo ni wa msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakua KIPARA NGOTO/NGOSO mkuu.
Kwa hakika suala hili linaonyesha jinsi Daudi Bashite aka Paul Makonda alivyo kilaza. Mtu yeyote aliye makini kabla hajaagiza kitu kutoka nje angependa kufahamu kiasi gani cha kodi kitalipwa. Kama Bashite aliamini kwamba angepata msamaha, angethibitisha hilo na TRA au Waziri. Lakini hakufanya hivyo. Kibaya zaidi samani hizo zimekuja kwa jina lake na si kwa jina la taasisi. Ama kweli kuwa kilaza ni mzigo!
 
KIKI
 
Ni jambo la aibu kabisa kwa watendaji wa serikali moja, chama kimoja, wameteuliwa na rais mmoja, wanalumbana wazi wazi kama watoto wasio na adabu.

Jambohili linaonesha udhaifu wa serikaliyetu,haifanyi maamuzikwa pamoja na kuzingatia "collective responsibility".

Kila mtu anafanya maamuzi kivyake.

Na panapotokeamgongano, viongozi hawana ukomavu wa kuongea na kumaliza tofauti zao kwenye vikao vya ndani.

Wanagombana kwenye vyombo vya habari kama wendawazimu.

Hapo, kitu cha kwanza kabisa, sijalinani yukosawana nani kakosea, kule kulumbana hivi tu, kunawafanya wote wawe wamekosea.

Kama viongozi wakubwa kabisa wa serikali wanatoa mfano huu, watoto wa shule ya msingi wanajifunza nini hapo?
Hii ni poul Makonda not RC against wizara ya fedha sio mamlaka mbili za uteuzi kulumbana ni mamlaka v/s mtu binafsi ambaye alishapewa utaratibu lkn hajafata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom