DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Kama kungekuwa na laana, Bashite asingekuwepo juu ya uso wa dunia mpaka sasa.

Watu kama hawa ndio wanafanya wakati mwingine ukristu uonekane kama kituko.Hivi, Yesu baada ya kufa msalabani bado kuna laana? Ina maana kazi yote aliyofanya Kristu pale msalabani haikufua dafu?

Hivi inawezekanaje, Babu ale dhabibu na kisha ganzi lije kumuibukia mjukuu? Ni hivi, laana ishindwe kumpata yeye Makonda anayetaka kuikosesha serikali mapato, ije iwapate watakaonununua hayo makontena na kuifanya serikali ipate mapato ambayo yalitaka kupotea?

Ndio maana tunawaambia kuwa makanisa ya kujiundia yana matatizo na mara zote hayawaachi wahusika salama.
 
Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Mpumbavu mbona yeye hajabeba laana kwa kuwa kinara wa sekeseke za kisiasa na upotevu wa watu.Shame on him.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dk Mpango angeonesha njia kwa kununua angalau kontena moja kuthibitisha kwamba yeye haogopi vitisho vya kulaaniwa yeye na uzao wake.
Mwisho wa siku hizo fanicha zitaozea hapo bandarini wakose wote!
Sheria inaelekeza, ikitokea imeshindikana kuuza kwa mnada, basi serikali itaamua namna ya kugawa hizo samani.

Msingi hapa ni kwamba hizo samani zikitaifishwa basi nchi nzima kwa ujumla itanufaika na hizo samani na sio Dar pekee.
 
Hakuna aliye juu ya sheria kama alitumika kumg'oa nape safari hii amegonga mwamba atakwenda yeye na vitisho vyake!
Nani kakudanganya ? Wewe subiri tu . Yani jiwe amtumbue makonda kisa huyu mtu wa kuja ?
Hii movie jiwe atajitokeza amtumbue mpango na awatumbue watu wa bandari then apate sifa yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa naona AKITUMBULIWA muda si mrefu. Nimesikiliza habari Azam, Dr. Mpango yaonyesha amekasirishwa sana na kauli ya bbMakonda eti atalayenunua hizo samani alaaniwe.
Hivi kwa hiyo HATAKI kulipa kodi na hataki sheria ifuatwe kwa wanaoshindwa lipa kodi? Sidhani kama ana siku nyingi huyu, atafute kazi nyingine mapema sana ya kufanya.
 
Dk Mpango angeonesha njia kwa kununua angalau kontena moja kuthibitisha kwamba yeye haogopi vitisho vya kulaaniwa yeye na uzao wake.
Mwisho wa siku hizo fanicha zitaozea hapo bandarini wakose wote!
anunue kwani yeye ana shule? Zipo taasisi nyingi tu zinaweza kununua kwa matumizi yao.
 
System ina mpango wa kumwondoa Bashite. Bashite ameshachokwa tayari.
 
Ni jambo la aibu kabisa kwa watendaji wa serikali moja, chama kimoja, wameteuliwa na rais mmoja, wanalumbana wazi wazi kama watoto wasio na adabu.

Jambo hili linaonesha udhaifu wa serikali yetu, haifanyi maamuzi kwa pamoja na kuzingatia "collective responsibility".

Kila mtu anafanya maamuzi kivyake.

Na panapotokea mgongano, viongozi hawana ukomavu wa kuongea na kumaliza tofauti zao kwenye vikao vya ndani.

Wanagombana kwenye vyombo vya habari kama wendawazimu.

Hapo, kitu cha kwanza kabisa, sijali nani yuko sawa na nani kakosea, kule kulumbana hivi tu, kunawafanya wote wawe wamekosea.

Kama viongozi wakubwa kabisa wa serikali wanatoa mfano huu, watoto wa shule ya msingi wanajifunza nini hapo?
Bashite ndiye hafai kuwa kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom