DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Nimetokea kumfuatilia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda kwamba kila anapojua kuwa kafanya tukio au tendo baya la Kumuudhi Mteule na Bosi wake Mkuu Rais Magufuli na ambalo linaudhi na kukera katika Jamii basi Yeye Kesho yake au wiki hiyo au ijayo atahakikisha anafanya tukio moja Kabambe sana la Kimaendeleo kisha anawaita Waandishi wa Habari walichukue na wahakikishe linasambaa ambapo humfikia kwa urahisi sana Bosi wake na kumfanya awe mzito sana Kutengua Uteuzi wake hivyo kujikuta akiendelea tu kumuacha huku wengi wetu tukinuna hadi mishipa ya Fizi inatukakamaa na Makonda anaendelea zake tu Kupeta madarakani.

Tukubali tukatae ukweli ni kwamba japo tunamcheka na kumdhihaki kuhusu Elimu yake na uwezo wake wa Kiupeo lakini kwa matendo yake na Ujanja wake anaoufanya nina uhakika anawazidi Wasomi wengi mno wenye sijui Degree, Masters na PhD's zao na kuna uwezekano mkubwa kwamba pengine wengi wetu tunaojiita Wasomi tungepata tu ujanja alionao Mkuu wa Mkoa Makonda basi huenda leo hii Tanzania ingekuwepo mbali sana Kimaendeleo.

Huyu Jamaa ni Mjanja sijapata kuona na acheni tu Rais Magufuli awe mzito Kumtengua kama RC. Tutanuna na Kukasirika sana ila Jamaa ndiyo Kwanza anachanja zake mbuga tu huku kila Kukicha Kujiamini Kwake kukiongezeka na akiendelea Kuaminika hali ambayo inamfanya Bosi wake azidi Kumuamini na Kumpenda.
 
Mimi kiukweli nipo hivi… .

Nilifundishwa kupenda maendeleo na wazaz wangu hvyo pia napenda mtu anayependa maendeleo…

Makonda amekuwa mpenda mwendeleo pamoja shutuma kibao lakini anapambana watu tumekalia maneno tu kumsema… ..

tufike mahali tuwe wakweli elimu sio kila kitu ila akili ndio kila kitu… ..

Nchi yetu inaponzwa na siasa za ubaguzi yaani tunaangalia nani kafanya na yupo upande upi upuuzi mtupu tufike mahali tuache siasa kwenye maendeleo… ..
 
Mwanamtandao Mashuhuri Afrika Mashariki na kati mwanadada Mange Kimambi amesema taarifa alizopenyezewa ni kuwa makontena 20 ya Makonda yamebeba furniture kwa ajili ya hoteli yake.

Mange amesema kwenye hayo makontena kuna hadi vitanda!
IMG-20180829-WA0019.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wanaochambua issues na siyo kujadili mtu/majungu Makonda ni Kiongozi mbunifu na ambaye kila Kiongozi mkubwa angependa kuwa naye kwenye safu yake ya Uonhozi.
Tatizo kubwa Tanzania MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA AU UJANGILI NI KITANZI.
Mhe. Makonda alikosea step alipojiingiza kwenye Vita ya Dawa za Kulevya, hakika hio vita haijawahi kumwacha mtu salama walahi, kikubwa wale wanaomuunga Makonda mkono waombee tu Mhe.Rais awe na maono vinginevyo drug dealer watatumia mpaka tone la mwisho kumwondoa. Kuna madon wako lupango leo unadhan hiyo vita ndogo. Pole sana Mhe. Makonda ulipaswa kusoma alama za Nyakati kwa mwezio Mhe. KAGASHEKI alichofanywa baada ya Vita ya Ujangili JK hajui kilichotokea mpaka akamtengua alikuja kujua baaadae kwamba alichezewa rafu.
Brother Makonda pambana werevu wooote wanajua mawe unayopopolewa yametoka wapi. Aluta Continua
 
Back
Top Bottom