Dar: Mahakama kuu yatupilia mbali kesi ya Halima Mdee na Wabunge wenzake 18. Sasa kupoteza Ubunge

Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 wa CHADEMA waliovuliwa uanachama na chama hicho, hivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea.
Tumsubirie sasa Tulia atulie na kutuliza kitulizo chake
 
Paskali Malaya uko wapi.

Ukuje huku ujue nchi inatawaliwa kwa misingi ya sheria na syo udikteta kama ilivyokua mjombako marehemu na ndugai
 
Tupe Basi kilichojiri au ulijifurahisha kuweka pambio
Mahakama ime struck out! Means kesho tuu watafaili upya kwakua the matter was not finaly determined rather iliondolewa for being defective.
..
Baada ya kuwepo mapingamizi ya awali ya kisheria, moja ya mapingamizi hayo ni kua
.
Walishitaki BOARD OF TRUSTEES OF CHADEMA BADALA YA REGISTERED TRUSTEES OF CHADEMA.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hukumu tayari kwani serikali haiwezi kukubali kuwapoteza wabunge hao kutokana na hitaji la kikatiba la Kamati za Bunge.
Hayo ni miongoni mwa makubaliano na Mbowe katika mkutano wa Ikulu kwamba hao wabunge waondolewe.Kwa hiyo tayari hao majaji wamekwisha elekezwa.Jaribu kufikiria tu,kwamba kwani wakina Halima ndio wa kwanza kufukuzwa kwenye chama na kwenda mahakamani?Watu wengi tu hawajawahi kushindwa hizo kesi.Zitto ,wabunge wa CUF wote waliishi na hizo kesi.Hayo ni miongoni mwa makubaliano ya Hangaya na Mbowe.Tutaona makubaliano mengi yanakuja
 
Kibibi wa Chadema unakenua meno tu.
 
Kuna wakili junior , amepata mteja mzuri tu, wamefile kesi commercial court.
.
Filing fee ya ile kesi ilikua 6.5 milion , na kesi imekua struck out kwakua kushindwa kufata font inayoelekezwa na commercial rules katika uandaaji wa document.
.
Kimsingi namhurumia Huyo Wakili ataenda ongea nini kwa mteja wake apate pesa ya kufile upya. [emoji19][emoji19][emoji19]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…