Dar: Mahakama ya Kisutu yajiweka kando kutoa uamuzi kesi ya Dkt. Slaa, Hakimu adai anafungwa mikono na Rufaa ya Jamhuri

Dar: Mahakama ya Kisutu yajiweka kando kutoa uamuzi kesi ya Dkt. Slaa, Hakimu adai anafungwa mikono na Rufaa ya Jamhuri

Unatafunwa na laana, kuna waliokua na mdomo sana wakati wa utawala wa mwendazake kuliko wewe , walipigwa na kitu kizito na kupoteana apa jf , usishabikie uhovu kwa ya kumtegemea mwanadam, mambo hubadilika
Uovu anao Slaa na badooo
 
Kuingilia lissu swala hili limezidi kuwa gumu
Kitu unachofanya ni kukiri kuwa mahakama zinafanya kazi kwa kukomoa na siyo kufuata sheria. Na hii inazidi kudhihirisha kuwa mwafrika (mtu mweusi) hajafikia level ya kujiongoza mwenyewe kama walivyokuwa wanasema wakoloni. Haiwezekani serikali iingie kwenye mchezo wa kukomoa badala ya kuongoza. Na zaidi tuna rais shangingi asiyejua ABC za uongozi. Madhara ya huu ujinga yatakwenda mbali na yatawapata watu wote bila kujali dini, jinsia wala chama.
 
Uamuzi uliotarajiwa kutolewa leo Januari 31, 2025 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenye shtaka linalomkabili Dkt. Wilbrod Slaa ikiwa ni baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuagiza shauri la Dkt. Slaa lirejeshwe Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake umeshindwa kutolewa.

Hoja iliyoelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki kukwamisha uamuzi huo ni kuwa, Jamhuri imekata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa, hivyo wanafungwa mikono katika kutoa uamuzi mpaka majibu ya rufaa hiyo yatakapotolewa.

Kufuatia uamuzi huo baada ya mabishano ya kisheria, Wakili upande wa mshtakiwa, Peter Madeleka ameeleza kuwa yeye na timu ya mawakili wengine wa utetezi hawajaridhishwa na maamuzi hayo kwani uwepo wa rufaa bado hauzuii haki zingine za msingi za mshtakiwa kama dhamana.

Itakumbukwa leo Januari 31, 2025 ilitarajiwa kutolewa uamuzi wa pingamizi la uhalali wa hati ya mashtaka, ambapo kwa mujibu wa mwendo wa kesi hiyo endapo ingefanyika hivyo ndipo mahakama ingeweza kiendelea na shauri juu ya dhamana ya Dkt. Slaa.

Kwa sasa mtuhumiwa huyo ambaye leo hakuletwa mahakamani kutokana na kilichodaiwa kwamba kulikuwepo na changamoto ya gari iliyotakiwa kuwapeleka washtakiwa Mahakamani, hivyo anaendelea kukaa rumande.
Wameamua kumuonyesha nguvu ya dola huyo mzee.

Kama mti mbichi unafanyiwa haya, je mti mkavu si itakua balaa??
 
Back
Top Bottom