Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Nchi ilipitia kipindi kigumu sana.
Mbaya zaidi, wananchi wakakubali kuwa manipulated...

Na tatizo zaidi, watu huwa hatutaki kutafuta ukweli kutoka kwenye vyanzo tofauti!! Tunasikiliza sana wanasiasa, bila kujali credibility ya kile ambacho kimesemwa!!
 
Mama Samia anaupiga mwingi sana. Hizi takwimu zimetolewa na Bank kuu ya Uganda na zinaonesha ni jinsi gani sasa tunafanya vizuri kiuchumi kwenye ukanda huu.

Ninachompendea huyu Mama pamoja na mafanikio yote hakuna majivuno Hakuna makelele ya kujisifu wala nini. Anapiga show kimya kimya.

Huyu Mama yupo vizuri hakika.
 
Raisi fulani aliyepita angepata wazo la kuwafungia wapinzani wa siasa wote humu ndani awapeleke Kisiwa cha Wagagagigikoko na nafasi bado ikabaki !

 
Bado sana, Meli kubwa ya container 5000 ndio ilifika mpaka ikaonyeshwa AZAM TV meli kubwa ya mizigo kutia nanga bandari ya Dsm. .



Huko Duniani kuna meli zinabeba container zaidi ya 20,000 kwa mara moja
Ku
Bado sana, Meli kubwa ya container 5000 ndio ilifika mpaka ikaonyeshwa AZAM TV meli kubwa ya mizigo kutia nanga bandari ya Dsm. .



Huko Duniani kuna meli zinabeba container zaidi ya 20,000 kwa mara moja
Kuna watu mkuu inabidi ujishushe ili uendane na akili zao.
 

Kwa hiyo ni uongo tunaambiwa hii meli haijaja Tanzania moja kwa moja toka Japan, kumbe imepitia Mombasa kwanza.

Kwa nini viongozi wanasema uongo siku zote?
 
Kwa hiyo kwa miezi 6 ya kubadili uongozi matokeo yake ndio haya.
 
hii inasaidia nini watanzania? au sifa za kijinga tuu maaammae.
 
Watetezi wa bandari ya Bagamoyo waone aibu. Maana tulikuwa tunaambiwa kuwa bandari ya Dar haiwezi kushindana na bandari ya Mombasa hivyo tukitaka kushindana basi tujenge bandari ya Bagamoyo; leo wamesutwa.

Narudia hakuna haja ya bandari ya Bagamoyo.
Kwahiyo kuja kwa hiyo meli ndo inaonesha Bandari ya Dar ina uwezo wa kushindana na Bandari ya Mombasa, au?!!

Au kwavile umeambiwa bandari imepokea "bonge la mmeli" ndo maana umefikia kusema hayo!!!

FYI, ile meli wamesema ina urefu wa almost 200M, wakati Megaships zinafikia hadi 400M; and it's matter of time kabla hazijitengenezwa zenye urefu wa hata 500M!!

Meli kama hizo nilizotaja hapo juu haziwezi kuingia Dar Port!!

Na kama unadhani kuingia meli yenye urefu wa 200M ndo inaonesha mbavu zetu dhidi ya Mombasa, hebu soma hapa chini:-
The Panama flagged vessel has a length overall of 300 m, a breadth of 48m, height of 62 m and deadweight of 110629 tonnes and a gross tonnage of 94469.
Hiyo ndo meli ambayo ilifunga gati Mombasa way back in 2018!!

Na hapa chini, ni idadi ya meli zilizofunga gati, na zinazotarajiwa kuingia kwenye bandari hizo mbili kama inavyoripitiwa na Marine Traffic---



Sasa endeleeni kuleta mizaa kwenye mambo serious, lakini nikukumbushe tu kwamba, Firs Phase ya Lamu Port imeshakamilika!!
 
Huwa tunashangaaga sana Kenya wanapotunyoosha kwenye mapato wakati utalii hata sisi tunao tena kuwazidi. [emoji1139]Kenya watu 52m kama sijakosea bajeti TZS 78 trillions. [emoji1241]Tanzania watu 60m bajeti TZS 36 trillions [emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]. Nimecheka tu lakini sio mazuri
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi sana, nami acha niseme kidogo kuhusu masuala ya kodi!!!

Pale Bandarini kuna kodi kuu za aina tatu...

1. Import/Export Tax
2. Value Added tax (VAT),
3. Excise Duty, na
4. Income Tax.

Hizo kodi #1 hadi #3 ni MALI YA SERIKALI.

Sasa kama kodi zote 3 ni mali ya serikali, Mchina atapata nini?!

Mchina kazi yake pale ni kutoa huduma!! Atapokea meli zinazoleta na kufuata mizigo!! Hapa atalipwa Mapato (Income)!

Atakuwa na eneo la kuhifadhi mizido... hapa tena atakuwa analipwa na wenye mizigo yao

Atakuwa pia anatoa huduma ya meli kufunga gati hapo bandarini... hapa napo Mchina atakuwa analipwa na wenye meli zao!

Zipo pia shughuli/huduma nyingine atakazotoa Mchina, na atakuwa analipwa!!!

Sasa hayo mapato hapo juu kisheria anatakiwa alipie kodi niliyotaja kama #4, yaani Income Tax!!

Sasa basi, kawaida ya Mchina, na hata Investors wengine hususani kwenye BOT Projects, huwa anaomba asamehewe hiyo Income Tax!!

Sasa Mamlaka husika badala ya kuwa wakweli ni kodi ipi Mchina anaomba kusamehewa, wao wanaongea kijumla jumla tu kwamba "Mchina anataka kusamehewa kodi"!

Lakini kama ulivyosema hapo juu, faida za mradi kwa ujumla ni kubwa kuzidi hata hiyo Income Tax!!!

Watu hatuangalii ni ajira ngapi zitatolewa kupitia Bagamoyo Port na mradi pacha wake, Yaani Industrial City!!

Watu hatuangalii multiplier effect itakayotokea hapo bandarini na kwenye mradi pacha wake!!

Kwa faida ya wengine, na kwa mujibu wa Investopedia...

Yaani, ndo hivyo imefanyika investment kubwa ya bandari ya Bagamoyo... what next?

The next is: Mosi kutakuwa na ajira itakayohakikisha kipato kwa waajiriwa!!! Huyu mwajiriwa akipata mshahara wake, sehemu ya mshahara atanunua mama nitilie, atanunua maji ya kunywa, atanunua nguo, atalipa nauli, n.k!!!

Yule Mama Ntilie aliyepokea pesa ya Mfanyakazi wa Bandari, nae sehemu ya hiyo pesa ataenda gengeni kununua nyanya, vitunguu, mchele, n.k! Hao waliolipwa na Mama Ntilie nao pesa hiyo itaenda kwa wengine!!

Sasa unakuta pesa iliyowekezwa Bandarini Bagamoyo, imenyambulika kidogo kidogo hadi imemfikia Mkulima wa Nyanya aliyepo Lushoto... yaani ime-multiply!!

Kwenye Decision Making, hususani serikalini, Multiplier Effect ni jambo la msingi kuliko hata hiyo direct tax kwa sababu, unaweza kukosa kodi bandarini lakini pesa iliyotoka hapo bandarini imeenda kuboresha sekta zingine za kiuchumi zinazoweza kukuletea kodi uliyoikosa bandarini!!
 
Ishu ni idadi kubwa ya magari iliyobebwa kwenye hiyo Meli na yakashuka Dar Port.

Meli hiyo aina ukubwa wowote mita 199.9, waandishi wa habari wameikuza Sana hii taarifa mpaka DG anatokea kwenye ishu ndogo kama hii.

Mwezi uliopita Dar es Salaam Port Kuna Meli ilikuja (Ship Carrier) ilileta meli za wachina wanaotanua bandari hakuna media au waandishi walioenda kupiga picha Wala kutangaza.

Kwa Sasa vyombo vya habari vingekuwa vinaweka mambo kama meli fulani ya Container au Bulk Cargo(Mzigo wa shehena) imekuja na mzigo kiasi Fulani na umeshuka ndani ya muda mfupi (Ship turn around) habari za uzalishaji bandari Ndio mpango.
 
Hapo nilipo-bold ndo umemaliza kila kitu!!

Nishawahi kusema hapa JF mara kadhaa kwamba wakati mwingine watu tunaingia Jukwaa la Kenya na kuamua tu kujitoa ufahamu ili kuitetea nchi yetu lakini ukweli ni kwamba, jamaa wametuzidi kwenye idara nyingi sana za kiuchumi!!!

Ni kutokana na hilo, ndo maana binafsi huwa nakwepa sana mijadala ya kule Jukwaa la Kenya kwa sababu nafahamu ili kuitetea nchi yangu nitatakiwa ama niwe na-twist mada zinazotolewa na Wakenya, au niamue kujitoa ufahamu!!
 
Siku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
Kwani wanaruhusu mkuu kuingia mule ndani na kufanya utalii mi mwenyew napenda sana kuona mule ndani shughuli zinavofanywa.
 
Ukweli mchungu, jamaa wametuacha inabidi tupambane.
 
Let's hope hayo magari asilimia kubwa yawe mapya,sio used,maana itakuwa kama imekuja kufanya dumping ya mikweche iliyochoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…