The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Method Damian Kumdyanko mkazi wa Sinza Dar Es Salaam anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wenye silaha siku ya Februari 28, 2025 nje ya geti la nyumba yake Sinza Dar Es Salaam.
Akizungumza na Jambo TV Tura Chaula ambaye ni rafiki wa kike wa Method na aliyeshuhudia tukio hilo amesema siku hiyo alisikia kelele getini za kuomba msaada kutoka kwa sauti anayoifahamu(sauti ya method) na alipotoka kwenda kufungua geti alikuta watu zaidi ya sita wakiwa na silaha aina ya bastola wakimlazimisha Method kuingia kwenye gari aina ya Prado
“ilikua majira ya saa mbili usiku Method ametoka kwenye mizunguko yake na alipofika getini nilisikia vishindo na kelele za Method akitaka asaidiwe kwa kufungua mlango”
"Baada ya kutoka na kufungua mlango nilimkuta amevamiwa na kushikiliwa na watu wenye silaha wasiopungua sita ambapo walimkamata na kumfunga pingu bila kutuambia wanampeleka wapi na sababu ya kumkamata ni ipi” amesema Tura.
Soma Pia:
“hawakutujibu ili tujue kama ana kosa au anapelekwa sehemu gani na baada ya hapo walimpakia kwenye gari na kuondoka naye”
Aidha ameeleza kuwa wamefanya jitihada za kumtafuta kwenye vituo vya Polisi lakini hawakufanikiwa kumpata.

- Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
- Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha