Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hio sir name waanze kuulizia ofisi za uhamiajiMethod Damian Kumdyanko mkazi wa Sinza Dar Es Salaam anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wenye silaha siku ya Februari 28, 2025 nje ya geti la nyumba yake Sinza Dar Es Salaam.
Akizungumza na Jambo TV Tura Chaula ambaye ni rafiki wa kike wa Method na aliyeshuhudia tukio hilo amesema siku hiyo alisikia kelele getini za kuomba msaada kutoka kwa sauti anayoifahamu(sauti ya method) na alipotoka kwenda kufungua geti alikuta watu zaidi ya sita wakiwa na silaha aina ya bastola wakimlazimisha Method kuingia kwenye gari aina ya Prado
“ilikua majira ya saa mbili usiku Method ametoka kwenye mizunguko yake na alipofika getini nilisikia vishindo na kelele za Method akitaka asaidiwe kwa kufungua mlango”
"Baada ya kutoka na kufungua mlango nilimkuta amevamiwa na kushikiliwa na watu wenye silaha wasiopungua sita ambapo walimkamata na kumfunga pingu bila kutuambia wanampeleka wapi na sababu ya kumkamata ni ipi” amesema Tura.
Soma Pia:
Tura ameongeza kuwa wahusika hawakuwa wakizungumza bali walimuingiza kwenye gari hilo jeupe aina ya prado na kupotea kusipojulikana.
- Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”
- Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
“hawakutujibu ili tujue kama ana kosa au anapelekwa sehemu gani na baada ya hapo walimpakia kwenye gari na kuondoka naye”
Aidha ameeleza kuwa wamefanya jitihada za kumtafuta kwenye vituo vya Polisi lakini hawakufanikiwa kumpata.
View attachment 3256233
Nimesoma sehemu huyu jamaa ni mserikaliAlikuwa anajihusisha na harakati gani za kuikera serikali
Humu nchini kuna kiongozi wa Dini, Dini gani wakati viongozi wote wapo kwenye Payrol.Haya mambo mbona kipindi hichi cha Samia yamekuwa mengi na yeye amekaa kimya? Viongozi wa dini wako kimya na huku raia wanatekwa na kuuawa!
Htr sana kwakweliMwamba ndiyo kaenda hivyo, na kwakuwa hakuna hata video ya wahusika ndiyo ganda la ndizi kabisa.