Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Habari hii kwenye gazeti la leo la Mtanzania limeandika habari ambayo imenifikirisha sana. Hebu na nyie wadau mtafakari haya maneno halafu muone yana maana gani.

Mtanzania limendika;-

...........hata baada ya Kamanda Mambosasa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudai kuwa waliotekeleza tukio hilo ni wazungu, hoja ambayo imezua maswali namna walivyofahamu uraia wao mara moja, licha ya watu hao kudaiwa kuvalia kininja.....
 
Kazi ya ulinzi na usalama ni ya kila mwananchi na kila mzalendo si ya majeshi pekee.Kila mwananchi asaidie kupatikana kwake.Kuliachia jeshi la polisi pekee ni ufinyu wako wa akili mleta mada
Jeshi la polisi si wamesema ni jambo la kawaida na watu waendelee na shghuli za kulijenga Taifa? Lugola mwenyewe badala ya kutuhakikishia kuwa uchunguzi wa kumpata mtekwaji unaendelea kwa kasi na kuomba huo ushirikiano, hakusema hivyo wala kuomba ushirikiano wa wananchi.Sanasana alisema kuna amani, na akukumbushia kuwa jiwe ndo rais(sijui kutekwa kuna uhusiano gani na yeye kutokuwa ama kuwa rais?), unless kuna yaliyomo nyuma ya pazia tusiyoyajua(ambapo mimi ninaamini hivyo)Pia alisema hakuna uhalifu zaidi ya wivu wa mapenzi ambao polisi ndo wanafuatilia. Khaa! kaazi!
 
Mpuuzi kweli wewe, kesho Tena utageuka utasema ni kazi ya Polisi wasiingiliwe.
Mtu akipotea mitaani pamoja na kuripoti polisi spika misikitini hutangaza kuwa yeyote atakayemwona apeleke taarifa kituo cha polisi au msikitini nk Kupotea mtu si kitu cha kuachia polisi tu
 
Kwani mtu akivaa mask mikono aiyonrkani kuona rangi ya ngozi, kingine ni saokolojia ndogo tu kwamba endapo weupe wamkono angekuwa nao mmoja ingekuwa ni wa Africa ila kuwaona wote na rangi nyrupe inamaana ni wazungu uwenda hata wakawa albino ila aiwezi albino kuongozana kwa infruence hipi asa.

Hitimisho
Mask aizibi mwili wote hivyo kuonekana wote wana rangi nyeupe lwa baadhi ya viungo vilivyoonekana inatosha kusema ni wazungu.

Nime tupe fasta naogopa kuibiwa simu kizani.
 
Maoni yangu: Linahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na pengine hata vyombo vya ulinzi vya kimataifa.
Na ushirikiano kutoka kwa wananchi itategemea na jeshi letu lina behave vipi kwa wananchi!
 
Kama rahisi fanya wewe mkuu
 
Maoni yangu: Linahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na pengine hata vyombo vya ulinzi vya kimataifa.
Na ushirikiano kutoka kwa wananchi itategemea na jeshi letu lina behave vipi kwa wananchi!
Ungerahisisha tu kuwa hawana uwezo huo peke yao.
 
Kwani muhindi sio mtu? Hata wewe si ni kabila fulani tu?
 
Kuna uhusiano gani kati ya ulichoandika na mada iliyopo mezani????
 
Mamlaka iliyomteua mkuu wa mkoa wa Dar ilifanya hivyo kwa kuzingatia vigezo vyote na kwa heshima ya mwenye kuteua. Nafikiri ni wakati muafaka wa kulinda vigezo na heshima ya mwenye mamlaka ya kuteua na taasisi yake
 
Hii ni kwasababu huyu ni tajiri mkubwa lakini mwezi huu Pekee waliopotea sio chini ya 50
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…