Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

hivii ni nani vilee alituambia kuwa ''wakishatumaliza upande huu watarukia upande wenu... jiandaeni tu kisaikolojia
 
Upo gizani, pole sana, hata umaskini wako umetengezwa makusudi na watu ili wakutawale, Mungu hakutuumba maskini.

Wanasiasa wanaunda tatizo na kulitatuwa ili wajinga kama wewe muweze kuwasifia.

Makonda aondolewe haraka kwenye hiyo nafadi ya RC na ahojiwe na Polisi kwa jinai anazohusika nazo.
Bahati mbaya mimi sio maskini Kaka
 
Dah tunaletewa movie nyingine
.sijui itakuwa na part 2?
.sijui itachezwa kwa ustadi au itafanana na zile nyingine?
.sijui inataka kumpa kiki nani ?

Wakati utasema...stay tuned....!!!!
bila shaka umejionea muvi nzima mkuuu 😕😕
 
.
 
Attachments

  • MV5BMjA3NTA1MjgwNV5BMl5BanBnXkFtZTcwMTgyMDExNA@@._V1_SX1472_CR0,0,1472,999_AL_.jpg
    MV5BMjA3NTA1MjgwNV5BMl5BanBnXkFtZTcwMTgyMDExNA@@._V1_SX1472_CR0,0,1472,999_AL_.jpg
    164.7 KB · Views: 39
Nimeawaambia hawa wazungu ni wazungu koko aiseehhh yani hata wabongo wamewazidi maana wanagekua ni wabongo tungesikia siku nne MO ndiyo anapatikana,cha kwanza watuambie dhamira ya hao kumteka Mo
Hawakuwa wazungu hao watakuwa ni Alibino wa Le mutuz kuna kamchezo kanatengenezwa ili kuwasahaulisha watanzania juu ya machungu ya matumizi mabaya ya pesa za umma pesa za walipa kodi.
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

Jambo la kushukuru kwa Mungu kuna tetesi kwamba tajiri Dewji AMEPATIKANA !
Tukio hili liwe funzo hasa kwa matajiri.
 
Sasa jamani hao wazungu ealiokuwa wamemteka, washahojiwa kujulikana ni raia wa nchi gani na nia yao ni nini?
 
Back
Top Bottom