Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Ukinunua mali ya wezi iko siku watakugeuka tu maana dhuluma ndio riziki yao.
 
Wakuu, watekaji hawajasema lolote hadi saivi?Hawahitaji lolote in exchange of Mo?
 
Hata yule demu wa Babu seya inadaiwa sio mtz
 
Ina maana huyu hakuwa na walinzi binafsi? Mbona wasanii kama Diamond huwa wanakuwa na walinzi??
Nadhani ni muda muafaka sasa kwa Mtu yeyote maarufu na mwenye uwezo mkubwa wa kifedha kuajiri walinzi wake binafsi. Tusijidanganye kwamba tuna Amani kiasi hicho!!
 
Kutumia neno wazungu INA upungufu, inaposemwa walijifunika nyuso. Vinginevyo pawe na uthibitisho. Si kila mweupe ni mzungu, kuna wahindi, warabu nk.
 
Sio kila taarifa usalama wa taifa wanaweza kuipata.

Mfano wewe unajua mimi nina mipango gani katika maisha yangu?
Usalama wa taifa sio wahitimu wa MEMKWA.. .. Usalama ndio kitu kikubwa kimewaweka hapo wanalamba pesa ndefu.
kuhusu wewe kuwaza nini Wapo watu wa kaz hiyo sio blaa blaa
 
Tuendelee kuwa watulivu wakati vyombo husika vikiendelea
na zoezi la kumtafuta ''MO''
Ninachoshukuru ni kuona jinsi watanzania tunavyoendelea
kuwa wakomavu katika mambo haya maana sijaiona lugha
ya kusema ''kajiteka'' na hii ni faraja kubwa kwa taifa.

Kuna haja ya watu maarufu,kuwekewa
vifaa maalum mwilini kwa ajili
ya kufuatiliwa mahali alipo,ila iwe siri yake
na familia yake,hili lingesaidia kipindi kama hiki
kurahisisha upatikanaji wa mhusika.

Lakini pia ni wakati muafaka
kwa watu maarufu kuwa na walinzi
binafsi wanaowasindikiza katika
kutimiza majukumu yao,maana tunayoyaona
kwenye sinema watu maarufu wanatekwa
ili watekaji wapewe pesa nyingi yanaweza
kufika hata huku kwetu.
 
Usalama wa taifa sio wahitimu wa MEMKWA.. .. Usalama ndio kitu kikubwa kimewaweka hapo wanalamba pesa ndefu.
kuhusu wewe kuwaza nini Wapo watu wa kaz hiyo sio blaa blaa
Usidhani usalama wa Taifa ni Miungu ni watu kama wewe hawawezi kuwa na taarifa zote kuhusu kinachotaka kufanyika.

Nimepanga kutekeleza mauaji au uvamizi sehemu fulani nikiwa mwenyewe nani atawaambia wanausalama habari hizo?

Usidhani wanausalama wananusa kila sehemu pia kaa ukijua kuwa yanapotaka kufanyika mambo ya kihalifu lazima wanaofanya uhalifu huo wajipange maana wanajua kuwa muda wowote wanaweza kuwa hatarini. (Kujipanga kwao ndiko hufanya iwe ngumu wao kupatikana)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…