Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Hili si tukio dogo. Ni vyema serikali ikalibeba kwa uangalifu mzito.

Ni Tukio ambalo linaweza kuathiri vibaya zaidi hali ya uchumi wa nchi kama halitashuhulikiwa kimakini!!! INVESTORS ARE WARY OF SECURITY ISSUES!!.
 
Mungu aitie nguvu familia yake kwenye huu wakati mgumu na tumuombee uzima huko aliko atoke salama.
 
Kwa mujibu wa derva hakukuwa na ubishani ktk huu utekaji. Mtekwaji alitii amri lakini watekaji wakapiga bunduki juu. Kama ndivyo ilivyokuwa basi hawa watekaji walitaka ijulikane kuwa huyu mtu katekwa. Swali, kama wangekuwa watu wa kudai ransom wangetaka tukio liwe kimya kimya tena wangefanya wakati anashuka au anapanda garini lakini kwenda kumchomoa ndani nu hakika walitaka ku exaggerate the kidnapping. Ngoja tusubiri report ila kwa mazingira yalivyo lengo la watekaji kujulikana kwa haraka na ngumu
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

Ngoja nikae kimya ili sinionekane mfuata upepo fulani hivi.

Polisi fanyeni kazi yenu ya kulinda raia pamoja na mali yake.

Mungu aingilie kati ili MoDewji apatikane akiwa salama salimini.

USHAURI
Kama unajua kuwa una mali plse jaribu kuwa na ulinzi binafsi.

ASANTE
 
Akipita kwa hili aanze kuishi kwa tahadhari, awe na ulinzi 24hrs, aache kujiamini kupita kiasi, Dunia ina mengi hii.
Hata maadui anao...wafanyabiashara huwa na mambo mengi sana
 
Ngoja nikae kimya ili sinionekane mfuata upepo fulani hivi.

Polisi fanyeni kazi yenu ya kulinda raia pamoja na mali yake.

Mungu aingilie kati ili MoDewji apatikane akiwa salama salimini.

USHAURI
Kama unajua kuwa una mali plse jaribu kuwa na ulinzi binafsi.

ASANTE
Japo wengi wanaamini ata walinzi binafsi mda mwingine wana matatizo yao
 
Whoever works this case must:
1.be knowing the motive of the kidnappers right now!
2.know what Mo owns -his balance sheet. And where everything is,keep track of that.
3.Know the closest people to Mo who can effect a transaction and keep track of them.
4.Make sure Mo is safe by following what the kidnappers while working a plan to get him back.

We may need heros of action in this but leadership of calm heads and am not sure we have any!
 
Kuna mtu alisema ,wakimaliza wapinzani na wanaokosoa serikali wataanzana wenyewe sasa wameanzana msishangae .Wale wengine waliotekwa na kupotea walikuwa watoto wa simba na sio wa wamama wa wenzenu.Mtoto ni mtoto tu mradi katoka kwa mwanamke kwa mwenzio ana dhamani kubwa hata akiwa kibaka.Ila Pole sana familia ya MO nimesikitika sana na kutekwa kwake ,namwombea Mungu akutwe akiwa salama.Mungu tusaidie.
 
Back
Top Bottom