Hii hali tumeilete na kuilea wenyewe Watanzania,nasena hivyo kwa sababu utekaji haukuanza leo na kwa watu wa kaliba ya MO,wanasiasa na "wasiokuwa upande wao" wamehujumiwa sana,wengine wameuawa wengine wamepotezwa lakini hatua hazikuchukuliwa,sasa imefika kwa "mwenzao" wameshtuka,wamesahau kuwa walichopanda sasa kinazaa,watoto wetu wangapi siku za hivi karibuni wamepotea, hakuna anayeonesha kujali hasa,nasikitika kwa hili kumtokea MO,ila naweza kusema ni ishara kuwa Mungu anatuamsha na kutukumbusha kuwa haya siyo maisha,sasa hatua zitachukuliwa kuutokomeza huu uhalifu tuliouasisi na kujiona tuko salama hautatugusa,Mungu twaomba MO huko wanakomshikilia wamuachie bila kumdhuru na bila sharti lolote,kwa jina la Yesu Kristo