Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Mkuu, Ishu hapo ni MASLAHI. Utatafutwa kwa bidii kiasi gani kuendana na wanaokutafuta wana maslahi kiasi gani na wewe.

Unaweza kuwa Tajiri mkubwa au mtu Maarufu lakini uhusiano wako na wanaokuzunguka ni mbovu au wivu ama wanakuchukia tuu kwa sababu wanazojua wao. Hapo ukipotea watu watasema bora tuu apotee, wataendelea tuu na shughuli zao kama vile hakuna kilichotokea. Pamoja na mapesa uliyonayo, no one will give a sht about yr disappearance!
Usemayo ni kweli lakini tuna-assume kwamba Mo hakuwa na matatizo makubwa na utawala wa Magu. Tuna-assume huyu ni tofauti sana na yule wa Jangwani mbele ya macho ya watawala! Hata kama kuna tetesi za hapa na pale kuhusu ugomvi wa kimaslahi kati yake na serikali lakini bado ugomvi huo haujawahi kuwa wazi sana!

Kutokana na hilo, hapa tunamchukulia Mo kwa hadhi ya kuwa tajiri mkubwa kabisa nchini! Kwani angekuwa ni yule "Mtukutu" wa Jangwani watu wangeshangaa sana! Hivi sasa tayari pangekuwa na rundo la theories zinazoweza kuwa chanzo cha kutekwa kwake!
 
Labda sijui lakini factor kubwa ni hela ya kuendesha huo ujambazi ndio huwa ishu kubwa. speedboat huwa ni ghali mno ilihali majambazi huwa hela zao ni za kuunga unga kabla ya kufanya tukio, ndio maana utaona huwa labda wana milioni mbili ambayo huitumia kupata Smg/Ak-47 then kuhusu magari huwa wanayateka ndio wakafanyie ujambazi. Majambazi kutumia speedboat aisee sijawahi kusikia matukio ya dizaini hii hapa nchini kwetu
Hii ndio shida tulionayo. Kamwe hata siku moja usimu-underestimate mtu kisa hujawahi kusikia kafanya kitu flani cha ajabu. Na hata katika ngazi ya kijeshi ni makosa makubwa sana kumdharau adui kwamba hawezi fanya kitu flani amazing au hawezi miliki chombo flani cha kivita.
 
Tuache wivu.....wanahaki ya kufunga....
Mo..ni kama balozi asie rasmi wa Tz, hasa ktk masuala ya kibiashara na uwekezaji. Kupitia watu kama akina Mo...wawekezaji wanaweza kuwa na imani na nchi yetu na pia umashuhuri wake ni kama nafasi ya sisi kujitangaza..
Mtu anatajwa na magezeti kama forbes kama the youngest billonaire Africa etc..tena wanasema kabisa anatoka Tanzania huoni kama ni fahari kwa taifa..
Zaidi ya hayo jamaa kaajiri watu zaidi ya 20,000 manake kuna watu kama 100,000 wanaishi sababu yake..hivyo si mtu mdogo..ni mtu muhimu sana kwetu..
Waafrika tuachane na ego na wivu

“Fahari kwa Tanzania... nafasi ya kujitangaza... wawekezaji wanakuwa na imani...”

NONSENSE ON STILTS !

mmefunga wafanyabiashara jela bila mashitaka

mmepitisha sheria za madini zilizofuta sanctity of contracts (serikali inaweza kufuta mkataba unilaterally, with impunity)

Rais wenu kila wiki anachanwa THE ECONOMIST kwamba he is irrational and despotic, amekuwa kikatuni cha dunia

takwimu zimepigwa marufuku

wapinzani wanapigwa risasi mchana mnafunga uchunguzi asubuhi yake

USAID na international nonprofits wamepigwa stop kwa sababu hawakubaliani na whims za Rais za wasichana wafukuzwe mashuleni, raia tukazaliane kama panya, mikopo ya elimu ni kwa graduates wa sekondari zako za kata tu...

mkiulizwa inakuaje mnasema Tanzania is a sovereign state

LEO MNAJALI HESHIMA NA IMANI YA JUMUIYA YA MATAIFA KWA KUFUNGA AIRPORT KISA BILIONEA KATEKWA? UNAFIKI MKUBWA

Mmewekwa mfukoni na matajiri!

Julius Nyerere is rolling in the grave, he would never shut down the borders because a rich citizen has been kidnaped when these vices occur everyday on students, journalists, politicians, critics and researchers ( Ben Saanane.)
 
Kangi Lugola anachanga karata zake kwa uangalifu mkubwa; kwanza hana uhakika kama hill tukio ni utekaji au ni maigizo. Kwa ufupi tukio lenyewe linachanganya kwani "motive" au sababu ya tukio haijajulikana.
 
Yule mfanyabiashara kule Tarime yeye aliwapiga Risasi bila msaada wa bodyguard iweje yeye ashindwe kujihami?
Harafu walifikili yeye ni fala walichukua ya kiunoni (mkanda) wakasahau ya kwenye soski
 
Nitajie nchi moja tu, yoyote ile ambayo tajiri wake mkubwa kuliko wote aliwahi kutekwa na saa 24 kupita bila vyombo vya dola kuwa na clue!

Kwamba, eti "haijalishi huyo mtu ni maarufu au kama mimi" hiyo ni kujaribu ku-justify uozo uliopo kwenye mfumo wetu wa ulinzi na usalama! Endelea kujidanganya kwamba akina eti sie tupo sawa tu na akina Reginald Mengi na kwamba, utekwaji wa yeyote miongoni mwetu hiyo ni ishara mbaya! Ni kweli, ni ishara mbaya lakini anapotekwa mtu kama Mo Dewji, hiyo sio tu ni ishara mbata bali ni ishara mbaya zaidi na zaidi!

Sie wengine miaka kadhaa iliyopita tulishuhudia Mzee Reginald Mengi akipewa ulinzi wa polisi nyumbani kwake Oysterbay baada ya kutishiwa kuuawa! Kama unaamini wewe na Mzee Mengi ni sawa, basi nenda kwenye kituo cha karibu ukaripoti kwamba unatishiwa kifo na kisha wathibitishe kwamba kweli unatishiwa kifo halafu uone kama unapewa askari polisi wa kuja kukulinda hapo unapoishi!!!

Mtu kama mimi, nitaenda viwanja gani kama sio Tandale, Mwananyamala, Manzese, Temeke n.k! Huko haitashangaza nikitekwa kwa sababu mfumo wetu wa ulinzi haujafika kisawasawa hadi Uswahilini!!! Lakini inapotokea mtu anatekwa maeneo kama ya Colleseum na kupita 24 hours bila vyombo vya dola kuwa na clue, hapo akina sie hatutaacha kujiuliza ikiwa maeneo kama yale na mtu kama yule anaweza kutekwa na watekaji kutokomea kusikojulikana! Maeneo ambayo angalau yana mifumo mizuri ya mitaa ambayo ingewezesha kuwa na street cams; vipi akina sie tunaoishi Kwa Mtogole! Huku kwetu watu si wanaweza kuingia hadi na vifaru na wasionekane!!

Ikiwa maeneo kama yake hayana hata Patrol inayoweza ku-respond kwa haraka anapotekwa mtu kama Mo Dewji, vipi huku kwetu?Ikiwa Richest Person anaweza kutekwa na polisi wasiwe na clue hata baada ya saa 24 kupita huku tukifahamu wamewekeza nguvu zao zote katika kufanya msako! Vipi ninapotekwa mtu kama mimi ambae polisi haitaweza kutoa japo askari mmoja kutafuta nipo wapi!!!

Kwa wale wanaoamini katika siku ya huku, mimi na Mo Dewji ni sawa lakini ni sawa mbele ya mwenye kiti cha enzi lakini hatuna usawa wowote mbele ya viti vya akina Magu!!

No wonder tunapotekwa akina sie wala hakuna anayejishughulisha! Endelea kuhangaika ku-justify ujinga!
Kabla ya kuzungumza fanya uchunguzi kwanza mkuu...

Kwa taarifa yako kama unamfahamu bilionea Jakob Juma wa kenya alitekwa na kuuawa mwaka 2016.

Marekani na ulaya matukio kama haya nanatokea sana. Hebu fuatilia matukio ya kutekwa hawa matajiri

BOBBY GREENLEASE
VIRGINIA PIPER
JOHN PAUL GETTY III
ALDO MORO na wengine wengi.

Halafu hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutetea uhalifu...mimi sivai gwanda wala nguo za kijani mkuu.
Mimi ni mtanzania mzalendo nayefikiria kabla ya kuongea nmsilishwi na mtu najilisha.

Sasa unaoolaumu vyombo vya usalama kwa uzembe una maana gani? Unakumbuka tukio la westgate attack?

Mamia ya watu waliuawa na watu kama watatu hivi...serikali ilituma polisi, wanajeshi, mpaka makomandooo lakini hawakukamata hata mhusika mmoja.

Kama hujui ni vizuri ukanyamaza kimya kuliko kuleta hisia zako kwenye mambo ya uhalisia.

Mfanyabiashara mkubwa kama Mo kutekwa sio jambo la kitoto. K7na mengi tusiyojajua its better kuwa kimyaaa. Achia vyombo vya usalama kazi yao.

Kikumbwa ni kumuombea huko aliko atoke salama.

ASANTE
 
“Fahari kwa Tanzania... nafasi ya kujitangaza... wawekezaji wanakuwa na imani...”

NONSENSE ON STILTS !

mmefunga wafanyabiashara jela bila mashitaka

mmepitisha sheria za madini zilizofuta sanctity of contracts (serikali inaweza kufuta mkataba unilaterlly, with impunity)

Rais wenu kila wiki anachanwa THE ECONOMIST kwamba he is irrational and despotic, amekuwa kikatuni cha dunia

takwimu zimepigwa marufuku

wapinzani wanapigwa risasi mchana mnafunga uchunguzi asubuhi yake

USAID na international nonprofits wamepigwa stop kwa sababu hawakubaliani na whims za Rais za wasichana wafukuzwe mashuleni, raia tukazaliane kama panya, mikopo ya elimu ni kwa graduates wa sekondari zako za kata tu...

mkiulizwa inakuaje mnasema Tanzania is a sovereign state

LEO MNAJALI HESHIMA NA IMANI YA JUMUIYA YA MATAIFA KWA KUFUNGA AIRPORT KISA BILIONEA KATEKWA?

Mmewekwa mfukoni na matajiri nyinyi, wanafiki wakubwa!

Julius Nyerere is rolling in the grave, he would never shut down the borders because a rich citizen has been kidnaped when these vices occur everyday on students, journalists, politicians, critics and researchers ( Ben Saanane.)
Naona una hasira sana...pasuka basi...
 
Mohammed Dewji: Wasifu wa Mo Dewji bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika anayetoka Tanzania

Mohammed Dewji, maarufu kama Mo Dewji, ni mmoja wa wafanyabiashara wanaofahamika sana kutoka nchini Tanzania.
Ni bilionea ambaye ametambuliwa kuwa miongoni mwa mabilionea wa umri mdogo zaidi Afrika.
Ni mfanyabiashara na mwanasiasa ambaye pia amewekeza katika kandanda na pia katika shughuli za hisani. Ni mnyenyekevu na huwa mara nyingi haandamani na walinzi kama ilivyo kwa wau mashuhuri.
Alipokuwa anatwekwa eneo la Oyster Bay alikuwa anajiendeshea gari mwenyewe.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aligusia hilo akizungumzia hali ya usalama Dar es Salaam: "Na ndio maana hata Mo mwenyewe angeweza kuwa na mabodyguard (walinzi) lakini kwa sababu ya amani iliyoko katika mkoa wetu, anatembea peke yake."
Mo Dewji ni nani?
Mo alizaliwa tarehe 8 Mei mwaka 1975, ikiwa na maana kwamba kwa sasa ana miaka 43.
Alizaliwa eneo la Ipembe, Singida maeneo ya katikati mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes, ana utajiri wa dola bilioni 1.5.
Vijana wa Afrika mashariki wanaotarajiwa kuwa mabilionea
Ni wa pili miongoni mwa watoto sita wa Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji.
Alisomea elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Arusha na baadaye akasomea elimu ya sekondari katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.
Alihamishiwa Marekani kwa masomo zaidi ya sekondari katika jimbo la Florida mwaka 1992.
Alisomea chuo kikuu cha Gerogetown jijini Washington DC na kuhitimu mwaka 1998 akiwa na shahada ya kwanza katika biashara ya kimataifa na fedha, na masuala pia ya dini. Miongoni mwa watu mashuhuri waliosomea chuo kikuu hicho ni rais Bill Clinton, rais wa zamani wa Ufilipino Gloria Arroyo, Mfalme wa Jordan Abdullah na wachezaji wa NBA kama vile Allen Iverson na Patrick Ewing.
Baada ya kufuzu, alirejea Tanzania na kuanza kushiriki katika usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.

Fedha

Alihudumu kwa miaka miwili kabla ya kuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, wadhifa ambao ameendelea kuushikilia hadi sasa.
Mo ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia miongoni mwa matajiri wa umri mdogo zaidi Afrika.
Kampuni ya METL, kwa mujibu wa Forbes, ilifanikiwa kwa kununua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti.
Tajiri mkubwa Afrika Mashariki Mo Dewji atekwa

METL ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.
Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.
Kwa mujibu wa tovuti yake, METL inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.
Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
METL ina shughuli zake katika nyingi barani Afrika na ina malengo ya kujipanua zaidi katika maeneo zaidi.
Inaendesha shughuli zake Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji na Zambia, ambapo huajiri watu zaidi ya 28,000.

Shughuli za MeTL huchagia 3.5% ya jumla ya pato la taifa (GDP) la Tanzania.
Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2014 kutoka $30 milioni hadi $1.3 bilioni kilikuwa ni 200%.
Lengo la kampuni hiyo ni kuongeza mapato ya taifa lake hadi $5bn kufikia mwaka 2020, pamoja na kuwaajiri watu 100,000.
Mo Dewji ameorodheshwa wa 17 kwenye orodha ya mabilionea barani Afrika na wa 1561 duniani kwenye orodha ya mabilionea mwaka 2018.
Wakati mmoja kampuni yake ilianzisha Mo Cola kushindana na Coca Cola.

Wakfu wa hisani

Dewji ni Mtanzania pekee aliyesaini mkataba mwaka 2016 wa kutoa kwa wahitaji nusu ya mali yake.
Mo Dewji Foundation ndio asasi ambayo aliianzisha mwaka 2014 ili kutekeleza nia yake hiyo na kazi yake kubwa ni kusaidia watanzania wasiojiweza kwa upande wa afya, elimu na maendeleo jamii.

Kujiingiza katika siasa

Mbali na biashara na shughuli za jamii Mo Dewji amewahi kuwa mwanasiasa na mwaka 2005 mpaka 2015, Mohamed Dewji alikuwa mbunge wa Singida Mjini.
Alijiingiza katika siasa mara ya kwanza mwaka 2000 ambapo alishinda uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo, wakati huo akiwa na miaka 25, lakini akazuiwa kuwania kwa madai kwamba alikuwa bado mdogo wa umri.
Alistaafu kutoka kwenye siasa baada ya kuhudumu mihula miwili.
Mzozo waibuka kuhusu udhamini wa klabu ya Simba Tanzania

TuzoTuzo

Mwaka 2012, alitawazwa Kiongozi Mdogo Duniani kwa Kiingereza Young Global Leader (YGL) wakati wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa uchumi Duniani (WEF).
Mwaka 2015, alitajwa kuwa bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika na jarida la Forbes na baadaye akatawazwa Mtu Mashuhuri wa Mwaka wa Forbes.
Mwaka uliopita, alishinda tuzo ya Afisa Mkuu Mtendaji bora wa Mwaka Afrika katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu watendaji wa Afrika.
Familia: Mke wake na watoto
Mke wa Dewji huitwa Saira, aliyekuwa wanapendana tangu utotoni, na wamejaliwa watoto watatu Nyla, Abbas na Mahdi. Alifunga ndoa mwaka 2001. Mo na mke wake walikutana Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Simba FC

Dewji pia ni mpenzi wa michezo na amewekeza katika klabu ya mpira ya Simba inayocheza katika Ligi Kuu ya Tanzania ambapo ni mfadhili mkuu kwa sasa.
Amekuwa akifadhili ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Sababu ya kurejea Tanzania kutoka Marekani

Mo Dewji alisomea Marekani na mpango wake ulikuwa kusalia na kufanya kazi huko.
Ilikuwaje mwishowe akajipata Tanzania?
Mwezi Septemba, aliandika kwenye Instagram sababu iliyomfanya kurejea, ambapo anasema ni ushauri wa babake pamoja na kugundua kwamba kulikuwa na fursa nyingi Tanzania.

Ujumbe aliouandika 10 Septemba, 2018 ndio huu:

"Nilipomaliza masomo yangu ya shahada nikiwa nchini Marekani niliamua kubaki huko na kufanya kazi. Nilitumia muda na nguvu nyingi kazini lakini pesa ambayo niliipata haikukidhi kufanikisha malengo yangu.
"Ndipo Baba yangu akanishauri nirejee nyumbani Tanzania na nilipofatilia kwa kipindi hicho niligundua kwamba Tanzania kuna fursa nyingi za kibiashara na hapo ndipo nilipoamua kurudi na kujiunga katika biashara ya familia.
Muhimu kufahamu ni kwamba mafanikio sio lazima uende kuyatafuta nje ya nchi, hapa hapa nchini kwetu kuna fursa ambazo ukifanyia kazi utafanikiwa. Unafikiri kwanini baadhi ya watu wanapenda kuishi/kufanya kazi nje ya nchi?"

Nukuu muhimu za Mo Dewji

Mara kwa mara, hutoa ushauri, na pia huwa hafichi upendo wake kwa klabu ya Simba FC ambayo ndiye mdhamini wake mkuu.
Ijumaa wiki iliyopita, aliandika: "Kila jambo unaloogopa, Mungu ana mpango wake. Mungu ni mkuu kuliko hofu uliyonayo. Ana mamlaka na maisha yako ya baadae. Kuwa na imani."
Kuhusu urafiki na mikopo, kauli yake hii: "Hamna kitu kinaua urafiki kama mikopo!"
Kuhusu utajiri na umaskini, aliweka nukuu hii aliyoitoa kwingine pengine kwenye Twitter majuzi: "Walio fukara hujaribiwa kwa umaskini, sisi nao hujaribiwa kwa kupewa zaidi ya tunavyovihitaji."
Ana ushauri pia kuhusu kufanikiwa maishani: "Vitu vingi katika maisha vinaweza kujaribu kukuondoa kwenye malengo yako lakini usipoteze mwelekeo. Mipango inaweza kubadilika lakini kamwe sio mwisho wa safari!"
Kuhusu kuwezeshwa kwa wanawake: "Kwenye Uislamu, mwanamke hahitaji kuwezeshwa na mwanaume, wameshawezeshwa na Mungu."
Kuhusu kuwa mfano bora kwa watoto: "Mtoto wako atafata mifano yako, sio ushauri wako. Hata tunapofikiri hawatuoni, wanatuona. Hata tunapofikiri hatulei, tunalea."
FB_IMG_15392701506484901.jpg
 
kwa mfululizo huu Mzee Mingi a take care,maana walianza na boss wa YANGA akapata taabu sanaa,sasa wamehamia kwa boss wa SIMBA na atapata tabu sanaa
 
Hivi jana mbona walituyumbisha kama dish mara kapatikana mara nakanusha ni uzushi leo wasicheza na hisia zetu wakija kutoa taarifa zikamiliki,kwanza wamemchagua nani kutoa tamko maana mo lazima apatikane leo
 
Back
Top Bottom