Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Tanzania ya viwander mkuu
Mtukufu hajasema kitu, makamu wake hajasema kitu hata PM hajasema kitu ngoja nirudi kolomoje nikachunge mbuzi mjini ni hatarii kuliko mbugani
 
Sifikiri kama inshu ya Mo itakuwa kama ya Ben wa saanane, mie naona Mo kajiteka kama Abdul nondo, kwani dogo abdul ilichukua muda gani mpaka kuonekana?
 
Aliyesema waTz tuna ubongo wa kuku au Samaki hakukosea kabisa. Tunasahau haraka sana.
Sijui kwanini?
 
Sifikiri kama inshu ya Mo itakuwa kama ya Ben wa saanane, mie naona Mo kajiteka kama Abdul nondo, kwani dogo abdul ilichukua muda gani mpaka kuonekana?
Wakubwa wanajua kinachoendeleaa...! Uhujumu wa mwendokasi naona ushasahaulikaaa.... Tanzania nchi ya wajingaa aisee tunachezewa balaaa
 
Ndugu watanzania kama kawaida yetu wazee Wa matukio

Alianza Ben siku ya kwanza ya pili yavtatu ya nne tukamsahau mpaka Leo mwaka Wa pili unaelekea kuisha Ben hajulikani halipo na tumesahau kabisa

Akafuata Azory siku ya kwanza ya pili ya tatu ya NNE ya tano mpaka Leo azory tumemsahau na maisha yanaendelea

Sasa amefuata bilionea MO siku ya kwanza tukaongea siku ya pili tukaongea siku ya tatu tukaanza kusahau
Siku ya NNE nayo imepita

Kimasihara masihara hivihivi tumeanza kusahau na maisha yameanza kusonga kama kawa

Bado najiuliza Leo siku ya NNE hajapatikana na watanzania wameshaanza kusahau sasa hivi huyu atapatikana kweli au ndio Yale Yale ya akina Ben? Ngoja niishie hapa

TIME WILL TELL
Haya mambo eti yameshaanza kuwa kawaida. Hii ni hatari kwa ustawi wa taifa letu
 
Ndo ishatoka hivo yanii

Profesa Jay anakuambia

"Mtangoja milele na mtakufa bila kelele kama walivyokufa wafuasi wa kibwetere"
 
Turning point ishindwe kua kwa yule Mkurya Tajiri Zakaria ije kua kwa huyu muhindi?

Kwa yule mkurya tena Adam Malima kasema watekaji walikua ni usalama wa Taifa na hakuna turning sembuse kwa huyu
Kuna tofauti kati ya hao akina Zakaria na Malima na Mo.

Kwanza mimi hao ndio leo nawasikia kwako. Na Mo sio mhindi ni Mtanzania.

Mo ana impact kubwa sana kwemye jamii ya Tanzania, East Africa na Africa kiujumla. Msitarajie International Community in pull blind eye kwenye hili suala.

Watu watachoka kuvumilia ujinga huu. Tumechoka kabisa haya masuala.
 
Mambo mengine yanafikirisha sana! Alafu hakuna majibu.
Yani unaweza ugua kichaa kwa kuwazaa...Just imagine Kijana tajiri wa miaka 43 anapotea kiutani utani tuu yanii...!! Aisee inaumizaa Sana.. Means makampuni aliyokuwa anaendesha MO yatakufaa... sijui hao vijana ajira atawapa nani
 
Habari wana Jamvi, nahesabu usiku na akili inanijuza kuwa ni usiku wa nne sasa, hakuna #updates wala fununu kuhusu huyu jamaa. Ukweli sina ukoo na Mo lakini najikuta nafsi inaniuma sana.
Natamani kuskia miujiza ila naona matumaini yangu yanafifia na moyoni naingiwa hofu. "Hivi kweli sifa zote tunazopewa jeshi letu limeshindwa kusema japo neno la faraja hadi leo?"

Naanza kuelewa maneno ya baadhi ya watu kuwa....huenda aliyemteka anacheza miguu miwili kwenye mechi hii.......NATAMANI AREJEE AKIWA HAI NIIPATE RADHA YA MOVIE.
 
Kuna tofauti kati ya hao akina Zakaria na Malima na Mo.

Kwanza mimi hao ndio leo nawasikia kwako. Na Mo sio mhindi ni Mtanzania.

Mo ana impact kubwa sana kwemye jamii ya Tanzania, East Africa na Africa kiujumla. Msitarajie International Community in pull blind eye kwenye hili suala.

Watu watachoka kuvumilia ujinga huu. Tumechoka kabisa haya masuala.
Baba tulichoka zamani Sana...Ila ndo hatuna cha kufanyaa!!
 
Kama MO akipotea mazima basi huo ndio utakuwa mwisho wa wasiojulikana....Ndugu zake lazima wapige kisomo HEAVY ambacho kitawadondosha hao wazungu waliomteka MO.
Hata akipatikana kisomo mbona kilisomwa na bado vinasomwa. Si na ndugu tu hata wale wanaopats rizk kupitia Mo wewe acha
Guru Nanak atawaonyesha.

1539541795341.jpeg

Guru Nanak
 
Back
Top Bottom