Matumizi sahihi ya fahamu ndiko kunako muweka mwanadamu mbali na wanyama mwituni.......
Mwanadamu yoyote aliyeachana au kupoteza udhibiti wa fahamu wa zake hana tofauti na wanyama wa porini na hafai kuishi kwenye jamii za wanadamu wengine
Kamwe mwanadamu hawezi kubakia salama kwa kuachana na matumizi ya fahamu zake na kuamua kufuata matakwa ya nafsi.....sisi sote tuwadhaifu na nyakati fulani tunaanguka katika matamanio ya matakwa ya nafsi......lakini fahamu zetu zinatukataza kuyatenda hayo........
Watu wapo jela, wapo waliopata vilema, wapo watu waliolazimika kuhama miji na wapo watu walioaga Dunia kwa kuwa tu wameshindwa KUDHIBITI nafsi zao juu ya matamanio..........
Mungu atuzidishie ustahimilivu na ufahamu katika kupambana na nguvu ya matamanio ili tuepuke majuto ya muda mrefu maishani mwetu.....
MTU ISIPOMFAA AKILI YAKE BASI UTAMDHURU UJINGA WAKE.......
....