Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
POLISI: HATUNA TAARIFA UTEKWAJI WA MWANDISHI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia kamanda Mussa Taibu limesema halina taarifa za kutekwa kwa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Bollen Ngeti, ambaye inadaiwa kuwa ametekwa leo na watu wasiojulikana eneo la Msasani, DSM.
=======
UPDATES
Kwa mujibu wa mke wa Bollen Ngeti, mumewe alimfahamisha kuwa amekamatwa akiwa maeneo ya Banana jijini Dar na alikuwa anahofia usalama wake
Bollen alimtaka mkewe awafahamishe watu haraka na alihisi ni katika sakata la Tito Magoti
#JFLeo #FreeBollenNgeti #FreeTitoMagoti
Zaidi soma:
- Dar: Mwandishi wa habari Bollen Ngetti akamatwa na Polisi, apelekwa Sitakishari
- Bollen Ngetti: Utawala wa Rais Magufuli na hatima ya CCM
- Bollen Ngetti CCM maarufu kwa kuikosoa Serikali na chama chake mitandaoni anusurika kifo baada ya gari lake kugongwa na gari lililokuwa likiwafuatilia
- Bollen Ngetti: Dk. Bashiru, Membe si size yako, kaa kimya
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana