Dar: Panya Road wengine 25 wapandishwa Mahakamani, wasomewa mashtaka 6

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Kundi lingine la wahalifu 25 ambao wengi wao ni Vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ waliokamatwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Kinyerezi Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha ikiwemo mapanga.

Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Fadhili Luvinga kusomewa mashtaka sita yanayowakabili.

Waendesha Mashtaka, Mawakili wa Serikali Michael Ng'hoboko, Avelina Ombock na Nancy Mushumbusi walidai kuwa watuhumiwa kwa nyakati tofauti walitenda makosa hayo Aprili 24, 2022, Aprili 29, 2022 na Mei 25, 2022 na maeneo ya Gongo la Mboto, Kipunguni na Karakata Jijini Dar es Salaam.

Walidai watuhumiwa hao walifanya matukio kwa Wananchi mbalimbali kwa kutumia mapanga na kujeruhi kwa lengo la kupora mali.

Waendesha Mashtaka walidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na waliomba tarehe kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka yao na kesi zao ziliahirishwa kwa tarehe tofauti ikiwemo 26/05/2022 na 30/05/2022 ambapo wamepelekwa rumande kutokana na makosa waliyoshtakiwa nayo hayana dhamana.
 
Hivi hakunag panya wa kike wote ni wa kiume tuu?!
 
Af kama vile.wengi wao wana staili flan ya nywele. N kama zimesukwa pembeni af kati ziko chini. Madogo kabisa. Na wakubwa on the background
 
Kuna vigogo wanapiga matirioni ya kodi zetu na wala hawajakamatwa, sasa hawa watoto wamepora tirion ngapi hadi uwaombee wauwawe kabisa?

Waporaji waliotangulia (vigogo) hao ndio unapaswa kuwaombea hiyo adhabu iwapate na sio hawa watoto
Unawafuga hao watoto? Na wao wakaibe matrilioni
 
Vijana wadogo wamegeuka wanyang'anyi, inasikitisha
 
Unawafuga hao watoto? Na wao wakaibe matrilioni
Waliotangulia kuiba mabilion wanaishi kama malaika wanakula bata kwa kwenda mbele, hivi kwa nini hawakamatiki hao mafisadi?

Sasa hawa watoto wameiba simu na TV ndio mnaona hawafai wkt wezi nguli wanapeta enzi na enzi!

Bila hata aibu wanatangaza wamewakamata panya road na kuwafikisha mahakamani 😀
 
Waliotangulia kuiba mabilion wanaishi kama malaika wanakula bata kwa kwenda mbele, hivi kwa nini hawakamatiki hao mafisadi?

Sasa hawa watoto wameiba simu na TV ndio mnaona hawafai wkt wezi nguli wanapeta enzi na enzi!

Bila hata aibu wanatangaza wamewakamata panya road na kuwafikisha mahakamani [emoji3]
Ushawahi kutishiwa panga na kibaka mkuu?

Usiombe. Sisapoti uhalifu wa aina yyt ila bora hao wanaotuibia kimya kimya (kistaatab [emoji23])
 
Kuna panya road wengine wapo 19 ndani ya Bunge letu, afande siro peleka vijana wako haraka kule panya zinatafuna bilions of money,

Panya buku 2 cry ana watetea.
 
Kuna vigogo wanapiga matirioni ya kodi zetu na wala hawajakamatwa, sasa hawa watoto wamepora tirion ngapi hadi uwaombee wauwawe kabisa?

Waporaji waliotangulia (vigogo) hao ndio unapaswa kuwaombea hiyo adhabu iwapate na sio hawa watoto
Ushawahi kupigwa panga la kichwa mkuu?, kukosa amani na kutishiwa uhai? ngoja nikusaidie kujibu "Hapana."
Sasa siku subiri upigwe panga la kichwa au ukatwe mikono na hao unaowaita watoto alafu utajua maumivu ya mafisadi ambao hawakudhuru physically na watoto wanaokupiga panga na kutishia maisha na uhai wako.
 
Back
Top Bottom