Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Wachina watageuza Tz kuwa jalala la kutupia bidhaa zao zinazokataliwa ulaya na Marekani
Mamlaka za serikali idhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia kutoka China.

Pia serikali itenge eneo ndani ya nchi liitwe China Town kwa ajili ya makazi yao rasmi, biashara, waishi kwa tamaduni zao kama China.
 
Hivi vikazi ndio tunalialia machozi ya damu kwamba tunanyanganywa, wakati kazi creme de la creme ambazo zingepatikana huko migodini kusimamia watu, au huko kwenye mbuga kwa watalii au kula full cake (sio commission) bandarini tunawapa watu kwamba sisi hatuwezi kufanya....
 
binafsi napenda hata lile soko la wachina pale Ubungo stand ya zamani liishe haraka ili ninyi watu wa kariakoo mshike adabu na muache umungumtu.biashara huru sio kuwa na syndicates, ni competition. msiogope competition kama ninyi huwa hamnyonyi raia.
Una upeo mdogo sana
 
Wewe ni mtumishi wa umma hujui hustling huku mtaani unadhani mchina akija eneo lako na akiuza bidhaa kama unayouza wewe utatoboa?
Mwenzako anaongea kichina na bidhaa zinatoka kwao bei yk anakuja nayo ya chini kabisa sasa huwezi kumzidi kwa chochote.
Ndo maana ninemwambia ana upeo mdogo
 
Hivi idadi ya wachina nchini ikifika robo ya idadi ya watanzania kiuchumi nchi itakuwaje?

Pia nashauri mamlaka izibe mianya ya wachina kutorosha pesa nje. Wanachokipata waendelee kukiwekeza hapa hapa kwenye kujenga viwanda n.k. Hope miaka 10 ijayo Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa kwenye viwanda.
Wewe unaakili nyingi sana, utoroshaji uzuiliwe, wapewe access yenye wepesi ili faida yao waiwekeze hapa!, that s all bright men did!, sijui kama hawa maprofesa wetu wana akili za upeo wa kiasi hiki.
 
Wewe unaakili nyingi sana, utoroshaji uzuiliwe, wapewe access yenye wepesi ili faida yao waiwekeze hapa!, that s all bright men did!, sijui kama hawa maprofesa wetu wana akili za upeo wa kiasi hiki.
Utoroshaji utazuiliwaje hibi unajua kuna magari mangapi ya gharama yananunuliwa ? Watu wananunua magari ya mabilioni ya shilingi. Hio hela wangewekeza kwenye viwanda hapa nyumbani uchumi ungekua. Kuwepo na kodi maalumu ya maari ya luxuri ikiwezekana iwe mara kumi ya bei kama singapore.
 
Nilienda ofisi za kinglion pale mwenge kununua guta iliniuma watanzania kuona wameajiliwa kwenye ajira za kutumwa tumwa na nzito zenye ujira mdogo wakati huo wachina wameshika nafasi zenye pesa nono na ambazo siyo za manguvu.Nikamuona mkurugenzi anaendeshwa kwenye V8GXR nikawaza hivi watanzania tunashindwa Nini kufanya biashara kama wenzetu?
Wewe hizo biashara kubwa za kuwalipa watanzania wenzako mishahara minono unazo ngapi ?
 
binafsi napenda hata lile soko la wachina pale Ubungo stand ya zamani liishe haraka ili ninyi watu wa kariakoo mshike adabu na muache umungumtu.biashara huru sio kuwa na syndicates, ni competition. msiogope competition kama ninyi huwa hamnyonyi raia.
Walifanya hivyo kenya sema wakenya sio wajinga kama sisi
1730721098732.png

https://www.theafricareport.com/289...-square-shop-as-local-traders-feel-the-pinch/
 
ila watu wote wenye akili huwa hawaogopi competition, jitafakari upo kapu lipi.
China wenyewe wanawekea ngumu makampuni ya marekani na ulaya kufanyabiashara china wanafanya hivyo kulinda makampuni yao sembuse Tanzania

Hakuna nchi duniani hailindi makampuni yake
Competition iwe kwenye soko la dunia sio ndani ya nchi
 
Wawekezaji kutoka China wakiendelea na shughuli za uwekezaji wa biashara zao Jijini Dar.

Pia soma Samia: Msiruhusu Wageni Kufanya Biashara za Wenyeji

====

UNAPOTEMBEA katika Mitaa ya Agrey, Nyamwezi, Livingstone, Swahili na Congo jijini Dar es Salaam, ni kawaida kuona raia wa kigeni wakifanya kazi ambazo zinapaswa kufanywa na Watanzania na wao kufanya kazi za kitaalamu na uwekezaji.

Hawa wageni wanapaswa kuwapo katika kazi za kitaalam na uwekezaji mkubwa, huku wakitakiwa kutekeleza majukumu yao katika kazi za kitaaluma.

Raia hao wenye asili ya China hutumia mbinu mbalimbali zikiwamo kuwa na maduka ambayo huonyesha wanauza bidhaa kwa jumla, lakini hugeuka kuwa wauzaji wa rejareja na wakati mwingine huchuuza bidhaa kutoka eneo moja hadi jingine la jiji la Dar Es Salaam.

Hivi karibuni, palizuka mgogoro baina ya raia wa China na Mtanzania wakigombea eneo la kupanga bidhaa zao.

Picha jongefu za tukio hilo zilisambaa kwa kasi kubwa kwenye mitaandao ya kijamii hatua iliyomshtua Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye aliagiza mamlaka za serikali kuhakikisha raia wa kigeni wanafanyakazi kwa mujibu wa vibali vyao, huku akitaka kazi za Watanzania kulindwa.

Aidha, alitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo, ā€œNimeona video Mchina akipigana na mwenyeji tena mwanamke, mchina mwanaume na mwenyeji mwanamke, ngumu za kweli kweli, nilipouliza kulikoni nikaambiwa yule Mchina naye anauza mitumba, biashara ya wenyeji, tena wenyeji vijana wetu. Hilo nalo kalitizameā€.

ā€œKama biashara haifai kufanywa na watu wa nje wasifanye, sababu ni nini mpaka wanapewa leseni ya kufanyabiashara za aina ile, na kama hawapewi leseni kwanini wanafanyabiashara za aina ile.ā€

Sidhani kama upo Sawa katika hili. Hao wanasindikiza mizigo yao kuelekea dukani. Wasipofanya hivyo wabongo wengi huwa mzigo wanatokomea nao. Sasa ili kudhibiti hilo,mchina anaamua kukomaa na mzigo wake jino kwa jino.
 
Aidha, alitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo, ā€œNimeona video Mchina akipigana na mwenyeji tena mwanamke, mchina mwanaume na mwenyeji mwanamke, ngumu za kweli kweli, nilipouliza kulikoni nikaambiwa yule Mchina naye anauza mitumba, biashara ya wenyeji, tena wenyeji vijana wetu. Hilo nalo kalitizameā€.
Hiyo kauli ya nwisho ndo inamfelisha Sa100.

Badala ya kutamka kuwa ni MARUFUKU ili itekelezwe chap, anaishia tu kusema "Hilo nalo kalitizame." Duh!!!
 
Back
Top Bottom