Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

We jidanganye kuwa mchina ni mwenzako. Nionyeshe shule, hospital au miradi ya maji ili jengwa kwa msaada wa WACHINA ili iwasaidie wazawa.
Huwa nashangaa sana, kwahio mtu akiwapa misaada ndio anakuwa mtu wa maana kwenu. Nyie kwanini msijitume kuijenga nchi yenu
 
Hakuna miujiza hapo, ni 10% na wale ndugu zetu hawanaga mkono wa birika wakitaka mambo yao yaende. Mwekezaji anakuja na $30 millions ila katika hizo hela anajua atatumia $3 millions ili kuweka mambo sawa. Wameshaambiwa na wenzao walioko huku kuwa bongo panaingilikaje.

Kama unavyotujua wabongo wakitaka rushwa viswahili huwa ni vingi na kuzungushana. Wao huwa wanadili na mamlaka za juu tu. Kamishna anawekwa kwapani, Mkurugenzi wa TBS kwapani, Waziri wa ardhi kwapani wakimaliza na IGP kwapani biashara imeisha.
Nahisi wachina wana mashushushu wa kibiashara Tz. Jamaa wamejipanga kuliko unavyofikiri. Kuna jamaa yangu alihusika kuanzisha kiwanda from A mpaka Z. Jamaa walipata industrial plot na hati fasta. Je ushawahi kusikia industrial plot inauzwa? Ila hao wachina walienda huko Ardhi fasta wakapata eneo. Wakajenga kiwanda fasta wakakimbiza kila kitu FASTA FASTA kiwanda kikaanza kazi. 🤣🤣🤣. Wachina wako vizuri mno 🤣 yaani connection+10% ni balaa
 
Wachina watazidi kumiminika sana bongo sababu mazingira ni rafiki. Bongo sheria ziko imara kwa maskini tu ila ukiwa na hela unahonga maaskari maisha yanaenda. Wao wanapokuja huku wanakuja na hela. We unamuona machinga ila ana hela ya kutosha ndio maana huwezi kukuta mchina anaishi Tandale au Vikindu wengi wamechukua apartments za kodi za laki 5 au zaidi kwa mwezi tena mostly wanaishi prime areas kama Kariakoo, Upanga, Oysterbay na Masaki.
Hiko si kielelezo, kuna limit kisheria kwamba kazi zipi zinaruhusiwa kufanywa na wageni ili kulinda kazi za wazawa, huwezi kumruhusu mtu afanye umachinga kisa kapanga apartment ya gharama
Hiyo ni personal life yake

Gov isipodhibiti hilo now, hali itakuwa mbaya mbeleni
 
sioni shida yeyote hapo, kwani ninyi mnaogopa nini? mnaogopa ushindani? ukienda china leo hii ukaseme ufanye kazi hizi za hali ya chini wakakuzuia utajisikiaje?

Sisi wabongo tufanye biashara tushindane nao, kwani tunawaogopa? na mbona bidhaa zao ni bei poa kuliko za kwenu au mnataka muendelee na syndicate zenu kuuzia watu vitu bei ya juu.
Nenda china kama hawajakuua? Ni wabaguzi sana wa rangi! Kuna watz wengi sana wameuwawa na walikuwa wanasoma! Washenzi sana Hawa!
 
Nilienda ofisi za kinglion pale mwenge kununua guta iliniuma watanzania kuona wameajiliwa kwenye ajira za kutumwa tumwa na nzito zenye ujira mdogo wakati huo wachina wameshika nafasi zenye pesa nono na ambazo siyo za manguvu.Nikamuona mkurugenzi anaendeshwa kwenye V8GXR nikawaza hivi watanzania tunashindwa Nini kufanya biashara kama wenzetu?
WaTz uaminifu ni bidhaa adimu, wacha tunyooshwe.
 
binafsi sioni shida yeyote mchina akiuza hata chips.

Mgeni yeyote anapoingia nchi yeyote kufanya chochote lazima apewe vibali na mamlaka za nchi husika kufanya hicho anachotakiwa kufanya.

Nenda china leo hii kaombe kibali cha kufanya biashara ya umachinga mitaani.
 
Nchi imefunguliwa,
Wachina ni ndugu zetu, mabeberu ni mashoga😁
 
Wawekezaji kutoka China wakiendelea na shughuli za uwekezaji wa biashara zao Jijini Dar.

Pia soma Samia: Msiruhusu Wageni Kufanya Biashara za Wenyeji

====

UNAPOTEMBEA katika Mitaa ya Agrey, Nyamwezi, Livingstone, Swahili na Congo jijini Dar es Salaam, ni kawaida kuona raia wa kigeni wakifanya kazi ambazo zinapaswa kufanywa na Watanzania na wao kufanya kazi za kitaalamu na uwekezaji.

Hawa wageni wanapaswa kuwapo katika kazi za kitaalam na uwekezaji mkubwa, huku wakitakiwa kutekeleza majukumu yao katika kazi za kitaaluma.

Raia hao wenye asili ya China hutumia mbinu mbalimbali zikiwamo kuwa na maduka ambayo huonyesha wanauza bidhaa kwa jumla, lakini hugeuka kuwa wauzaji wa rejareja na wakati mwingine huchuuza bidhaa kutoka eneo moja hadi jingine la jiji la Dar Es Salaam.

Hivi karibuni, palizuka mgogoro baina ya raia wa China na Mtanzania wakigombea eneo la kupanga bidhaa zao.

Picha jongefu za tukio hilo zilisambaa kwa kasi kubwa kwenye mitaandao ya kijamii hatua iliyomshtua Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye aliagiza mamlaka za serikali kuhakikisha raia wa kigeni wanafanyakazi kwa mujibu wa vibali vyao, huku akitaka kazi za Watanzania kulindwa.

Aidha, alitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo, “Nimeona video Mchina akipigana na mwenyeji tena mwanamke, mchina mwanaume na mwenyeji mwanamke, ngumu za kweli kweli, nilipouliza kulikoni nikaambiwa yule Mchina naye anauza mitumba, biashara ya wenyeji, tena wenyeji vijana wetu. Hilo nalo kalitizame”.

“Kama biashara haifai kufanywa na watu wa nje wasifanye, sababu ni nini mpaka wanapewa leseni ya kufanyabiashara za aina ile, na kama hawapewi leseni kwanini wanafanyabiashara za aina ile.”

Naona kama wanalinda mizigo yao baada ya kuibiwa kupitiliza na wezi wa kko!
 
“Nimeona video Mchina akipigana na mwenyeji tena mwanamke, mchina mwanaume na mwenyeji mwanamke, ngumu za kweli kweli, nilipouliza kulikoni nikaambiwa yule Mchina naye anauza mitumba, biashara ya wenyeji, tena wenyeji vijana wetu. Hilo nalo kalitizame”.
Yaani hapo eti mtu mwenye mamlaka ndiyo ameagiza! 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nchi yetu hivi sasa inapita kwenye majaribu makubwa,mtu anaweza akatoka kokote akaja kuchezea Watanzania kadri awezavyo.
 
Hivi idadi ya wachina nchini ikifika robo ya idadi ya watanzania kiuchumi nchi itakuwaje?

Pia nashauri mamlaka izibe mianya ya wachina kutorosha pesa nje. Wanachokipata waendelee kukiwekeza hapa hapa kwenye kujenga viwanda n.k. Hope miaka 10 ijayo Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa kwenye viwanda.
 
Hivi idadi ya wachina nchini ikifika robo ya idadi ya watanzania kiuchumi nchi itakuwaje?

Pia nashauri mamlaka izibe mianya ya wachina kutorosha pesa nje. Wanachokipata waendelee kukiwekeza hapa hapa kwenye kujenga viwanda n.k. Hope miaka 10 ijayo Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa kwenye viwanda.
Wachina watageuza Tz kuwa jalala la kutupia bidhaa zao zinazokataliwa ulaya na Marekani
 
Mkuu na kuunga mkono kwa mtazamo huu, serikali ilitakiwa Kuboresha maslahi ya watumishi wake na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kutoboa na wenyeji kutoka ili kila mtanzania awe na shughuli inayomuingizia kipato cha kizuri.

Infact umachinga ulitakiwa ufanywe na wageni. Sisi tunafanya kinyume chake, watanzania tuna shida mahali.
Wazawa wanataka wawe wamachinga wageni ndio wamiliki viwanda 😆
 
“Kama biashara haifai kufanywa na watu wa nje wasifanye, sababu ni nini mpaka wanapewa leseni ya kufanyabiashara za aina ile, na kama hawapewi leseni kwanini wanafanyabiashara za aina ile.”
Babu wa Babu zao walijenga reli ya kati walifia kwenye miamba, makaburi yao yapo mpaka kesho hapo kambi ya Jeshi ukonga Gongo la Mboto km unaelekea Pugu kushoto kwa hio Mimi siwachukulii km Wageni watu km hao nawachukulia km ndugu
 
Back
Top Bottom