Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

wachache sana waliowahi kuishi nje wakabaguliwa kwenye fursa ndio watakuwa na uelewa kwamba mchina akifanya kazi yeyote hapa, kama haingilii maslahi yako na hakudhuru, hakuna shida. mwacheni afanye biashara. au wanataka tuwe kama wasouth, wavivu, wakiona wabongo na wasomali wanafanya biashara, wanawauwa ati wanafaidikia kwenye nchi yao, kwani wewe bongo wa kariakoo ukiona mchina anfanya biashara, na wewe si ufanye? anakuzuia nini? weka service nzuri mshindane, kwani tukija kwenye duka lako bila uwepo wa wachina unatupatia bidhaa bure? wapambane wawashinde wachina. pia wajue na wao kuna sikuw ataenda china, watazuiwa, wataenda ufaransa watazuiwa, wataenda ulaya watazuiwa, watajisikiaje wakati wanatafuta kipato?
Wewe ni mtumishi wa umma hujui hustling huku mtaani unadhani mchina akija eneo lako na akiuza bidhaa kama unayouza wewe utatoboa?
Mwenzako anaongea kichina na bidhaa zinatoka kwao bei yk anakuja nayo ya chini kabisa sasa huwezi kumzidi kwa chochote.
 
Mkuu huku Kanda ya Ziwa wakenya,wanyarwanda na waganda wanatufikia Hadi mashambani kijijini wakinunua nyanya,vitunguu,na dengu!! Najiuliza ukienda Rwanda unaweza ingia Hadi kijijini kweli kufuata mazao? Wazawa watafanya issue Gani Sasa. Mimi nalima nyanya na wateja wangu wanyarwanda wanakuja kijijini wanalala mashambani huko Bila wasiwasi. Chato yote wateja ni kutoka Uganda. Wanunua dengu maeneo sarawe ni nk wateja wao ni wakenya!
they are more aggressive kuliko sisi, badala ya wewe kushukuru sasa angalau unauzia nyanya zako shambani, unawalaumu wakizuiwa, nyanya zako zitaozea shambani utaanza kulialia!
P
 
Nilienda ofisi za kinglion pale mwenge kununua guta iliniuma watanzania kuona wameajiliwa kwenye ajira za kutumwa tumwa na nzito zenye ujira mdogo wakati huo wachina wameshika nafasi zenye pesa nono na ambazo siyo za manguvu.Nikamuona mkurugenzi anaendeshwa kwenye V8GXR nikawaza hivi watanzania tunashindwa Nini kufanya biashara kama wenzetu?
Wenzetu wana mitaji mikubwa serikali inawakopesha. Wachina wanapewaga kati ya 200M mpaka 500M per head kuja kuanzisha biashara Africa huku.

Anajipanga kuanzia kiwandani analipa 50% ya fedha anachukua mzigo kwa mali kauli kwa guarantee ya serikali. Wakija huku fursa wanaziona kwa haraka sababu vitu vingi walivyonavyo sisi hatuna.

Niambie ili upewe 200M bongo utahitaji kuzungushwa miaka mingapi?😂 Mikopo tu ya million 10 mtaambiwa mjipange muende kama wanakijiji 🤣 na huo mkopo kupewa mtazungushwa mwaka mzima.
 
they are more aggressive kuliko sisi, badala ya wewe kushukuru sasa angalau unauzia nyanya zako shambani, unawalaumu wakizuiwa, nyanya zako zitaozea shambani utaanza kulialia!
P
Nasema kinachoonekana mkuu. Mimi nifaida kwangu huu ndo ukweli. Lakini tatizo lipo kwenye Nchi yetu maana nyanya zinazo enda Rwanda na Kenya wanenda kusindika Ili Hali hata sisi kama serikali ingeleta wawekezaji wa maanatungeuza Kwa bei ya utupwa. Kipindi Cha himaya nyani mipaka ilifungwa nyanya zikashuka bei sana. Hii yote serikali haimjari mkulima. Ukiangalia hatuna viwanda vya kusindika nyanya zetu zikikoswa wateja siku3 Zina haribika zote!!

Serikali iwekeze kwenye viwanda tusindike na tuuze Nje mkuu. Hapa ni jukwaani Sioni kitu Cha kuficha Hali halisi ndo hii. Ahsantee
 
Sheria za uwekezaji zinasemaje kuhusu raia wa kigeni? Kazi za kimachinga nadhani hawatakiwi kuziingilia, lakini mamlaka husika ziko kimya, wako busy na uchaguzi
Wachina watazidi kumiminika sana bongo sababu mazingira ni rafiki. Bongo sheria ziko imara kwa maskini tu ila ukiwa na hela unahonga maaskari maisha yanaenda. Wao wanapokuja huku wanakuja na hela. We unamuona machinga ila ana hela ya kutosha ndio maana huwezi kukuta mchina anaishi Tandale au Vikindu wengi wamechukua apartments za kodi za laki 5 au zaidi kwa mwezi tena mostly wanaishi prime areas kama Kariakoo, Upanga, Oysterbay na Masaki.
 
sioni shida yeyote hapo, kwani ninyi mnaogopa nini? mnaogopa ushindani? ukienda china leo hii ukaseme ufanye kazi hizi za hali ya chini wakakuzuia utajisikiaje?

Sisi wabongo tufanye biashara tushindane nao, kwani tunawaogopa? na mbona bidhaa zao ni bei poa kuliko za kwenu au mnataka muendelee na syndicate zenu kuuzia watu vitu bei ya juu.
Una hoja ,ila sidhani kama anazijua Sheria za uhamiaji.
 
Wenzetu wana mitaji mikubwa serikali inawakopesha. Wachina wanapewaga kati ya 200M mpaka 500M per head kuja kuanzisha biashara Africa huku.

Anajipanga kuanzia kiwandani analipa 50% ya fedha anachukua mzigo kwa mali kauli kwa guarantee ya serikali. Wakija huku fursa wanaziona kwa haraka sababu vitu vingi walivyonavyo sisi hatuna.

Niambie ili upewe 200M bongo utahitaji kuzungushwa miaka mingapi?😂 Mikopo tu ya million 10 mtaambiwa mjipange muende kama wanakijiji 🤣 na huo mkopo kupewa mtazungushwa mwaka mzima.
🤣

Wachina wanapewa mikopo na serikali yao. Pia wanapewa mali za mabilioni toka viwandani kwao kwa mali kauli. China viwanda ni vingi kuliko mahitaji na bidhaa ni mafuriko na wana changamoto ya uzalishaji wa bidhaa uliopitiliza, surplus industrial production. Kwa hiyo wakiona nchi yoyote imelegealega wanaifanya soko..

Pia wachina wako bongo kutokana na material za ubora wa chini ambazo ni reject sehemu zote duniani hasa ulaya na Marekani ila kwa nchi za kiafrika zinakubaliwa.

Nakupa siri nyingine kwa nini wachina wako bongo wengi mno. Ni profit margin ya juu ambayo wafanyabiashara wa kitz ambao wanaagiza vitu toka nchini kwao. Profit margin ya watz ukilinganisha bei ya kununua china+usafiri+kodi na bei ya kuuza Tz ni kama mara 2 mpaka mara 15+. Ndio maana wachina wanafurika. Na wanajenga kituo cha biashara zao na viwanda vyao huku Tz Ubungo. Hiyo kariakoo itabaki stori tu 🤣🤣
 
WACHINA siyo wakuwaendekeza, kazi wanazofanya hapa kwao hawakubali tufanye. Sheria ichukue mkondo wake wakabanane huko huko kwao.
Bongo sheria haifanyi kazi kwa mtu mwenye hela. Hao wasimamizi wa sheria ndio wala rushwa wakubwa na wachina kwa kujua hilo ndio wamezidi kuitana nchini.

Sahizi ukienda maeneo ya nyuma ya Kinondoni Morocco Square kule unaweza dhania upo Ghanzhou😄 au Shenzen. Kule ndio wamejitwalia block nzima wamejenga apartments na supermarket zao za kichina na migahawa. Sidhani kama sheria zao zinaweza kuruhusu mbongo akanunue ardhi na kufanya yale yaliofanywa pale Kinondoni.

Ila sababu mamlaka zimeruhusu hayo sisi ni nani hata tupingane na mamlaka. Japo kisheria haliko sawa.
 
Mkienda nchi yao huwa mnaenda kufanya kazi gani?.
Kariakoo sishangai sababu kwenye maduka yao, machinga wameziba hadi milangoni kwao... Mnategemea watafanya nn?. Kuna Wamalawi, Wakenya, Waganda, n.k wanafanya umachinga kkoo na hakuna anayeropoka asa iweje Wachine muwabughudhi?
 
🤣

Wachina wanapewa mikopo na serikali yao. Pia wanapewa mali za mabilioni toka viwandani kwao kwa mali kauli. China viwanda ni vingi kuliko mahitaji na bidhaa ni mafuriko na wana changamoto ya uzalishaji wa bidhaa uliopitiliza, surplus industrial production. Kwa hiyo wakiona nchi yoyote imelegealega wanaifanya soko..

Pia wachina wako bongo kutokana na material za ubora wa chini ambazo ni reject sehemu zote duniani hasa ulaya na Marekani ila kwa nchi za kiafrika zinakubaliwa.

Nakupa siri nyingine kwa nini wachina wako bongo wengi mno. Ni profit margin ya juu ambayo wafanyabiashara wa kitz ambao wanaagiza vitu toka nchini kwao. Profit margin ya watz ukilinganisha bei ya kununua china+usafiri+kodi na bei ya kuuza Tz ni kama mara 2 mpaka mara 15+. Ndio maana wachina wanafurika. Na wanajenga kituo cha biashara zao na viwanda vyao huku Tz Ubungo. Hiyo kariakoo itabaki stori tu 🤣🤣
Mimi nina mtu Kinglion pale😂 jamaa wanauza sana mapikipiki mikoani. Hesabu zao wanazofungakwa mwaka its billions za kutisha 🤣. Kodi wanakwepa ile laana na wako njema kwenye kuhonga mamlaka.

Jamaa wanapiga hela sana, mtu anakuja na mtaji kidogo after 5 years ni billionaire wa kutupa. Nadhani baada ya wahindi na warabu hawa jamaa ndio watakuja ku take over kwenye utajiri bongo.
 
Mimi nina mtu Kinglion pale😂 jamaa wanauza sana mapikipiki mikoani. Hesabu zao wanazofungakwa mwaka its billions za kutisha 🤣. Kodi wanakwepa ile laana na wako njema kwenye kuhonga mamlaka.
🤣 watu wengi wanawachukulia poa wachina. Ila hao wachina wanaifanya biashara ya mabilioni ya hela. Mimi kuna jamaa yangu yumo kwenye chain ya vifaa vya ujenzi vya kichina hasa mabati. Jamaa anasema wanafanya biashara za mabilioni. Boss wao Mchina anataka kujenga viwanda nchi nzima kila wilaya 🤣
 
yaani mimi nihangaike kuunda kampuni, nimetoka china, nimekuja TIC hangaika na maburokrasi kibao, agiza mzigo toka china hata faida sijapata, mimi kama mchina nitamweka mbongo kweli sehemu ya juu?mbonbo? wengi ni wavivu, wezi, wanachelewa kufika kazini na kuwahi kutoka, muda mwingi wanawaza wanawake tu, ulevi n.k ufanisi utatoka wapi hapo, si lazima mtajikuta mnapewa nafasi za chini huko saidia fundi, atakayejirekebisha na kuonyesha ubora ndio huwa anapewa nafasi za juu.
😂 Sio kila mbongo ni mduanzi. Kuna watu smart ila ndo hao weupe wana ubaguzi. Mhindi hana shule anakuja kupewa nafasi ya kiuongozi kwenye kampuni ya muhindi mwenzake. Anatolewa mtu mwenye CPA anawekwa form 4 mwenye cheti cha uhasibu amuongoze mtu mwenye CPA wale jamaa ni mikwunduw sana siwapendi wahindi na kama nikipata urahisi watu wa kwanza kuwafukuza itakuwa wao.

La hashaa wakubali kulipa mishahara mizuri kwa wazawa ambao ni sawa na wanavyolipa wahindi wenzao.
 
🤣 watu wengi wanawachukulia poa wachina. Ila hao wachina wanaifanya biashara ya mabilioni ya hela. Mimi kuna jamaa yangu yumo kwenye chain ya vifaa vya ujenzi vya kichina hasa mabati. Jamaa anasema wanafanya biashara za mabilioni. Boss wao Mchina anataka kujenga viwanda nchi nzima kila wilaya 🤣
Hela wanapata sana, yani mtu anauza unit moja anapata faida 10 folds. Utaachaje kufungua viwanda kila kona. Unaanza na mtaji wa 200M ukimaliza mzigo una billion 2. Utaachaje kufungua viwanda kila kona.🤣

Halafu nachowapendea wachina hawana tabia za kishenzi kama wahindi. Mchina akipiga hela anakuachia gepu na wewe uishi.
 
Hela wanapata sana, yani mtu anauza unit moja anapata faida 10 folds. Utaachaje kufungua viwanda kila kona. Unaanza na mtaji wa 200M ukimaliza mzigo una billion 2. Utaachaje kufungua viwanda kila kona.🤣
Kiufupi hao jamaa wamejipanga kupata utajiri. Ila kuna ubaguzi wa rangi kwenye taasisi Tanzania, mchina akitaka kuanzisha kiwanda anahudumiwa harakaharaka
Akitaka kiwanja (industrial plot)anapewa fasta na hati fasta, vibali anapata fasta, kodi wanapunguziwa fasta, bandarini kilakitu wanafanyiwa fasta,umeme unawekwa kiwandani FASTA,tbs fasta, anazalisha bidhaa fasta zinaingia sokoni fasta. Ukiachana na rushwa pia kuna kama ubaguzi wa rangi kwenye taasisi zinazohusika.

Ukienda wewe ngozi nyeusi utazungushwa mpaka upate kizunguzungu 🤣
 
Wanajua kuitumia mithali hii: Aliyelala usimwamshe!
Watanzania tunalala mno.
Kama kwa ripoti ya sasa hivi inasema 87% ni Tegemezi ina maana(ukiondoa Watoto,Wazee na Walemavu) wavivu ni wengi.
 
Mkuu na kuunga mkono kwa mtazamo huu, serikali ilitakiwa Kuboresha maslahi ya watumishi wake na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kutoboa na wenyeji kutoka ili kila mtanzania awe na shughuli inayomuingizia kipato cha kizuri.

Infact umachinga ulitakiwa ufanywe na wageni. Sisi tunafanya kinyume chake, watanzania tuna shida mahali.
Kinachofanya watu wajazane kwenye umachinga ni lack of government support. Hatuna viwanda vingi sasa utaishije bila kazi. Lazma uanze kuuza makava na chaja za simu bila kusahau sumu za kuua mende na kunguni😂 ilimradi mkono uende kinywani.

Ila kungekuwa na large scale productions masoko ya chakula tu yapo nchi nyingi zinazotuzunguka. Tumekuwa na bahati mbaya na serikali ambayo haina vipaumbele vya kubadilisha maisha ya watanzania kwa dhati. Tunakazana na mambo ambayo impact yake ni ndogo kwa social welfare.
 
Kiufupi hao jamaa wamejipanga kupata utajiri. Ila kuna ubaguzi wa rangi kwenye taasisi Tanzania, mchina akitaka kuanzisha kiwanda anahudumiwa harakaharaka
Akitaka kiwanja (industrial plot)anapewa fasta na hati fasta, vibali anapata fasta, kodi wanapunguziwa fasta, bandarini kilakitu wanafanyiwa fasta,umeme unawekwa kiwandani FASTA. Ukiachana na rushwa pia kuna kama ubaguzi wa rangi kwenye taasisi zinazohusika.

Ukienda wewe ngozi nyeusi utazungushwa mpaka upate kizunguzungu 🤣
Hakuna miujiza hapo, ni 10% na wale ndugu zetu hawanaga mkono wa birika wakitaka mambo yao yaende. Mwekezaji anakuja na $30 millions ila katika hizo hela anajua atatumia $3 millions ili kuweka mambo sawa. Wameshaambiwa na wenzao walioko huku kuwa bongo panaingilikaje.

Kama unavyotujua wabongo wakitaka rushwa viswahili huwa ni vingi na kuzungushana. Wao huwa wanadili na mamlaka za juu tu. Kamishna anawekwa kwapani, Mkurugenzi wa TBS kwapani, Waziri wa ardhi kwapani wakimaliza na IGP kwapani biashara imeisha.
 
Wazawa watafanya shughuli gani?

Wawekezaji kutoka China wakiendelea na shughuli za uwekezaji wa biashara zao Jijini Dar.

Pia soma Samia: Msiruhusu Wageni Kufanya Biashara za Wenyeji

====

UNAPOTEMBEA katika Mitaa ya Agrey, Nyamwezi, Livingstone, Swahili na Congo jijini Dar es Salaam, ni kawaida kuona raia wa kigeni wakifanya kazi ambazo zinapaswa kufanywa na Watanzania na wao kufanya kazi za kitaalamu na uwekezaji.

Hawa wageni wanapaswa kuwapo katika kazi za kitaalam na uwekezaji mkubwa, huku wakitakiwa kutekeleza majukumu yao katika kazi za kitaaluma.

Raia hao wenye asili ya China hutumia mbinu mbalimbali zikiwamo kuwa na maduka ambayo huonyesha wanauza bidhaa kwa jumla, lakini hugeuka kuwa wauzaji wa rejareja na wakati mwingine huchuuza bidhaa kutoka eneo moja hadi jingine la jiji la Dar Es Salaam.

Hivi karibuni, palizuka mgogoro baina ya raia wa China na Mtanzania wakigombea eneo la kupanga bidhaa zao.

Picha jongefu za tukio hilo zilisambaa kwa kasi kubwa kwenye mitaandao ya kijamii hatua iliyomshtua Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye aliagiza mamlaka za serikali kuhakikisha raia wa kigeni wanafanyakazi kwa mujibu wa vibali vyao, huku akitaka kazi za Watanzania kulindwa.

Aidha, alitoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo, “Nimeona video Mchina akipigana na mwenyeji tena mwanamke, mchina mwanaume na mwenyeji mwanamke, ngumu za kweli kweli, nilipouliza kulikoni nikaambiwa yule Mchina naye anauza mitumba, biashara ya wenyeji, tena wenyeji vijana wetu. Hilo nalo kalitizame”.

“Kama biashara haifai kufanywa na watu wa nje wasifanye, sababu ni nini mpaka wanapewa leseni ya kufanyabiashara za aina ile, na kama hawapewi leseni kwanini wanafanyabiashara za aina ile.”

Kwani mnyie mnapoenda nchi za watu huwa mnaenda kufanya shughuli zipi? Huwa mnaenda kuwekeza na kufungua viwanda?

Acheni hizo, waacheni wafanye kile wanachokiweza ili mradi hawavunj sheria. Wakiwafanyieni hivyo kwao mnawaita wabaguzi.
 
Back
Top Bottom