Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Wachina watageuza Tz kuwa jalala la kutupia bidhaa zao zinazokataliwa ulaya na Marekani
Mamlaka za serikali idhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia kutoka China.

Pia serikali itenge eneo ndani ya nchi liitwe China Town kwa ajili ya makazi yao rasmi, biashara, waishi kwa tamaduni zao kama China.
 
Hivi vikazi ndio tunalialia machozi ya damu kwamba tunanyanganywa, wakati kazi creme de la creme ambazo zingepatikana huko migodini kusimamia watu, au huko kwenye mbuga kwa watalii au kula full cake (sio commission) bandarini tunawapa watu kwamba sisi hatuwezi kufanya....
 
binafsi napenda hata lile soko la wachina pale Ubungo stand ya zamani liishe haraka ili ninyi watu wa kariakoo mshike adabu na muache umungumtu.biashara huru sio kuwa na syndicates, ni competition. msiogope competition kama ninyi huwa hamnyonyi raia.
Una upeo mdogo sana
 
Wewe ni mtumishi wa umma hujui hustling huku mtaani unadhani mchina akija eneo lako na akiuza bidhaa kama unayouza wewe utatoboa?
Mwenzako anaongea kichina na bidhaa zinatoka kwao bei yk anakuja nayo ya chini kabisa sasa huwezi kumzidi kwa chochote.
Ndo maana ninemwambia ana upeo mdogo
 
Wewe unaakili nyingi sana, utoroshaji uzuiliwe, wapewe access yenye wepesi ili faida yao waiwekeze hapa!, that s all bright men did!, sijui kama hawa maprofesa wetu wana akili za upeo wa kiasi hiki.
 
Wewe unaakili nyingi sana, utoroshaji uzuiliwe, wapewe access yenye wepesi ili faida yao waiwekeze hapa!, that s all bright men did!, sijui kama hawa maprofesa wetu wana akili za upeo wa kiasi hiki.
Utoroshaji utazuiliwaje hibi unajua kuna magari mangapi ya gharama yananunuliwa ? Watu wananunua magari ya mabilioni ya shilingi. Hio hela wangewekeza kwenye viwanda hapa nyumbani uchumi ungekua. Kuwepo na kodi maalumu ya maari ya luxuri ikiwezekana iwe mara kumi ya bei kama singapore.
 
Wewe hizo biashara kubwa za kuwalipa watanzania wenzako mishahara minono unazo ngapi ?
 
ila watu wote wenye akili huwa hawaogopi competition, jitafakari upo kapu lipi.
China wenyewe wanawekea ngumu makampuni ya marekani na ulaya kufanyabiashara china wanafanya hivyo kulinda makampuni yao sembuse Tanzania

Hakuna nchi duniani hailindi makampuni yake
Competition iwe kwenye soko la dunia sio ndani ya nchi
 
Sidhani kama upo Sawa katika hili. Hao wanasindikiza mizigo yao kuelekea dukani. Wasipofanya hivyo wabongo wengi huwa mzigo wanatokomea nao. Sasa ili kudhibiti hilo,mchina anaamua kukomaa na mzigo wake jino kwa jino.
 
Hiyo kauli ya nwisho ndo inamfelisha Sa100.

Badala ya kutamka kuwa ni MARUFUKU ili itekelezwe chap, anaishia tu kusema "Hilo nalo kalitizame." Duh!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…