Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Kifo cha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Konstebo Kulwa Gilbert, aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake, kimezua mshtuko kwa ndugu, jamaa, askari wenzake na majirani aliokuwa akiishi nao nyumbani kwake, Ukonga-Mazizini jijini Dar, Gazeti la Uwazi pekee ndilo lenye mkasa mzima wa tukio hilo.

NI SINZA JIJINI DAR
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea Jumanne ya wiki iliyopita, majira ya jioni wakati afande Kulwa na FFU wenzake wakiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi wakishusha pesa kwa ajili ya kuziweka kwenye mashine ya ATM ya Benki ya CRDB iliyopo Sinza-Mori pembezoni mwa Kituo cha Mafuta cha Big Bon, jijini Dar.

Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Uwazi kuwa, wakati maafande hao wakiwa kwenye harakati za kushusha pesa hizo karibu na mashine hiyo, kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine hiyo hivyo afande Kulwa na wenzake walimuamrisha aondoke haraka eneo hilo kwa sababu za kiusalama.

MASHUHUDA WASIMULIA
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda hao, Jimmy Kaishozi, mkazi wa Sinza-Meeda, mwanajeshi huyo, baada ya kupewa amri ya kuondoka haraka eneo hilo, aliona kama amedharauliwa na askari hao hivyo aliwataka wamwambie kistaarabu na siyo kumwamrisha.

Kaishozi alisimulia kuwa, hali hiyo ilizua malumbano kati ya askari hao na mwanajeshi huyo ambapo Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea ambapo mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuwa alikuwa na utaalam wa masuala ya silaha.

“Kitendo hicho kilizidisha taharuki ambapo askari mwingine wa FFU naye alitoka kwenye gari lililokuwa limebeba pesa na bunduki nyingine na kumlenga mwanajeshi huyo, lakini katika hali iliyoonekana kama bahati mbaya, risasi hizo zilimpata afande Kulwa na nyingine ilimlenga mwanajeshi huyo.

“Hapo mapambano yalizidi kukolea kama sinema ya kivita ambapo askari aliyekuwa akilenga shabaha, alipoona amempiga mwenzake, aliikoki tena bunduki na kumpiga risasi nyingine mwanajeshi huyo ambapo afande Kulwa na mwanajeshi huyo, wote walianguka chini na kuanza kutapatapa huku wakitokwa na damu nyingi.

“Ilichukua muda wakigaragara chini hadi walipofika askari wa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) na kuwachukua, sijui walipelekwa wapi,” alisimulia Kaishozi.

KITUO CHA MABATINI
Hata hivyo, habari kutoka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ambapo mwandishi wetu alifika, baadhi ya polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakisema kuwa majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wakiwa njiani afande Kulwa aliaga dunia.

MAKAO MAKUU FFU
Mwandishi wetu pia alikwenda Makao Makuu ya Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga-Madafu jijini Dar ambapo aliwakuta askari wenzake marehemu ambao walionesha hisia za majonzi wakati wakizungumzia kifo cha mwenzao huyo.

Askari hao hawakuwa tayari kuandikwa majina kwa maelezo kuwa hawaruhusiwi ambapo walimwelekeza mwandishi wetu nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mazizini jijini Dar.

NYUMBANI KWA MAREHEMU
Mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa marehemu, lakini alikuta chumba chake kimefungwa ambapo mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema kuwa, msiba ulihamishiwa Tazara-Mchicha kwa dada yake aitwae Doto ambaye ndiye pacha wake.

Mwandishi wetu alizungumza na majirani aliowakuta eneo hilo ambao walisema kuwa, kifo hicho kilisababisha mshtuko mkubwa mtaani hapo na kuibua majonzi makubwa.
Kutokana na afande huyo kuishi vizuri na majirani zake, mwandishi wetu aliwakuta wakiendelea kuchangisha pesa za rambirambi huku wakiwa na picha ya marehemu.
ACP Muliro Jumanne Muliro.

UJIJI, KIGOMA KWA MAZISHI
Mwanahabari wetu pia alifika alipoelekezwa ulipokuwa msiba huo, lakini alipofika alikuta tayari mwili wa marehemu ulishasafirishwa kupelekwa kijijini kwao, Ujiji mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

MWANAJESHI MUHIMBILI
Habari kutoka Muhimbili zilidai kuwa mwanajeshi aliyepata kisanga hicho yeye anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo japokuwa hakuna afisa habari yeyote katika hospitali hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.

“Ni kweli huyo mwanajeshi yupo, lakini chini ya ulinzi mkali, itakuwa vigumu ninyi kumuona,” alisema mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini hospitalini hapo.

KAMANDA MAMBOSASA
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema angempigia mwandishi baadaye.

KAMANDA MULIRO
Mwandishi aliamua kumpigia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro na alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema ni vema kuzungumza na Kamanda wa Kanda Maalum.

“Ndugu yangu si unajua kuwa kuna Kamanda wa Kanda Maalum? Mpigie yeye,” alisema Kamanda Muliro.

Alipoambiwa amepigiwa hajajibu swali ndiyo maana akapigiwa yeye RPC, Muliro alisema atampigia yeye Mambosasa.

Mwandishi alimpigia simu tena Kamanda Mambosasa na kumueleza kuhusiana na tukio hilo ndipo akasema yupo chumba cha daktari na akaahidi kumpigia mwandishi baadaye.

MSEMAJI WA POLISI
Hata hivyo, ili kupata undani wa tukio hilo, pia Uwazi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Barnabasi Mwakalukwa na kumuuliza juu ya taarifa za tukio hilo ambapo aliomba atafutwe Kamanda Mambosasa.

“Hilo jambo anayepaswa kulizungumzia ni Kamanda Mambosasa, mtafuteni huyo,” alisema Kamanda Mwakalukwa.

UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.

Haikujulikana mara moja kama polisi aliyempiga risasi mwenzake pamoja na mwanajeshi huyo kama amekamatwa au la.

KUMRADHI
Jina la Konstebo Justine Mtesigwa, ambalo awali lilitumika kwenye habari hii kwenye gazeti la Uwazi leo kwamba ndiye aliyeuawa lilikosewa, jina sahihi ya aliyeuawa ni konstebo Kulwa Gilbert. Justine na Kulwa walikuwa ni marafafiki na walikuwa wakifanyakazi pamoja Ukonga. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa Justine, ndugu, jamaa, marafiki na wafanayakazi wenzake – Mhariri.

Stori: Richard Bukos, Dar.

My Take;
Polisi wawili kupambana na Mwanajeshi mmoja asiye na silaha na kuishia kuuana wenyewe ni picha kuwa hawa wanahitaji mafunzo ya uhakika ili unyonge wao wasiutumie kuwaonea raia wasio hatia
Niliwahi andika humu JF kuwa Kamanda wa Mafunzo nabOperations Polisi ni Kilaza.
Product za mafunzobya kipolisi ni hovyo kabisa.
No weledi.
 
Hili swala gumu,
Wanajeshi wana tabia ya kujiona sana,,na hao wengine nao lugha chafu coz of bangi,
 
Sio dharau bwana mdogo nakupa makavu ujue mwanaume kamili adharau kaz ya mwanaume mwenzie
...na mwanaume kamili halingishii uanaume wake kwa mwanaume mwenzake au vipi??
Ulienda mwenyewe polisi, hatukukutuma sisi, wewe fanya kazi yako kwa mujibu wa mkataba wako siyo kutisha tisha watu na uanaume wako
 
Ndo maana UN walisema kuna mapungufu katika mafunzo na vijana wa jwtz hili swala inatakiwa liangaliwe kwa jicho pevu sana

Hili tukio limitufumbua macho nidhamu ya vijana wetu wa jwtz
nimegundua huna ulijualo ww kasome tena UN walisemaje ?usiongopee watu nyie ndo mnaodanganyana vijiweni.
 
Hivi vyombo viwili vya ulinzi hapa nchini sidhani kama iko siku vitapatana na kufanya kazi pamoja kwa moyo mmoja maana maisha yote
Polisi
Ye siku zote anajihisi anadharauliwa
Hajiamini
Silaha ndio mtetezi wake
Yuko juu ya sheria

Mwanajeshi
Ye siku zote anajihisi hawezi kudharauliwa na aliye chini yake
Anajiamini sana
Hata kama hana silaha
Anajua kama sheria zote zina mbana.

Sasa kwa sisi raia mara nyingi huwa tuko upande wa wanajeshi, na hii yote ni kutokana na matatizo tunayopata kwa kusababishiwa na polisi, kudhulumiwa, rushwa ndogo ndogo wanazochukua.
Ifike kipindi polisi waelewe majukumu yao na sio kutuonea sisi raia.
Ni imani yangu wakifanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, sidhani kama kutatokea tena kudharauliana.
 
...na mwanaume kamili halingishii uanaume wake kwa mwanaume mwenzake au vipi??
Ulienda mwenyewe polisi, hatukukutuma sisi, wewe fanya kazi yako kwa mujibu wa mkataba wako siyo kutisha tisha watu na uanaume wako
Hakuna alie kwambia mtu ni polisi ila nakufundisha wew mtoto mlaini acha kudharau watu wanaokufanya utembeze hicho kibamia chako mtaani bwege wewe
 
Dah nchi hii POLISI hata wakienda kikosi kizima kupambana askari wa JWTZ tena PRIVATE asiye na silaha wanaweza kufa WOTE.
Na wanabahati mwenzetu hajafa maana tungewafuata palepale FFU-Ukonga tukitumia askari wa AIRWING 603KJ Au Gongo la mboto 511KJ

Na niwaambie ukweli mchungu wanaJF msioelewa haya mambo ya kijeshi kuwa mjeshi anatibiwa na akipona anarudi kuendelea na kazi kama kawaida na pongezi atapewa za kutosha na muda sio mrefu atapanda na cheo.

Huu ni kweli mchungu,msiamini mtakacho tangaziwa kuwa kapewa adhabu kali.Ni uongo mkuu hata kama kesi itafika kisutu!
 
nimegundua huna ulijualo ww kasome tena UN walisemaje ?usiongopee watu nyie ndo mnaodanganyana vijiweni.
Nahisi kama wewe ungekuwa unalo ulijualo ungelifafanua hapa nasio ngebe ulizoleta na pili hao watu si tunaishi nao mtaani nidhamu na umakini wao si tunauona wewe ndo ukarudie kusoma ile ripoti

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
 
Dah nchi hii POLISI hata wakienda kikosi kizima kupambana askari wa JWTZ tena PRIVATE asiye na silaha wanaweza kufa WOTE.
Na wanabahati mwenzetu hajafa maana tungewafuata palepale FFU-Ukonga tukitumia askari wa AIRWING 603KJ Au Gongo la mboto 511KJ

Na niwaambie ukweli mchungu wanaJF msioelewa haya mambo ya kijeshi kuwa mjeshi anatibiwa na akipona anarudi kuendelea na kazi kama kawaida na pongezi atapewa za kutosha na muda sio mrefu atapanda na cheo.

Huu ni kweli mchungu,msiamini mtakacho tangaziwa kuwa kapewa adhabu kali.Ni uongo mkuu!
Mh! Sheria za wapi mnatumia?
 
Nahisi kama wewe ungekuwa unalo ulijualo ungelifafanua hapa nasio ngebe ulizoleta na pili hao watu si tunaishi nao mtaani nidhamu na umakini wao si tunauona wewe ndo ukarudie kusoma ile ripoti

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
Mkuu wee kubali uhalisia kuwa ile lugha iliyotumika hukuelewa kabisa,usitake kujiona unajua uhalisia wa maisha halisi ya hao watu ngoja nikuache.
 
Mkuu wee kubali uhalisia kuwa ile lugha iliyotumika hukuelewa kabisa,usitake kujiona unajua uhalisia wa maisha halisi ya hao watu ngoja nikuache.
Wewe si ndo unajua lugha iliyotumika fafanua hapa
 
Hakuna alie kwambia mtu ni polisi ila nakufundisha wew mtoto mlaini acha kudharau watu wanaokufanya utembeze hicho kibamia chako mtaani bwege wewe
Utakuwa hauko vizuri upstair, mimi silindwi na askari wala sijawahi kupewa escort na askari na hata kwangu hawajawahi kukesha wananilinda, so zungumza kama mwanaume usizungumze kama mwanamke kusifia sifia wanaume...
 
Utakuwa hauko vizuri upstair, mimi silindwi na askari wala sijawahi kupewa escort na askari na hata kwangu hawajawahi kukesha wananilinda, so zungumza kama mwanaume usizungumze kama mwanamke kusifia sifia wanaume...
Haaaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaa ngoja nicheke kwanza na elimu yako hyo ya 1+2= 12 ndio unajifanya uko juu bwana mdogo humu kila mtu akileta CV zake si utakimbia usimwambie mtu usiemjua hayuko vizuri upstair pambana na ujinga wako bwana mdogo

Jifunze kuheshimu kazi za watu na wewe utaheshimika,jifunze kutumia ulim vizuri nawe watu watatumia ulim wao vizuri juu yako

Ila inavyooneka wewe hakuna kitu kichwan mwako huwa unafikiria pale kibamia chako kinapo simama tu kisha lala hakuna jipya.
 
Usimwamin mtu yeyote ukiwa na silaha ya moto
Hivyo kwa kuwa hutakiwi kuamini inakupasa kumimina risasi tena hovyo...


Bora hata mngekuwa mnafahamu jinsi ya handle a gun na ku-hit a target....ona sasa mlivyojiabisha badala ya ku-hit target likaenda muua mwenzake...

Nyie polisi mlipjitokeza huku kutetea ndio mnaharibu kabisa.....
 
Back
Top Bottom