Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Yaani polisi bana, now wanauana wao kwa wao. Wanapambana na mtu asiekuwa na silaha then wanamimina risasi.
 
Well said njoo na jero nkupe mia tano
 
Kusema ukweli polisi kwenye lugha wanaboa!!...ina uma sana ...mtu anakuita....weeeeh Toka toka toka ......huku kakielekezea mtutu, hata ingekuwa mwanajeshi ningemnyoroshaa!
 
Tulishasema, hizi silaha kwa askari zinawapagawisha, yaani wanakuwa kama wamevuta bangi walahi...
Wakiwa na hizo silaha za moto...
  • Usiwabishie, hata kama watakuwa na makosa..
  • Hawapendi kuulizwa vitambulisho..
  • Usipite karibu yao..
  • Usiwatazame.
  • Uwaogope kama Miungu..
  • Wanabadilika ghafla, kichwani kwenye akili zao tayari wanajiona kama wamepewa leseni ya kuuwa au kujeruhi..
Yote haya ya nini, kuna haja..
  • Wakiwa na TRA wabebe silaha za moto?! Za nini?!
  • Kubeba masilaha ya moto kwenye maandamano?!
  • Kubeba silaha wakienda kudai bills za DAWASCO TANESCO n.k. n.k.??! Kwani hakuna vyombo vya sheria kuhakikisha mapato ya dola yanapatikana bila mtutu?!
Na hata tukilalamika bado hatusikilizwi, na dola haijali raia wake, wanaamini kutishia kwa mtutu wa silaha kuliko kujenga hoja au kutumia akili zao kupata haki ya kaisari, inasikitisha sana, hivi Mh, Mwigulu kweli anashindwa kutumia Phd kuwafundisha wenzake?!
 
Wanajeshi mafunzoni kwao wanafunzwa kudharau kz ya polisi ndy maana huyo mjeshi alikana hiyo amri. Wajeshi ni mazwazwa haiwezikani upo kiraia alfu unaleta ubabe. Wajeshi wote ni mazwazwa, mfano mzuri naona kwa babu yangu ni zwazwa wa kutupwa.
 
Wanajeshi mafunzoni kwao wanafunzwa kudharau kz ya polisi ndy maana huyo mjeshi alikana hiyo amri. Wajeshi ni mazwazwa haiwezikani upo kiraia alfu unaleta ubabe. Wajeshi wote ni mazwazwa, mfano mzuri naona kwa babu yangu ni zwazwa wa kutupwa.
walituambia UN kuwa wanajeshi wetu wana mafunzo duni na ndo maana kila uchao wanauwawa kule Kongo!!Mimi binafsi nimeishi kota za jeshi nimekaa karibu na kambi ya jeshi ni watu wa hovyo sana kuna kipindi pale mbeya washawahi kuleta vurugu kubwa sana kituo cha polisi iliyopelekea barabara kufungwa,biashara za watu kuharibika n.k.!eti kisa mwenzao kakamatwa kwa sababu alikuwa akiendesha pikipiki pasipo kuvaa helmet!!na hakukamatwa peke yake..
 
Wewe umesikitishwa na michango ya watu wanao watetea wanajeshi ila hapo juu unawatetea polisi ,sasa shida ni nini kama kila mtu kaamua kuwa upande wake ?

Hii dunia bana
 
wakati mwingine askari ukiwa kiraia uaskari unaacha nyumbani kabisa..sio umekutana na askari anafanya uaskar wake na wewe unaanza kuhoji moyoni hivi askari mzima ananipa kauli hizi inakuwaje?hapo shetani anaanza kukuingia na unaanza kujiona wewe nawe askari huwezi kukoromewa..


Alafu ajabu sana huyo askari wa jwtz hakuenda kozi kufundishwa kule depo si kunakuwa na matusi na kauli za vitisho kiasi kwamba ukitoka mafunzo hata mtu akupe kauli gani unaona kawaida??

nyinyi mnaolaumu niwaambie ukienda kozi huwa kuna waalimu wapigani na wanamatusi na kauli mbaya sana kwa recruit hii yote lengo ni kumfanya huyu askar akitoka awe mvumilivu huko mtaani kuepusha upuuzi kama huu ambao umetokea..

sasa huyu mwanajeshi hakupitia mafunzo haya au naye ni nanga tu???


pili kwa askar polisi siwezi kujua yalikuwa mazingira gani lakini kwa upande mwingine askar polisi ikiwa aliona huyo jamaa hana uniform basi alikuwa na haki ya kutoa kauli za command ili kumtoa kwa haraka eneo hilo... watu mnataka atumie ulaini hivi mnajua ulaini Unatumika wapi??

kwa sisis tuliopita moshi enzi hizo tunafahamu kwamba kuna customer care ambayo hasa ni vituoni ambapo askari anatakiwa kumsikiliza mteja aliefika kituoni kueleza shida yake na anatakiwa kuwa na kauli za kistaarabu..

sasa hii customer care huwezi tumia sehemu hatarishi kama hizo za benki ambapo kuna mtu mnamshuku


.sasa jamani mlitaka huyu askari anaesindikiza mzigo wa pesa naye awe na kauli za ki C.R.O ?

hamjui pesa zikiporwa askari naye anasokotwa???

basi ama ikiwa jamaa alikuwa na unifom basi nadhani hapo ndugu zetu GHASIA wangetumia komand ya kistaarabu mfano kumwambia. "kamanda fasta tuache tumalize mapango kisha utaendelea" kwa sababu ni askar mwenzie pia na askar hujuana bwana...


lakini pia nawasapoti wadau walosema jamaa hakutakiwa kuwa zero distance na huyo mwanajeshi kwa sababu ni hatari kimafunzo ya kijeshi kuwa zero distance na mtu asiejulikana katika mazingira kama hayo...


NIKO MBALI NA KILA ANAETOA POROJO AMBAZO ZIPO KICHUKI ZAIDI....
 
Hilo jamaa kwenye avatar yako ndio lile lilikuwa linatumiwa na Michael Corleone kwenye ishu zake za kutoa watu roho ?


Bora umeishia hapo usije ukanyonga mtu bure
 
Wewe umesikitishwa na michango ya watu wanao watetea wanajeshi ila hapo juu unawatetea polisi ,sasa shida ni nini kama kila mtu kaamua kuwa upande wake ?

Hii dunia bana
kutokana na hali ya eneo lile wale askari wana haki,katika mazingira kama hayo hatakiwi mtu yoyote kusogelea na hata kama atasogelea akipewa amri anatakiwa kutii asipotii tafsri yake ni kuwa yeye ni mharifu!!
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,kosa la askari ni kumsogelea yule mjeshi, alitakiwa ampige risasi akiwa mbali!!
 
Huo ni ukweli kabisa, umeelezea vizuri sana.
Askari mwenye mafunzo dhabiti hashindwi kumtambua askari mwenzie kwenye hali kama hiyo.
Polisi wamekosa elimu ya saikolojia hapo.

Walipaswa watumie akili zaidi kuliko nguvu. Huyo jamaa alikuwa peke yake na hana silaha yoyote iweje harakaharaka tu wahisi kuwa ni jambazi?
Alivyowambia watumie ustaarabu, polisi walitakiwa watambue huyo ni askari mwenzao.
 
naam hawa jamaa some times wanazungumza kisiasa sijui..

hawajui kama hata kama huna bunduki lakini ukiaratiwa na soja simama ukawa waja tu anapiga juu waja hapo mzee hata uwe uchi anakushuti tu na hana kosa kwa sababu alishakupa onyo simama..

lakini hawa jamaa sijui wamekaririshwa na wana siasa gani ...

unaweza ukawa mikono mitupu na ukashutiwa kabisa kwa sababu askar wana taratibu zao
 
Watu as research wafanye study ktk eneo la polisi na matumizi ya silaha za moto. Tujue shida ni nini
 
Akili zaidi inatakiwa itumike kwanza, si kutumia nguvu bila akili.
Unasema akitoa amri isipotekeleza (asipotii) ampige risasi, vipi endapo umetoa amri ya mdomo kwa mtu ambaye ni mlemavu wa kutosikia?...utamshoot tu bila kutumia akili kwanza?
Atumie akili kulingana na mazingira ya eneo alipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…