Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

UMESOMA STORY VIZURI? UMEAMBIWA TOKA SEHEMU YA ATM WATU WANAWEKA HELA,UNALETA UJEURI NA KUMNYANG'ANYA SILAHA FFU KISA NI MWANAJESHI?
Twende taratibu...nadhani wewe ndio hujasoma story vizuri....ama umesoma kwa kurukaruka..

Ilikuwa hivi...
karibu na mashine hiyo, kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine

Kisha Polis wa hovyo...akafanya hivi..
Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea
Kisha mwanajeshi asiye na silaha akafanya hivi baada ya kuona anelekezewa mtutu wa bunduki..
mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuw

Sasa kwanza umedanganya eti Mwanajeshi alitaka kumnyang'anya silaha...


Polisi mtendelea kudharaulika iwapo hamtabadilika....naona hata majibu yenu huku yamejaa mihemko tuu
 
Wewe hujawahi kukutana na hao Askari siku ukikutana nao utakuja kuanzisha thread humu wana maneno machafu sana hawana adabu kabisa
 
Pole kwa wafiwa, Mungu wa Majeshi awafariji katika hiki kipindi kigumu
 
Sawa ila wewe hujawahi kukutana na kauli zao unaweza ukaambiwa tena kwa kutukanwa matusi sasa mwanajeshi hawez kuambiwa lugha ya matusi ndo maana yametokea haya
 
Mr Policeman, huwezi kumkuta mtu anatoa pesa katika ATM hata kama unataka kuweka basi ukamtoa mkuku na kwa vitisho eti kwa vile unataka kuweka zingine. Lazima umwambie toa pesa na kadi yako kuna shughuli zingine zinataka kufanyika. Ni ujinga kumnyooshea bunduki mtu uliyemkuta ana fanya mambo yake kwa utulivu.
Hapa hata utetezi uweje, polisi walichemsha na mwanajeshi kwa vile anafahamu madhara ya kuonyeshwa mtutu akachukuwa hatua haraka. Au ulitaka aje kuwa kama Akwilina? Hongera Mwanajeshi kwa kujilinda, hatutaki kuwa na wanajeshi mdebwedo
 
Wewe hujawahi kukutana na hao Askari siku ukikutana nao utakuja kuanzisha thread humu wana maneno machafu sana hawana adabu kabisa
Mkuu nakubaliana na wewe....
Lakini hao wote ni kama nafaka ... tofauti ni majina tu..kunde ..maharage...mtama...ulezi!
 
sawa,
ila !
kwanini police amekua mwepesi wa kumuonyeshea bunduki raia?

ni wendawazimu askari kumuonyesha mtutu wa bunduki raia asie na siraha yoyote.

bunduki inatakiwa itumike wakati gani hasa unapokua ktk sehem yako ya ulinzi?

JIBU:-
Bunduki inatumika wakati adui yako akiwa na siraha pia.

kama una mashaka hasa labda anaweza kua nayo katika mavazi au mzigo ,basi hutakiwi kumsogelea adui ,ila unasimama mita kadhaa bila ya kumuonyesha mtutu mtu huyo,bali unaweza kumuita askari au hata raia kama wawili na kumpekua au avisalimishe mwenye vitu alivyobena.

HII NI KANUNI NZURI KWA ULINZI WA ASKARI WANAODILI NA ULINZI WA MAENEO YA RAIYA.PUBLIC.

ukiwa mwepesi wa kuonyesha mitutu raia unaowalinda ,kuna siku unamuonyeshea jeneral wako.
 
Mwanajeshi alikuwa na sare au la? hata hivyo alipaswa kutii amri iliyotolewa! nasikia aliesababisha hayo anashitakiwa kwa kusababisha kifo!! jamani hizi kazi busara muhimu!!
Hata kama angekuwa amevaa sare, kumbuka hata majambazi wanaweza kuvaa sare za jeshi. Kiufupi chanzo cha yote hayo ni ukaidi wa mwanajeshi huyo kwenye mambo ya msingi. Pia askari Polisi aliyerusha risasi hakuwa makini sana katika kuitumia silaha yake vema
 
Tatizo ni ubishi wa mwanajeshi. Kiutaratibu hatakiwi mtu yeyote (unauthorised) eneo hilo muda wa kuweka pesa. Askari wetu hawajui mipaka yao. Muda huu askari hushika silaha kwa utayari hivyo inaonesha mwanajeshi alivyosogelewa akawahi kuishika bunduki na kuielekeza juu. Mpaka hapo tayari ni vita na pengine angefanikiwa kuchukua lingetokea jingine. Ajali kutokea kwa ukaribu huo ni very probable ....chanzo cha yote ni ubishi wa kijinga ...
 
Sawa ila wewe hujawahi kukutana na kauli zao unaweza ukaambiwa tena kwa kutukanwa matusi sasa mwanajeshi hawez kuambiwa lugha ya matusi ndo maana yametokea haya
mkuu huu wako ni usingiziaji mkubwa sana kwa polisi...

hakuna hakuna hakuna ...eti matusi mkuu???
nakuambia tena hakuna askari ambae atakukomand kwa kukutukana..labda zile kauli we toka fasta potea na mfano wa hizo..lakini akuambie we fala toka hapo mkuu??

mkuu tuwe wakweli tu hilo haliwezi kutokea..

alafu nikuambie basi jeshini ukiwa kozi huwa kuna wale walimu mkuu wana kauli chafubza matusi na kauli mbovu mbovu wanazitoa kwa recruit inafikiri ni kwa nini mkuu??


ni kukujengea askari ukikutana na mfano wa kauli mbovu mtaani uwe umezizowea na uchukuliee kawaida tu usipanic..sasa huyo mwanajeshi inaonyesha alipanic baada ya kupewa amri na askar mwenzie kisha naona akaanza kujitathmini na hapo ndipo shetani akapata. chancee kila mmoja akajiona ndo yeye..

lakini kwa askari hasa hata angepewa kauli gani angeona kawaida na angewapisha wapite kutokana na mafunzo wanayopewa huko ni vigumu kumkuta anapanic ovyo
 
Sawa ila wewe hujawahi kukutana na kauli zao unaweza ukaambiwa tena kwa kutukanwa matusi sasa mwanajeshi hawez kuambiwa lugha ya matusi ndo maana yametokea haya
Ila yeye wanajeshi anaweza kumwambia na kumfanya mtu upuuzi....
Kisa nini?
Hilo ni funzo kuwa wanavyowaonea raia mtaani wajuwe kuwa wanaumia vile vile

Walikutana mwenye lugha mbovu na mwenye vitendo viovu!
 
Nasemaje wewe hujawah kukutana nao na sidhani kama ulichokiandika una uhakika nacho mimi nimeshakutana nao na nikiwa na mke wangu mpaka wife alishangaa kwa maneno machafu ila wakiwa wamevaa sare zao huwa jamaa wanaona Dunia ni ya kwao sasa nashangaa unachokataa kama ni Askari au una ndugu Askari lazima utetee
 
Mwanajeshi alikuwa na sare au la? hata hivyo alipaswa kutii amri iliyotolewa! nasikia aliesababisha hayo anashitakiwa kwa kusababisha kifo!! jamani hizi kazi busara muhimu!!
Je, ni kweli kwamba askari akipeleka fedha kwenye ATM analazimika kumfukuza mteja anayemkuta kwenye ATM husika au ndiyo kiherehere cha Jungle Green kufanya kazi zisizowahusu...
So far wenye pesa zao (i mean banks) wao huwa wanaamini kwamba fedha siyo muhimu kama uhai maana fedha zao zimekatiwa bima lakini hawa wanausalama wetu kwa kutaka masifa sometimes wana-exaggerate sana security issues wanaposafirisha fedha na kuzichukulia kiujiko ujiko sana. Sioni logic ya kumsogelea adui kiasi kile, kama alikuwa mwanajeshi chambo kuna uwezekano hata fedha zingeondoka na wakora pia na uhai wa wanausalama wetu wote ungekuwa mashakani.
Pole kwa wafiwa, ila kwa waliobaki hapo FFU Ukonga wajifunze kupitia kosa la mwenzao, unless otherwise death was calling him but the policemen did was wrong.
 
Daaaah pole sana mwanajeshi na sijui kwanini hakumnyanganya kabisa ile bunduki na kulenga yule pimbi aliyekuwa amebaki kwenye gari nawachukia sana hawa mbwa wa kaki ***** zao narudia tena pole sana mwanajeshi Mungu akufanyie wepesi upone haraka
hahahaha mkuu,kweli wewe unawachukia polisi nimeamini.....,wakipatikana watu 1000 tu kama wewe Tanzania itakuwa huru kutoka mikononi kwa hawa watu wanaonyayasa wenzao bila ya sababu msingi
 
ulikutana nao kwenye escot au ulikutana nao wapi mkuu???

tunachozungumza ni maeneo hatari mfano katika kusindikiza pesa kama hizo...

wewe UKnaleta matukio ya wapi mkuu??
 
Askari polisi hawa wawe hata 50 hawana uwezo kupambana na mwanajeshi mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…