Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 25,258
- 48,589
Hellow
Serikali imeingilia kati huduma za kiroho zitolewazo kanisa la WRM kivule maarufu kwa nabii Suguye mpaka sasa hawajatoa sababu maalumu ya kuzuia huduma hizo kusitishwa kwenye kanisa hilo.
Kwa upande wangu kama walivyo chunguza hilo kanisa na kugundua mapungufu yaliyopo basi wafanye hivyo kwa Mwamposa pia japo watu wanaosali huko kwa Mwamposa wakisikia unamponda watakujia juu as if walizaliwa huko.
Na baada ya hapo pia mchunguzeni pia Kuhani Musa nae ana jambo lake yule msihishie hapo tu piteni, na kwa Gwajima hawa watu wana kula hela za masikini acha leo tuwapazie sauti wanyonge hawa labda watatukumbuka huko mbeleni.
Mkalitazame na mnipe mrejesho nawasilisha.
========
Huduma za kiroho katika Kanisa la The Word of Reconciliation Ministries (WRM) la Kivule- Matembele ya pili, jijini Dar es Salaam zimesitishwa huku ulinzi wa Jeshi la Polisi ukiimarishwa ili kuzuia huduma yoyote isifanyike.
Huduma ya kanisa hilo lililo chini ya Nabii Nicolaus Suguye imezuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, huku waumini zaidi ya 4,000 wakidai kupewa maelekezo ya kutakiwa kutafuta maeneo mengine ya kuabudu.
Vyanzo vinaeleza kanisa hilo lilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo hazijapata usajili rasmi, isipokuwa barua ya usajili wa awali inayoruhusu kufanya huduma sehemu moja bila kualika wageni kutoka nje, kufungua matawi na kufanya makongamano huku Serikali ikifanya uchunguzi wa mwenendo wake.
“Baada ya uchunguzi wa mamlaka za usajili imeonekana huduma ya WRM imepungukiwa sifa za kupata usajili kamili, hivyo ikapewa notice ya kuzuiwa kuendelea na shughuli, ikisajiliwa ataruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya neno la Mungu,” kilieleza chanzo.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema kwa sasa anayelalamikia si yeye (Suguye) kwani yeye anajua kanisa halina usajili na anajua kwa nini amefungiwa.
Muliro alisema wao ni wasimamizi wa sheria na wanapaswa kuzilinda, “na kama (kufungiwa) ingekuwa ni kinyume cha sheria au taratibu unafikiri wenye kanisa wangekaa kimya? Kuna vitu haviko sawa kuhusiana na taasisi hiyo ya dini na lazima vitimie.”
Suguye, anayetambuliwa na waumini wake kama nabii, alianza kutoa huduma za kiroho mwaka 1998 kabla ya kuanzisha kanisa hilo mwaka 2007.
Kanisa hilo limefungwa ikiwa ni mwaka mmoja baada ya wizara hiyo chini ya ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa kutangaza mabadiliko ya hadhi ya vyeti vya usajili wa taasisi za kidini na jumuiya mbalimbali za kijamii inayoelekeza kuhuisha vyeti vya usajili kila baada ya miaka mitano.
Pia limefungiwa ikiwa ni miezi minne baada ya Nabii Suguye kuibua mjadala ufunuo wa kucha na nywele, akidai Mungu wake kuagiza waumini kutoa kucha za kidole cha mwisho cha kushoto (mguu na mkono) na nywele za utosini na paji la uso kisha kufunga kwenye kitambaa cheupe ili awaponye.
Kisheria ili kusajili taasisi hizo za kidini, mwombaji anatakiwa kuwa na nakala za katiba, kujaza fomu mbili yenye wasifu wa viongozi, muhtasari wa vikao, kulipia ada ya maombi ya usajili, ada ya usajili, ada na tozo ya kila mwaka baada ya kusajiliwa na kuwasilisha ripoti ya utendaji na fedha ya kila mwaka.