Ok.
Nimekuelewa..
Lkn Shehk mbona kajipa Kazi ya Mungu ya kuhukumu...???
Maana nakumbuka mwaka 1992 pale Mwembeyanga maduka ya nguruwe yalipochomwa moto,wakati serikali iliingiza FFU na Mbwa msikitini wkt wa Adhuhuri na kuwatandika waumini wa Kiislam kisawasawa kesho yake asbh viongozi wa Kiislam waliwakusanya waumini kwaajili ya kumsomea ALBADIRI wkt huo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Agaustine Lyatonga Mrema.
Mrema leo tunae na ni Mwenyekiti wa chama flani cha siasa.
Sijaona haja ya kiongozi wa heahima kama yule kumjibu Mange zaidi ya kumpuuza.
Hilo la kujipa nafasi ya kuhukumu, anyway... kwangu naona ni very complicated kuliko tunavyochukulia!!
Tusisahau, huyu sio mwanasiasa kwamba keshazoea kuoga matusi! Watu kama akina JPM wanafahamu kabisa kwamba kuoga matusi itakuwa ni sehemu ya maisha yao!!
Kinyume chake, huyu ni kiongozi wa dini... wala hana uzoefu wa kutukanwa hovyo hovyo tena bila sababu! Mbaya zaidi, ni mtu mzima! Halafu anaibuka mtu from nowhere na stori za uongo na kuanza kumwamgia matusi mazito mazito!!
Man, simuungi mkono suala la kuapiza lakini jaribu kuchukua nafasi yake! Nae ni binadamu... usitarajie eti kwavile ni kiongozi wa dini ndo basi wala haitamuuma kuambiwa mse'nge... tusi baya kuliko yote kwa mwanaume!
Suala la kumjibu Mange... naona ukisoma maoni ya watu wote yanaashiria kitu kile kile ambacho Sheikh amekisema! Kwamba, Mange anatumia matusi kama njia ya kuwatisha watu na kweli 99% ya watu wanamuogopa sana Mange kwa sababu tu ya kuogopa atawamwagia matusi!
Hatujui tu lakini ukweli ni kwamba Watanzania wapo vifungoni na aliyeshika funguo za Mahabusu ni Mange!! Na Mange hilo analifahamu ndo maana amejawa na kiburi kwa sababu tu anafahamu watu wanamuogopa kwa ajili ya matusi yake! Ni kwamba ameshapewa free pass ya "usimguse huyo... hivi unamjua vizuri wewe!!!"
Sheikh amegoma kuwa mfungwa!! Na amesema wazi kwamba watu walimuonya asimjibu kwa sababu atazidi kumwagiwa matusi! Sheikh Mkuu akagoma kuwa terrolized hata kama alifahamu haya yangetokea! Na kwenye Uislamu, kujitia unyonge wala sio sifa ya uchamungu!
Na hapa ndipo Waislamu wanapoonekana wakorofi manake kujitia unyonge kwao wala sio sifa!!